Ushawahi Kupokea muujiza gani ukaamini kuwa Mungu yupo?

Ushawahi Kupokea muujiza gani ukaamini kuwa Mungu yupo?

Mungu yupo, amini usiamini hainihusu....

Nasema pokea sifa na utukufu Mungu 🙏
 
Ukiwachunguza wanatoa ushuhuda wa muujiza waliokutana nao wakaamuni mungu yupo, utakutana nao jumapili wanaomba toba mbele ya mifuko miwili ya cement iliyochanganywa na kokoto
downloadfile.png
 
Mdogo wangu naye alipona.

Magari baada ya kugongana, kabla ya kushika moto, basi liliendelea kubiringida mpaka kwenda kutulia nje ya barabara ambako kulikuwa na moto unawaka kwenye nyasi. Mimi na jamaa mmoja tulikuwa wa kwanza kutoka, tukipitia upande wa juu kwenye dirisha lilivunjika. Mara baada ya kutoka, nilikazana kuzima moto kwenye nyasi kwa kutumia matawi, lengo nikitaka niingie kumtafuta mdogo wangu. Mara kwa mbali, tulikotokea nikamwona mdogo wangu anakuja. Kumbe yeye alirushwa nje ya basi kupitia nyuma ambako kulikuwa kumebomoka. Yeye hakufika nasi kule mwishoni.

Mara baada ya kumwona, nikaishiwa nguvu, nikaa chini, moto ukalifikia basi, likashika moto. Moto ukawa mkubwa kiasi cha kuzuia mtu yeyote kulusogelea. Mdogo wangu sijui aligongwa na kitu gani, alikuwa amevimba kwenye paja, lakini alikuwa anatembea kwa kuchechemea. Mimi nilijaa damu maeneo mengi lakini siyo kutoka kwenye mwili wangu, ni za watu wengine. Sikuwa na jeraha lolote la kuonekana, japo nilikuwa nasikia maumivu ya wastani kwenye kifua. Vipimo vyote vilionesha sikuvunjika sehemu yoyote.
Mungu ni muweza.
 
Mkurugenzi fulani aliniachisha kazi bila sababu ya msingi kumbe alikuwa na mtu wake niliumia mno nkamuuliza Mungu ntaishije ..kwa nn hili limetokea nimekosea wapi ..Tramp akafanya yake saivi kawa jobless kweli Mungu yupo na anajibu kwa wakati
 
Shida ya kiranga na wafuasi wake wanataka kulinganisha spiritual world na material world kitu ambacho hakiwezekani abadani.

Spiritual world iko dominated na faith, na faith zote zimeelekezwa kwa Mungu kama Mfalme wa watu wamuaminio.

Imani ndiyo silaha ya binadamu wote haijalishi unaamini katika kitu gani ila iman yako ndiyo chanzo cha mwenendo mzima wa tabia, matendo na maisha ya binadamu kwa ujumla.

Imani huleta tumaini.
Imani huleta amani na utulivu kwa binadamu.
Imani humsukuma binadamu kuamka hasubuhi na kuamini kuna kitu kinachomsukuma aamke akafanye kitu akiamini anaweza kukitimiza na kikaleta manufaa kwenye maisha yake.

Kuamini katika Mungu kunatokana na jinsi mtu alivyoikuza imani yake na namna imani yake inavyofanya kazi.
Wengi wenye imani juu ya uwepo wa Mungu tunaamini Mungu ndiyo ameumba ulimwengu na viumbe vyote vilivyomo kutokana na complexity ya viumbe vyenyewe, nikiwa na maana kwamba haikuwa rahisi hivi vitu katika ulimwengu kutokea vyenyewe tu bali kuna alieviunda ndiyo maana tunaamini Mungu ndiye ameviumba.
Huenda tafsiri ya neno Mungu inapelekwa kuwa ni kiumbe kama binadam ndiyo maana watu wanacomplain wakitaka kumuona, la hasha Mungu ni nguvu iliowezesha vyote kuwa hapa vilovyo na nguvu hiyo wajuzi wa mambo wa kiroho wanaamini inasifa kama za kibinadamu ikiwemo kuona na kusikia ndiyo maana inasemekana tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, ndiyo maana tunaambiwa tuabudu na kusifu nguvu ya kiungu hupenda matendo kama hayo.

Kiranga yeye ni mtu anaeamini katika material world na science, anachokitaka yeye ni kulonganisha spiritual world ifanane na material world, kwa kuwepo na facts, evidences ili aprove kila kitu.

Spiritual world ni ulimwengu wa vitu intangible, ila hisia na imani ndiyo nyenzo kuu ya kuishi ndani yake.

Naweza kuuliza je binadamu hana roho?
Je kuna mtu anaweza kuishika roho?
Je binadanamu hatumii oxygen?
Kuna mtu anaweza kutuonesha oxygen tukaiona kwa macho tuiprove kwamba ndiyo hii?
Kwahiyo dunia ndivyo ilivyo, imegawanyika katika sehemu mbili na moja ni invisible world nyingine ni visible world.

Mungu ni King wa watu wanaoamini katika spiritual world haimaanishi kwamba hayupo.
Yupo ila spiritually.
 
Kitendo tu cha kubaki napumua nalala naamka mzima naenda kupambana hapa na pale kwa ajili ya malengo yangu huku baadhi ya niliolala nao jana nao wakiwa na malengo kama mimi hawajaamka huo ni zaidi ya muujiza.

Hivi vitu haviko kwa bahati mbaya na siyo wote waliopewa upeo wa kuyaelewa hayo.
aise toa ufafanuzi wako juu ya hili.
 
Back
Top Bottom