Ushawahi kumuuguza mtu mwenye matatizo ya akili?

Ushawahi kumuuguza mtu mwenye matatizo ya akili?

Yani Rebecca wewe ungekua daktari sisi vichaa tungepigwa marungu hadi tukome. Nimeona kichaa mwenzangu pale juu alikua anapita zake ukaanza kumfurumusha.

Hakuna kazi ngumu kama kuishi na mtu mwenye matatizo ya akili hasa kuishi naye nyumbani kwani usalama wenu unakua ni mdogo sana hasa kwa watoto wadogo. Humo ndani muda wote mnakua attention vitu vyenye silaha kali mnaficha, hamlali usingizi wa fofofo muda wote mnamhofia yeye, hasa wale vichaa wagomvi.

Na huu mwezi wa 11-12 ndio miezi yao ya kupandisha ukichaa, hapa jirani yetu kuna nyumba ina fence, ndani kuna mti mrefu sana sasa wakijisahau kuacha get wazi kuna kichaa huwa anaingia anapanda juu ya ule mti mpaka mwisho kwenye matawi anaanza kuimba, kushuka mpaka ajiskie yeye anaweza kupanda asubuhi akashuka jioni. Kuna nyimbo yake moja huwa anaimba.

Rebecca wanisumbuaa aaaeeeeehhhh
Rebecca wanisumbua aeeeee eeehhhe eeehhh
 
Sina uzoefu wowote wa karibu na tatizo hilo zaidi ya kuwaona tu, kuna mwaka mmoja 2000s nilikuwa kwenye daladala mkoa fulani hivi ghafla dada mmoja wa makamo aliyekuwa pembeni yangu alianza kuwa uncomfortable then kujikuna baada ya gari kusimama kwenye kituo yule dada alidrop kisha kuanza kukimbia hovyo na kuvua nguo zake zote hadi uchi wa mnyama, na hapo ndio ukawa mwanzo wa maisha yake ya kiuwendawazimu.

JE, UKICHAA UNATIBIKA?
I don't know exactly but i think inadepend na sababu yenyewe iliyopelekea mtu kutokwa na akili, wapo watu waliokuwa vichaa kutokana na drugs ,hata stress za maisha, hawa wakiwahiwa mapema kuna nafasi ya kupona , wale wakurogwa (we can't prove this scientifically ) wapo wanaoenda kuombewa na kupona (heard some of these cases) though ni mambo ya kiimani zaidi.

Kwa sababu nyingine sijajua kama kuna possibilities za kupona. And i think huu uzi ungekuwa kule kwenye forum ya afya labda kungepatikana msaada zaidi.
 
Ni ngumu. Nina dada, baada ya kujifungua ikawa inamkuta hali kama ana seizure hivi, yaani mnaweza kukaa hata miezi then ghalfa hiyo hali inakuja, kisha ataact weird, kipindi hicho mimi mdogo.

Mama yangu na baba ni watu wa dini kunizidi so wakawa wanampeleka kanisani. Ilikua ni kuombewa na kusema maneno ya kuashiria atapona karibuni.

Bibi upande wa baba inadaiwa ni mchawi, yeye akatupiwa lawama, dada akawa anakiri mbele ya madhabahu kua bibi na shangazi humfuata na kumfundisha uchawi, ila bibi alishafariki hatuwezi muuliza.

Kwa mapenzi ya mama kwa mtoto akaenda hadi kwa waganga. Haikua dawa. Hospitali haikua dawa pia. Naweza pigiwa simu kuambiwa amepigana na mama yako n.k. kuna siku niliwatembelea nyumbani nikiwa chumbani nikasikia mama anapiga kelele kumuita binamu yangu na mimi nikatoka nikakuta anataka kuwapiga wote wawili, nikaingilia, nikampiga, I am not proud of it, tho nimekua mtu anayemwogopa, yaani nikiwepo nyumbani anakua na heshima ila am not proud of it.

Ishu ni ndefu ila kifupi ni kua uvumulivu katika kuishi na mental case ni jambo la msingi.
 
JE UKICHAA UNATIBIKA?

Asante mkuu,wengi tunaowaona huko mabararani wakiokota makopo ama majalalani...hao ni waliwahi kuwa na ndugu zao hapo awali.. halafu wa 'Kapotea' hatuna mfumo sahihi wa kuweka Records ukute watu wanaokuwa wamepotea wanatafutwa na ndugu zao ni watu ambao wamepoteleaa kwenye Jangwa la ukichaa.,..very Sad.

