Ushawahi Kupokea muujiza gani ukaamini kuwa Mungu yupo?

Freewill haipo.

Tunazaliwa bila kuchagua wala kutaka.

Hakuna freewill ya mtu kuchagua uzaliwe ama usizaliwe.

Unashtukia tu umesha zaliwa bila kuamua na bila kutaka.

Huu tayari ni uthibitisho tosha kwamba hakuna freewill.

Tunazaliwa kwenye dunia iliyojaa shida na mahangaiko ya kila aina bila kuchagua wala kupenda.

Freewill haipo.

Freewill is an illusion.
Au labda hao wanaokufa hawamtafuti kwa bidiii? Kwa sababu katika kitabu cha yeremia 29.13 ana sema

"Nanyi mtanitafuta na kuniona , mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote"
 
Miafrika bado tu toleo la Mwisho katika uumbaji...itoshe kusema udongo ulomfinyanga mwafrika ni wa kichuguu mabaki baada ya kuumbwa kumbikumbi na mchwa.
Wewe kweli ni Mamsosa🤣
 
Kitendo tu cha kubaki napumua nalala naamka mzima naenda kupambana hapa na pale kwa ajili ya malengo yangu huku baadhi ya niliolala nao jana nao wakiwa na malengo kama mimi hawajaamka huo ni zaidi ya muujiza.

Hivi vitu haviko kwa bahati mbaya na siyo wote waliopewa upeo wa kuyaelewa hayo.
 
Kitendo tu cha kubaki napumua nalala naamka mzima naenda kupambana hapa na pale kwa ajili ya malengo yangu huku baadhi ya niliolala nao jana nao wakiwa na malengo kama mimi siyo wote walioamka kama mimi huo ni zaidi ya muujiza.

Mkuu hata panzI anapumua,na hamjui wala kumwabudu Mungu, huwezi kusema kupumua ni muujiza,kupumua ni lazima na ukifa huo ulazima huisha,muujiza ni tendo ambalo haukutarajia katika maisha yako linatokea. ulikuwa hutarajii kuwa utakuwa unapumua?
 
Mara nyingi miujiza inakuwa coincidences tu , imagine una nauli tu (hujui mchana utakula nini) ila unapanda mabasi mawili yaani kutoka Chanika mpaka Segera afu Segerea Mpaka Kawe na kote kuwili konda anasahau kukudai; unashuka kama ulivyopanda
Aisee hii kuna siku nilikutana nayo nyuma huko mwaka 2011 ila mimi nilipanda matatu,Kariakoo to Mbezi,Mbezi to Shekilango na Shekilango to Sinza Kijiweni.

Though sikuwa na shida but kilichonifanya nisilipe nauli baada ya kusahaulika ni kauli mbaya na za kuchukiza za makonda kwa abiria,huyu watatu nilijisikia mwenyewe kumpa baada ya kuona ana kauli nzuri kidogo.
 
Mkuu hata panzI anapumua,na hamjui wala kumwabudu Mungu, huwezi kusema kupumua ni muujiza,kupumua ni lazima na ukifa huo ulazima huisha,muujiza ni tendo ambalo haukutarajia katika maisha yako linatokea. ulikuwa hutarajii kuwa utakuwa unapumua?
Unaifahamu lugha ya panzi wewe hadi ujue kama anamjua au hamjui Mungu?

So mshika dau toka unalala usiku ulikuwa guaranteed kwamba utaamka na ile pumzi uliyolala nayo jana mkononi leo?hongera sana but post yangu pale juu soma maneno niliyoandika pale mwisho utaelewa.
 
PANZI hakuja duniani kwa ajiri ya kumuomba Mungu, unapingana na maandiko ya dini yako mkuu.
 
Nikiwa nasoma UDSM, nilikuwa natoka likizo kurudi chuoni. Nilikuwa na mdogo wangu aliyekuwa anasoma chuo kingine.

Tukaingia kwenye basi, mdogo wangu akiwa ametangulia. Kwa kuwa basi lilikuwa tupu, mdogo wangu akakaa viti vya mbele. Mimi nilipoingia, nikamwambia aondoke alipokuwa amekaa, twende tukakae nyuma. Yule mdogo wangu alitii bila hata ya kuuliza. Na hata angeniuliza, wala sikuwa na jibu lolote, na hata mimi mwenyewe sikujua kwa nini nataka kwenda kukaa nyuma.

