Ushawahi Kupokea muujiza gani ukaamini kuwa Mungu yupo?

Ushawahi Kupokea muujiza gani ukaamini kuwa Mungu yupo?

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Wakuu
kumekuwepo na mijadala mingi humu ya mivutano baina ya wanaokubali uwepo wa Mungu na wasioamini uwepo huo

Mungu mala zote ni mtenda miujiza,na amekuwa akifanya hivyo mala zote kwa waja wake, amekuwa akiponya magonjwa yaliyoshindikana,vipofu wanaona,viziwi wanasikia,viwete,bubu,wasio na kazi, watoto, mume,mke nk wote wamekuwa wakiuona mkono wa BWANA/ALLAH.

Tuambie mkuu, ulipokea muujiza gani kutoka kwa Mungu ukaamini uwepo wake?

KARIBUNI.
 
Niliwahi kua na deni nyeti sana, halafu mshahara hautoshi, yaani deni ni mara mbili ya mshahara, halafu mwenyewe kanikalia kooni hatari sana! Sasa nimejilaza nawaza hii issue nasolve vipi, mara paap, Boss kajichanganya kaweka mishahara miwili.. aisee! Hiyo siku niliamini Mungu yupo! Nilisolve kimeo halafu juma3 nikaenda kupambana na Boss.
 
Tarehe 31 March 1993 nilipata ajali ya kukatwa na kitu chenye ncha Kali kwenye maeneo ya Mshipa wa jugula lakini Kwa uwezo wa Mungu ijapokuwa nilivuja Damu kiasi cha shati nililovaa kuwa mithili ya dekio lililowekwa kwenye ndoo ya maji lakini sikufariki, Kwa hakika siku ile niliamini Mungu Yupo kupitia damu ya Yesu Kristo.
 
Wakuu
kumekuwepo na mijadala mingi humu ya mivutano baina ya wanaokubali uwepo wa Mungu na wasioamini uwepo huo

Mungu mala zote ni mtenda miujiza,na amekuwa akifanya hivyo mala zote kwa waja wake, amekuwa akiponya magonjwa yaliyoshindikana,vipofu wanaona,viziwi wanasikia,viwete,bubu,wasio na kazi, watoto, mume,mke nk wote wamekuwa wakiuona mkono wa BWANA/ALLAH.

Tuambie mkuu, ulipokea muujiza gani kutoka kwa Mungu ukaamini uwepo wake?

KARIBUNI.
Uhai
 
Mara nyingi miujiza inakuwa coincidences tu , imagine una nauli tu (hujui mchana utakula nini) ila unapanda mabasi mawili yaani kutoka Chanika mpaka Segera afu Segerea Mpaka Kawe na kote kuwili konda anasahau kukudai; unashuka kama ulivyopanda
 
Mungu gani mtoa miujiza ameshindwa na anashindwa kuwasaidia maelfu ya watoto na wanawake waliokufa na wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa, umaskini na majanga mbalimbali ya asili..!!!

Maelfu ya watoto na wanawake wamekufa sana hapa duniani, Na huyo Mungu mnayedai ni mtenda miujiza hajafanya chochote wala kusaidia lolote...👇View attachment 3259456View attachment 3259458
Huyo Mungu kama yupo hana msaada wowote wala muujiza wowote.

Huyo Mungu hafai kabisa anastahili kufurushwa huko alipo.
View attachment 3259455
Au huku Mungu kaua hawa watoto labda kuna kitu amekasirika mkuu🤔
 
Back
Top Bottom