Kutibika ndio nilitaka kujua Perceptions za watu..wanatumia au wangetumia njia gani..kama kuna waliokua successful watatumia au walitumia njia gani...

Mkuu hii sio topic ya jukwaa la Afya as natafuta perceptions tu za watu na sio kama nataka msaada per se..hafu kule kunatembelewa na wachache 😆 😉
 
Hakuna mtu kichaa duniani bali akili inaweza kuwa affected kwa namna mbili:

1. Kupitia ‘learning disability’ haya ni maradhi ambayo mtu anazaliwa nayo yanayomfanya kuwa na uwezo mdogo wa kujifunza vitu. Inategemea kujifunza inaweza kuwa uwezo wa kusoma na kuandika au hata namna ya kuweza kuishi kwa misingi ya kanuni za jamii.

Kwa sababu learning disability sio ugonjwa unaoponyeka kabisa umegawanya mara tatu kuna mild, moderate and severe. Hayo mawili ya mwanzo unaweza control ukiyagundua mapema ulaya kuna special schools ambazo hao watoto wanaenda na kufindishwa kuelewa vitu kwa njia zingine na wengi wanakuwa poa; severe ndio tatizo kwa sababu uja na multiple conditions na si ajabu medical conditions zikawepo ambazo zinamfanya mwathirika kuitaji msaada wa kuangaliwa maisha yake yote.

2 Psychological disorders huu sio uchizi haya ni madhara ambayo binadamu upata kutokana na life experience which affects their coping mechanism. Mfano mwanamke akijifungua kwa ugumu anaweza pata Post Natal Stress Disaorder ni vitu ambavyo vinahitaji therapeutic intervention tu wala sio uganga na dawa sometimes but the latter is a choice.

Sasa hizo psychological disorder ndio nyingi kweli kweli na vyanzo ni luluki but mainly life experience.

Mtu mwenye psychological disorder anaishi poa tu isipokuwa pale ambapo kuna serious condition kama schezophrenia ambapo huyo mtu anaweza jidhuru au anaweza dhuru wengine ndio anafungiwa kwa matibabu.

Ni vema kutoanzisha mada au kuchangia vitu ambavyo mtu unajua huna elimu navyo; kupitia michango ya humu ndani na picha kama kweli ndivyo Tanzania inavyotambua maswala ya mental health huyo Ummy Mwalimu ni wakutimuliwa maana ata vitu vingine vidogo tu kama kusimamia quality ya huduma za matibabu hawezi. Sasa ikija kwenye sera za kuelimisha jamii kuhusu maswala ya mental health na intervention zake trust me huko sio size yake.
 
Asante mkuu,wengi tunaowaona huko mabararani wakiokota makopo ama majalalani...hao ni waliwahi kuwa na ndugu zao hapo awali.. halafu wa 'Kapotea' hatuna mfumo sahihi wa kuweka Records ukute watu wanaokuwa wamepotea wanatafutwa na ndugu zao ni watu ambao wamepoteleaa kwenye Jangwa la ukichaa.,..very Sad.

Kutibika ndio nilitaka kujua Perceptions za watu..wanatumia au wangetumia njia gani..kama kuna waliokua successful watatumia au walitumia njia gani...

Mkuu hii sio topic ya jukwaa la Afya as natafuta perceptions tu za watu na sio kama nataka msaada per se..hafu kule kunatembelewa na wachache 😆 😉

Well, understood ! As i said early for my perception i think YES they can be cured ,kutegemea na chanzo cha tatizo lenyewe. 😐
 
Ni ngumu. Nina dada, baada ya kujifungua ikawa inamkuta hali kama ana seizure hivi, yaani mnaweza kukaa hata miezi then ghalfa hiyo hali inakuja, kisha ataact weird, kipindi hicho mimi mdogo.

Mama yangu na baba ni watu wa dini kunizidi so wakawa wanampeleka kanisani. Ilikua ni kuombewa na kusema maneno ya kuashiria atapona karibuni.

Bibi upande wa baba inadaiwa ni mchawi, yeye akatupiwa lawama, dada akawa anakiri mbele ya madhabahu kua bibi na shangazi humfuata na kumfundisha uchawi, ila bibi alishafariki hatuwezi muuliza.

