Ili mada yako ijadilike vizuri, nashauri kama unaweza uiboreshe, badala ya kutumia neno KICHAA utumie neno neno AFYA YA AKILI. Kama ulivyosema, its a taboo topic so kutumia hilo neno kunafanya mada iwe ngumu kidogo kujadilika ukichukulia ni ugonjwa na waadhirika ni ndugu, jamaa na marafiki zetu.
Ninachoweza kuchangia ni kuwa, tatizo la afya ya akili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na msongo wa mawazo, umasikini, unyanyapaa na bullying ... now, dawa kuu kuliko yote ni kupambana na nilivyovitaga hapo juu na UPENDO.
Asante
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mimi nimeomba poo mapemaaaYani Rebecca wewe ungekua daktari sisi vichaa tungepigwa marungu hadi tukome. Nimeona kichaa mwenzangu pale juu alikua anapita zake ukaanza kumfurumusha.
Hakuna kazi ngumu kama kuishi na mtu mwenye matatizo ya akili hasa kuishi naye nyumbani kwani usalama wenu unakua ni mdogo sana hasa kwa watoto wadogo. Humo ndani muda wote mnakua attention vitu vyenye silaha kali mnaficha, hamlali usingizi wa fofofo muda wote mnamhofia yeye, hasa wale vichaa wagomvi.
Na huu mwezi wa 11-12 ndio miezi yao ya kupandisha ukichaa, hapa jirani yetu kuna nyumba ina fence, ndani kuna mti mrefu sana sasa wakijisahau kuacha get wazi kuna kichaa huwa anaingia anapanda juu ya ule mti mpaka mwisho kwenye matawi anaanza kuimba, kushuka mpaka ajiskie yeye anaweza kupanda asubuhi akashuka jioni. Kuna nyimbo yake moja huwa anaimba.
Rebecca wanisumbuaa aaaeeeeehhhh
Rebecca wanisumbua aeeeee eeehhhe eeehhh
Mental condition na psychological condition ni kitu kimoja they are both induced. Psychology is another name for mental by definition....I guess kama unaona hatujui then utuambie wapi tunakosea….and this is what this platform is for...
..Mie Sio daktarin ila ku classfy learning Disability as Mental health condition is wrong(My opinion regardless what DSM-5 says)..
..Again Schizophrenia tu be classified as Psychological condition in my opinion is wrong too..it is a Mental condition.One might affect the other..but its not the same thing....(Again is my opinion)
Wale wanaotolewa mapepo Kanisani,,,na wengine tunawaona wakikimbia marabarabarani..tunadhani ni Schizophrenia...kama unadhani ni condition nyingine then tuelimishe….
Mkuu wewe ndio ufahamu kabisa kuhusu haya maswala bora usiwe unachangia unapotosha sana jamii.Yani Rebecca wewe ungekua daktari sisi vichaa tungepigwa marungu hadi tukome. Nimeona kichaa mwenzangu pale juu alikua anapita zake ukaanza kumfurumusha. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mimi nimeomba poo mapemaaa
Mental condition na psychological condition ni kitu kimoja they are both induced. Psychology is another name for mental by definition.
Learning disorder ni tofauti mtu anaerusha mawe bararani anaweza asijue namna sahihi ya kukabuliana na mtu anapokasirishwa. Huyu sisi tunasema kichaa wakati mtu ana matatizo ya uelewa na wasipopata elimu ya kuishi na watu mwishowe most people with learning disability upata na pyschological disorders ambazo jamii inachangia kwa sababu tunawachukulia vichaa wakati ni watu wenye akili timamu sema wana mapungufu tu ya kuelewa kanuni za kuishi na watu.
Ndio maana kuna aina tatu za learning disability classification mild, mild and severe. Sisi mtu mpaka anafika la saba awezi kusoma na wala kuandika tunasema ni mbumbumbu kumbe mtu dyslexia condition ambayo inamfanya awe mgumu wa kuweza kuelewa kirahisi jinsi ya kuunganisha sentensi na kusoma. Mtu anaweza kuwa mjeuri sana darasani kumbe ana autism atujuhi.
Sasa watu kama hao bila ya kuelewa matatizo yao jamii inaweza wapa label zingine na kupelekea kuwapa stress na magonjwa ambayo yapo related.
