Sisi tuna ndugu alipata ugonjwa wa akili akiwa university pale Mlimani. Wenzake walisema alianza kuongea kupita kiasi wakati wa mijadala na hata darasani, akawa analazimisha kazi za group kuziwasilisha mwenyewe kwa niaba ya group, lakini alikuwa anakesha anaandika mambo marefu sana kuliko swali lenyewe na hata wakati wa presentation anataka atumie muda wote kuongea mambo yake. Akakosana na wenzake chuoni na hata walimu, na baadaye akaripotiwa kupotea. Baada ya wiki kama 3 za kumtafuta, akaonekana Mbagala akiwa mchafu sana, amekonda, anazurura hovyo mitaani. Akakamatwa akapelekwa hospitali Muhimbili wataalamu wakamtibu mwezi mzima akatoka msafi na akili zimerudi. Semester yote alibaki nyumbani akawa anaendelea na clinic Muhimbili, na baadaye chuo kikamruhusu kurudia mwaka.
Kufupisha, alimaliza kozi yake vizuri. Naamini nidhamu aliyozingatia ya kuhudhuria tarehe zote za clinic alizowekewa na kumeza dawa zake bila kukosa ilimsaidia. Sasa hivi ana kazi nzuri kule TCAA na ukimuona alivyo nadhifu huwezi kuamini amewahi kupata changamoto hiyo. Bado anazingatia matibabu yake, ana mke na watoto wanaosoma shule tofauti na kote wako very bright, ndio wanaoongoza madarasa yao.
kwa uzoefu huu nilioshea, nashauri sana kuwa wagonjwa wa akili wapelekwe hospitali katika vitengo maalumu vya magonjwa ya akili, na hata wakishatoka hospitali waendelee kupata support ya familia katika kuzingatia dawa na clinic schedules. Familia isiwanyanyapae, badala yake iwape nafasi ya kuonesha uwezo wao baada ya kupona. Huyo ndugu yetu ni mara moja tu alifikia hiyo hatua ya kuokota makopo, lakini tangu atoke hospitali haijarudia tena ilibaki hadithi tu kwa waliomuona wakati ule lakini sasa hivi hata ukisimulia jirani au wafanyakazi wenzake hawatakuamini, yuko safi kabisa. Hii hali inatibika, ni suala tu la kuzingatia matibabu na ushauri.