Nikiwa nasoma UDSM, nilikuwa natoka likizo kurudi chuoni. Nilikuwa na mdogo wangu aliyekuwa anasoma chuo kingine.
Tukaingia kwenye basi, mdogo wangu akiwa ametangulia. Kwa kuwa basi lilikuwa tupu, mdogo wangu akakaa viti vya mbele. Mimi nilipoingia, nikamwambia aondoke alipokuwa amekaa, twende tukakae nyuma. Yule mdogo wangu alitii bila hata ya kuuliza. Na hata angeniuliza, wala sikuwa na jibu lolote, na hata mimi mwenyewe sikujua kwa nini nataka kwenda kukaa nyuma.
Tukaenda kukaa nyuma kabisa, kama mstari wa 3 tokea nyuma. Baada kama ya masaa mawili, basi lilipata ajali mbaya ya kugongana na lorry kubwa aina ya Fiat, kisha magari yote mawili yakashika moto. Madereva na watu wote kuanzia eneo la mbele mpaka karibia katikati ya basi ama walikufa au kuumia vibaya sana. Wengine waliungulia vibaya ndani ya basi.
Tulionusurika tulikimbizwa hospitali, baada kama ya masaa 8 ya uangalizi, niliruhusiwa kutoka hospitali.
Siwezi kusema kupona kwangu ulikuwa ni werevu wangu, bali Mungu alipenda niendelee kuishi.