Ni hivi hili si swala la kujadiliwa na watu ambao not qualified.
Psychology is a jargon for mental (psyche) therefore the meaning is the sameThank you for your input on this topic,kuna vitu nimejifunza..lakini mnhhh
Ila wewe ni qualified, pale juu umeandika Learning Disability and then post yako ya chini umeandika Learning Disorder hivi sio vitu tofauti??????
Halafu mimi nilijua Mental health conditions ni magonjwa mengi..ila Psychological Disorders ni Psychology peke yake???
Psychology is a jargon for mental (psyche) therefore the meaning is the same
Disorder and disability in psycholohical contexts are the same things too; they are just used interchangeably.
Ukiingia humo ndani watakwambia mild and moderate learning disability ndio hazina cognitive impairment and acute learning disability ndio zenye kuathiri.
Ukiingia humo ndani watakwambia mild and moderate learning disability ndio hazina cognitive impairment and acute learning disability ndio zenye kuathiri.
Ni hivi usitegemee google tu kufanya reference unahitaji kulielewa somo zima la psycholology i.e all the perpesctive, how they differ and overlap.
Ukija huku kwenye maswala ya mental health ndio utaelewa kupitia perspective na mambo ya deviation sasa mtu una google vitu wakati ata fundamental bado ujazi master.
Mkuu wewe ndio ufahamu kabisa kuhusu haya maswala bora usiwe unachangia unapotosha sana jamii.
Me out
Mnhhhh hata sijui unakubali nini na unakataa nini,ndio natumia Google.lakini kama huoni differences then ngoja nibaki na mtazamo wangu na wewe baki na wako..Google wanakupa snap shot wewe ndio utafute kwengine...kama unatumia PsyINFO ni wewe..hatuandiki humu Papers humu...
Asante mkuu,wengi tunaowaona huko mabararani wakiokota makopo ama majalalani...hao ni waliwahi kuwa na ndugu zao hapo awali.. halafu wa 'Kapotea' hatuna mfumo sahihi wa kuweka Records ukute watu wanaokuwa wamepotea wanatafutwa na ndugu zao ni watu ambao wamepoteleaa kwenye Jangwa la ukichaa.,..very Sad.
Kutibika ndio nilitaka kujua Perceptions za watu..wanatumia au wangetumia njia gani..kama kuna waliokua successful watatumia au walitumia njia gani...
Mkuu hii sio topic ya jukwaa la Afya as natafuta perceptions tu za watu na sio kama nataka msaada per se..hafu kule kunatembelewa na wachache [emoji38] 😉
Ndugu naomba Ufafanue kwa kina. Inaelekea unafahamu Mengi sana Naomba Unisaidie Nijifunze zaidi.Kwanza naomba nikurekebishe kwamba kiswahili fasaha ni wagonjwa wa akili/magonjwa ya akili. Kwenye kamusi ya kiswahili hatuna msamiati wa kichaa. Kwa kimombo tunaita mental disorders/illnesses..
Haya magonjwa yamegawanyika katika makundi yafuatayo, soma kwa makini huenda na wewe msomaji umo kwenye kundi mojawapo:
1. Magonjwa ya Mhemuko (Mood disorders) kama vile unyogovu(depression) na mfadhaiko wa akili (bipolar disorder).
2. Magonjwa ya Wasiwasi (Anxiety disorders).
3. Magonjwa ya Kuvurugika Haiba ya Mtu (Personality disorders).
4. Magonjwa ya Kisaikolojia (Psychotic disorders) kama vile Schizophrenia.
5. Magonjwa ya Kula (Eating disorders).
6. Magonjwa ya Kiwewe (Trauma-related disorders) kama vile msongo wa mawazo baada tukio baya ama kusikitisha mfano ajali au kufiwa (Post-taumatic stress disorder).
7. Magonjwa yatokanayo na Kubwia Madawa ya Kulevya (Substance abuse disorders).
Kwa hiyo ukiangalia hizo categories kila mmoja wetu lazima ataangukia kundi fulani Japo unaweza usiwe na sifa zote za kuitwa mgonjwa wa akili.
Cc Unforgetable