Kwa mapenzi ya mama kwa mtoto akaenda hadi kwa waganga. Haikua dawa. Hospitali haikua dawa pia. Naweza pigiwa simu kuambiwa amepigana na mama yako n.k. kuna siku niliwatembelea nyumbani nikiwa chumbani nikasikia mama anapiga kelele kumuita binamu yangu na mimi nikatoka nikakuta anataka kuwapiga wote wawili, nikaingilia, nikampiga, I am not proud of it, tho nimekua mtu anayemwogopa, yaani nikiwepo nyumbani anakua na heshima ila am not proud of it.

Ishu ni ndefu ila kifupi ni kua uvumulivu katika kuishi na mental case ni jambo la msingi.

Pole Mkuu…

.nahisi hili eneo la Magonjwa ya akili..

halijawa priority kwa serikali zetu serikali zote zilizopita na ya sasa,

,..Haiwezekani tuwe na utitiri wa dispensaries na Refereal Hospitals for Physical diseases

na sio Mental health hospitals

..Sijui Until when kutakua na Muamsho?!!..but until then,some people with mental issues are going to suffer in Silence
 
Ni juzi tuu baada ya kukutana na mtu mwenye matatzo ya akili tulikua tunajalibu kueleweshana na rafk yangu.....

Yeye alikua anasema yule ni kichaaa,
mm nikamwambia sio kichaa ni taahira/zuzu...

Hapo ndio mazungumzo yakaendelea...

Yeye alikua anasema kichaa ni yyt yule ambaye kichwani akili hazipo sawa kulinganisha na binadamu wengne....

Mm nikamwambia,
Kichaa na taahira wote ni wagonjwa wa akili lkn wenye sifa tofauti...

Sifa kubwa ya kichaa ni usumbufu ktk hali ya kukera mpk watu wa pembeni
mfn... Kukimbiza watu, uropokaji, matusi, kuokota mauchafu, kutupia watu mawe, na mambo mengne meeengi ambayo ni ya kushangaza kwa binadamu ANGALAU mwenye akili timamu(elewe hio angalau)

Sifa kubwa ya taahira/zuzu ni upole, ukimya, kuzubaa, huyu nakosa lugha moja ya kumuelezea, yaani naweza sema ni ujinga uliopitilizaaa
mfn....kutililisha udendaa, ulegelege uliopitiliza, ukimya uliopitiliza au akiongea huna unachosikia wala kuelewa,
(vuta picha utanielewa tuu)..

Yaani wakati kichaa akipita mtaani kuokota makopo abebe mfukoni, taahira yy anakaa pembeni anaangalia jinsi kopo lilivyo,
kichaaa anapo ropoka na kutukana, huyu mda wote kakaa kimya hata umuongeleshe yy ni denda tuu...

kwa niliokutana nao mm
kitu nilichoshuhudia ni kua
kichaa ANAWEZA kua na usafi binafsi na pia kuna mda akili yake hua nzuri na pia kumpatia tiba akapona ni rahisi, nishashuhudia hili
Taahira muda krbn wote ni mchafu na sijawah ona taahira aliepona labda leo mniambie..

Upole na ukimya wa taahira unamfanya awe na hasira sana unapogusa maslahi yake, ndio kichaa ni msumbufu, anaweza akimbize mtu bila sbb, atupe mawe.....
Hio ni sehem ya maisha yakeee...
Lkn taahira akikutarget aloo hakuachiii....
Nasema hivi maana nakumbuka nipo drs la tatu nilikimbizwa na taahira krbn km 2 haniachii,
Mm nilikua natoka mbio yy mdg mdg tuu lkn kila nikisema nimchungulie huyu hapo, nalia, namwomba msamaha kwa kupga magoti, namrushia biskut, anakuja tuu, inabd niamke nikimbiee tenaa...
mpk tulipokutana na rafk yake akampoza wakarudi......
Sikusimama mpk home kufika nako nikazimaa....
Kosa lenyewe et nilikua nimebeba kidumu cha maji nikakipiga karibu yake 'paaaaaa'

Japo kumwita mtu kichaa kwa mtizamo wako, hili ni suala jingne kubwa sana,
 
Kwa mtu ambae kasoma psychology unapozungumzia mental health lazima upitie historical evolution na jinsi jamii ilivyokuwa inaelewa kuhusu hayo magonjwa na namna watu walivyokuwa wakisaidiwa tofauti kadri medical knowledge inavyozidi kuongezeka.

Ukisoma hii thread inaonekana Tanzania tuko bado karne ya 1700 kwa tafsiri za watu humu ndani kuhusu mental health.

Trust me kutibu mental health sio swala la medical intervention bali sera pia kama ‘social models’ ambazo ni inclusive na elimu pana kwa umma kuhusu hizo conditions hili jamii icheze part yake.
 
