Ushawahi kununua gari Be Forward?

Ushawahi kununua gari Be Forward?

We jamaa unazingua , unaponunua gari kuna vitu vya kuangalia
1. Bei ya CIF mpaka DAR
2. Ingia mtandao wa TRA weka details zote za gari unayonunua utapata makadirio ya gharama ya kulipa serikali
3. Weka gharama ya wakala atakayekutolea na kufanya clearance ya gari yako bandarini, ela ya plate number, bima, minure service
4. Weka ela ya emergence/contigency kati ya $500-1,000 kutegemea na ukubwa wa gari unayoagiza

Ukishajiridhisha na yote hayo na hela unazo, jaza details zako watakutumia invoice nenda kalipie bank, na bank watakukamua kati ya $45-50,
Usubiri gari yako ndani ya mwezi moja hivi itakuwa imefika bandarini
Wakishakutumia Bill of loading peleka nyaraka kwa clearance agency aanze mchakato wa malipo kabla gari haijafika kuepuka gharama zinazoweza kujitokeza plae unapochelewa kutoa gari bandarini baada ya kufika. Pia Befoward nao wanatoa huduma ya clearance unaweza kuwatumia ila gari itachelewa kutoka maana wana magari mengi kuanzia TZ, Congo, Zambia, etc za wateja wao wanaoagiza kwao. Ukishawalipa kinachotakiwa kaa nyumbani mpaka watakapokupigia ukachukue gari yako, pia watakupa na T-shirt yao ya Befoward
 
Back
Top Bottom