Tukaenda kukaa nyuma kabisa, kama mstari wa 3 tokea nyuma. Baada kama ya masaa mawili, basi lilipata ajali mbaya ya kugongana na lorry kubwa aina ya Fiat, kisha magari yote mawili yakashika moto. Madereva na watu wote kuanzia eneo la mbele mpaka karibia katikati ya basi ama walikufa au kuumia vibaya sana. Wengine waliungulia vibaya ndani ya basi.

Tulionusurika tulikimbizwa hospitali, baada kama ya masaa 8 ya uangalizi, niliruhusiwa kutoka hospitali.

Siwezi kusema kupona kwangu ulikuwa ni werevu wangu, bali Mungu alipenda niendelee kuishi.
 
Kuwa hai tu mpaka muda huu unasoma hii comment ni muujiza ndugu
amen
Kitendo tu cha kubaki napumua nalala naamka mzima naenda kupambana hapa na pale kwa ajili ya malengo yangu huku baadhi ya niliolala nao jana nao wakiwa na malengo kama mimi siyo wote walioamka kama mimi huo ni zaidi ya muujiza.

Hivi vitu haviko kwa bahati mbaya na siyo wote waliopewa upeo wa kuyaelewa hayo.
Amen
 
Nikiwa nasoma UDSM, nilikuwa natoka likizo kurudi chuoni. Nilikuwa na mdogo wangu aliyekuwa anasoma chuo kingine.

Tukaingia kwenye basi, mdogo wangu akiwa ametangulia. Kwa kuwa basi lilikuwa tupu, mdogo wangu akakaa viti vya mbele. Mimi nilipoingia, nikamwambia aondoke alipokuwa amekaa, twende tukakae nyuma. Yule mdogo wangu alitii bila hata ya kuuliza. Na hata angeniuliza, wala sikuwa na jibu lolote, na hata mimi mwenyewe sikujua kwa nini nataka kwenda kukaa nyuma.

Tukaenda kukaa nyuma kabisa, kama mstari wa 3 tokea nyuma. Baada kama ya masaa mawili, basi lilipata ajali mbaya ya kugongana na lorry kubwa aina ya Fiat, kisha magari yote mawili yakashika moto. Madereva na watu wote kuanzia eneo la mbele mpaka karibia katikati ya basi ama walikufa au kuumia vibaya sana. Wengine waliungulia vibaya ndani ya basi.

Tulionusurika tulikimbizwa hospitali, baada kama ya masaa 8 ya uangalizi, niliruhusiwa kutoka hospitali.

Siwezi kusema kupona kwangu ulikuwa ni werevu wangu, bali Mungu alipenda niendelee kuishi.
Amen
 
Nilikua nadaiwa ada wiki moja kabla ya UE, so jina langu likabandikwa kila kona ya chuo, nilikua sina namna ya kupata ada maana aliekua ananilipia ni mamangu, na alikua kalazwa kama mwezi mzima ndugu walikua wanamuuguza so awakuweza kunisaidia.
Sasa ikawa hata class siudhurii kwasababu ya mawazo, ilikua ijumaa lekcha akawa anaita watu wasaini kozweki nikaenda akaniuliza mbona ujafanya kwizi kama tatu, nkamwambia hali ya maza na deni nnalo daiwa, mzee wa watu akapiga simu nyumbani akamwambia mfanyakazi wake alete kiasi flani akanipa nikaenda kulipa ada.
 
Uhai hauna miujiza bhana, ni haki yako ya msingi. Hata majambawazi yapo hai.
 
nipo nasoma coments zenu endeleeni kutiririka msiniulize kuhusu mimi sina majibu
 
Wakuu
kumekuwepo na mijadala mingi humu ya mivutano baina ya wanaokubali uwepo wa Mungu na wasioamini uwepo huo

Mungu mala zote ni mtenda miujiza,na amekuwa akifanya hivyo mala zote kwa waja wake, amekuwa akiponya magonjwa yaliyoshindikana,vipofu wanaona,viziwi wanasikia,viwete,bubu,wasio na kazi, watoto, mume,mke nk wote wamekuwa wakiuona mkono wa BWANA/ALLAH.

Tuambie mkuu, ulipokea muujiza gani kutoka kwa Mungu ukaamini uwepo wake?

KARIBUNI.
Muujiza ni kitu gani?
 
Miafrika bado tu toleo la Mwisho katika uumbaji...itoshe kusema udongo ulomfinyanga mwafrika ni wa kichuguu mabaki baada ya kuumbwa kumbikumbi na mchwa.
Kuna matoleo mangapi ya watu?

Kila toleo limetoka mwaka gani?
 
Back
Top Bottom