Wapo huwa wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao vizuri tu sema wanabaki na doa la kuwa alishaugua kichaa
 
Hakuna mtu kichaa duniani bali akili inaweza kuwa affected kwa namna mbili:

1. Kupitia ‘learning disability’ haya ni maradhi ambayo mtu anazaliwa nayo yanayomfanya kuwa na uwezo mdogo wa kujifunza vitu. Inategemea kujifunza inaweza kuwa uwezo wa kusoma na kuandika au hata namna ya kuweza kuishi kwa misingi ya kanuni za jamii.

Kwa sababu learning disability sio ugonjwa unaoponyeka kabisa umegawanya mara tatu kuna mild, moderate and severe. Hayo mawili ya mwanzo unaweza control ukiyagundua mapema ulaya kuna special schools ambazo hao watoto wanaenda na wengi wanakuwa poa; severe ndio tatizo kwa sababu uja na multiple conditions na si ajabu na medical conditions ambazo zinamfanya mwathirika kuitaji msaada wa kuangaliwa maisha yake yote.

2 Psychological disorders huu sio uchizi haya ni madhara ambayo binadamu upata kutokana na life experience mfano mwanamke akijifungua kwa ugumu anaweza pata Post Traumatic Stress Disaorder ni vitu ambavyo vinahitaji therapeutic intervention tu wala sio uganga na dawa sometimes but this is choice.

Sasa hizo psychological disorder ndio nyingi kweli kweli. Mtu mwenye psychological disorder anaishi poa tu isipokuwa pale ambapo kuna serious condition kama schezophrenia ambapo huyo mtu anaweza jidhuru au anaweza dhuru wengine ndio anafungiwa.

Ni vema kutoanzisha mada au kuchangia vitu ambavyo mtu unajua huna elimu navyo; kupitia michango ya humu ndani na picha kama kweli ndivyo Tanzania inavyotambua maswala ya mental huyo Ummy Mwalimu ni wakutimuliwa maana ata vitu vingine vidogo tu kama kusimamia quality ya huduma za matibabu hawezi sera za kuelimisha jamii kuhusu maswala ya mental health na intervention zake trust me sio size yake.

...I guess kama unaona hatujui then utuambie wapi tunakosea….and this is what this platform is for...

..Mie Sio daktarin ila ku classfy learning Disability as Mental health condition is wrong(My opinion regardless what DSM-5 says)..

..Again Schizophrenia tu be classified as Psychological condition in my opinion is wrong too..it is a Mental condition.One might affect the other..but its not the same thing....(Again is my opinion)

Wale wanaotolewa mapepo Kanisani,,,na wengine tunawaona wakikimbia marabarabarani..tunadhani ni Schizophrenia...kama unadhani ni condition nyingine then tuelimishe….
 
Habari JF,

Ningependa kujua subjective experiences zenu kuhusu kichaa.

Ushawahi kuumwa kichaa? Ushawahi kukumbana na kichaa? Ulijuaje huyu ni kichaa? Wewe au familia yenu mshawahi kuwa na kichaa? Mlienda wapi kutafuta msaada? Hospitalini? Kanisani? Kwa Mganga?

Alipona? Alipona kabisa, au alirudia kuumwa?

Nini mtazamo wako kifanyike kusaidia vichaa na familia zao, at Individual level, family support and at national level?

I know its a taboo subject, ila ningependa kuona uzoefu wenu. LETS TALK ABOUT IT hapa, tuko anonymous usiogope, kama vipi njoo na ID yako afu utiririke. 😂 😂

Ili mada yako ijadilike vizuri, nashauri kama unaweza uiboreshe, badala ya kutumia neno KICHAA utumie neno neno AFYA YA AKILI. Kama ulivyosema, its a taboo topic so kutumia hilo neno kunafanya mada iwe ngumu kidogo kujadilika ukichukulia ni ugonjwa na waadhirika ni ndugu, jamaa na marafiki zetu.

Ninachoweza kuchangia ni kuwa, tatizo la afya ya akili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na msongo wa mawazo, umasikini, unyanyapaa na bullying ... now, dawa kuu kuliko yote ni kupambana na nilivyovitaga hapo juu na kuongeza UPENDO.

Zaidi ya hapo kama hali hiyo imetokea, ni vizuri kumpeleka mgonjwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na si kutegemea maombi peke yake (very big mistake)

Asante
 
Back
Top Bottom