Atoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 86,410
- 169,862
Mweeeh mweeh!Nililipwa kiasi kikubwa cha hela kwa ajili ya shughuli fulani,ila nikazifanyia shughuli tofauti,tajiri yangu akanisakama sana hadi niliposikia amefariki nikajua Mungu yupo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mweeeh mweeh!Nililipwa kiasi kikubwa cha hela kwa ajili ya shughuli fulani,ila nikazifanyia shughuli tofauti,tajiri yangu akanisakama sana hadi niliposikia amefariki nikajua Mungu yupo.
Check post #78Wapi? Weka link ya post ulipothibitisha hapa.
Unajuaje hii ni personal divine enconter na si ugonjwa wa akili tu unakufanya uone maruweruwe?Muujiza hautoshi kuthibitisha uwepo wa M-ngu,even devils can do miracles.
Kinacho thibitisha uwepo wa M-ngu ni personal divine encounter,yaani M-ngu mwenyewe anajifunua kwako kibinafsi,hakuna dini wala sayansi inatosha kuthibitisha uwepo wa M-ngu,it must be your personal divine experience,binafsi nimeshakutana na malaika 2 times na nime encounter na Mwana wa M-ngu 1 time,sihitaji mtu wa kunithibitishia,Mimi mwenyewe nimethibitisha.
haaah[emoji32][emoji46]Nililipwa kiasi kikubwa cha hela kwa ajili ya shughuli fulani,ila nikazifanyia shughuli tofauti,tajiri yangu akanisakama sana hadi niliposikia amefariki nikajua Mungu yupo.
LETA MUUJIZA WAKO MKUU PRAISETOTHEMOSTHIGH kuthibitisha uwepo wake.God is good all the time,I dare not to mock his presence.
Nimejua kulingana na upeo wangu.Unajuaje hii ni personal divine enconter na si ......
Huo upeo wako unauhakiki vipi?Nimejua kulingana na upeo wangu.
Huyo atakuwa anaburuzwa asijue anaabudu nini,amejaribu kuleta utetezi wake kutetea asichokijua,ila amepigwa maswali ameshindwa atetee vipi, watu wa namna hii tunao katika jamii,na ukute katika mtaa wao yeye ndiye mwenyekiti,wanamwamini kuwa mzee wenye hekima na maarifa, ila humu tunamwona kana kwamba ni mmoja wa member asiye na mchango wowote jukwaani. Kiranga Tanzanian DreamSi unaona mkuu?
Yani mtu anashusha viwango vya mazungumzo mpaka unatamani usimjibu tu.
Sasa mtu anayekujibu kama guluguja asiye na ubongo wala uti wa mgongo ukimbeza utakuwa umekosea?
Apuuzwekiranga anaweza kuwa ni freemason yule, 😂 mtu gani haamini Mungu licha ya vyote vilivyomo duniani 😂
Vip mdogo wako naye?
Mungu ni mkuu sana.Mdogo wangu naye alipona.
Magari baada ya kugongana, kabla ya kushika moto, basi liliendelea kubiringida mpaka kwenda kutulia nje ya barabara ambako kulikuwa na moto unawaka kwenye nyasi. Mimi na jamaa mmoja tulikuwa wa kwanza kutoka, tukipitia upande wa juu kwenye dirisha lilivunjika. Mara baada ya kutoka, nilikazana kuzima moto kwenye nyasi kwa kutumia matawi, lengo nikitaka niingie kumtafuta mdogo wangu. Mara kwa mbali, tulikotokea nikamwona mdogo wangu anakuja. Kumbe yeye alirushwa nje ya basi kupitia nyuma ambako kulikuwa kumebomoka. Yeye hakufika nasi kule mwishoni.
Mara baada ya kumwona, nikaishiwa nguvu, nikaa chini, moto ukalifikia basi, likashika moto. Moto ukawa mkubwa kiasi cha kuzuia mtu yeyote kulusogelea. Mdogo wangu sijui aligongwa na kitu gani, alikuwa amevimba kwenye paja, lakini alikuwa anatembea kwa kuchechemea. Mimi nilijaa dakuwa na jeraha lolote la kuonekana,sana.
Mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitisha Mungu yupo.
Mungu ni mkuu sana.
Imani si uthibitisho.Miujiza siyo uthibitisho pekee wa uwepo wa Mungu. Uwepo wa Mungu na yale anayotuagiza kwa njia ya manabii wa kale ni masuala ya imani. Jambo lolote la kiimani halithibitishwi kwa majaribio ya kisayansi.
Kutoamini kuwa Mungu yupo, wewe huwezi kuwa wa kwanza, hata hapo kale walikuwepo, na inathibitishwa kwenye biblia:
Zaburi 53:1
Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema.
NB: Kuanzia pale uwezo wa mwanadamu unapoishia, ndipo ukuu wa Mungu unapoanzia.
Mwanasayansi mmoja alikuwa akidai kuwa Mungu hayupo. Akaambiwa aeleze mwanzo wa mwanadamu ni nini? Akasema mwanadamu alitokana na wazazi wa kale. Akaulizwa na hao walitokana na nini? Akasema hao watakuwa walitokana na cells zilizo-undergo evolution ya muda mrefu. Akaulizwa na hizo cells zilitoka wapi? Akasema, there must be a power without which nothing can be done. Wanateolojia wakamwambia, hiyo POWER ndiyo MUNGU mwenyewe.
"aheri anayeamini bila kuona'