Ushawahi kuwa na mwanamke anayenuka kikwapa? Nampenda ila ananuka kwapa

Perfume ipo nipe order nikuletee tu
 
Hahaha. .... aisee.
 
kuu huu ni utaratibu tu wa usafi sio dawa ya kikwapa

Nafikiri wengi hawajakutana na wenye hii shida ni ngumu kuelewa, mimi pia sikuwai kukutana na mwenye hali hii before.
Kuna jamaa tulisoma nae sekondari alikuwa ananuka kikwapa sio kawaida akiingia hata ukumbi wa shule wa kubeba watu hata mia nane utajua jamaa kaingia. Siku moja tunaoga mtoni vidume wengi mimi nikasema wacha nimchore jamaa anavyooga. Asee nikagundua jamaa ni mvivu kuoga na hafati kanuni za kuoga. Nikatafuta muda nikakaa nae akanieleza tatizo lake la kutopenda kuoga. Nikamueleza namna ya kuoga na mtego (dodoki ) yale ya mtego wa samaki nikampatia. Kilichofata hadi waalimu walinishukuru jinsi nilivyomsaidia. Ile harufu ilimuisha kabisa.
 
Kama hataki deodorant basi kazi unayo.

Pia ajaribu kutumia ndimu/limao ukisugulia kwapani inasaidia kukata harufu.

Ila ongea nae kwa utaratibu, wengine wana nongwa
 
Yeye mwenyewe na wanafunzi wenzako hawakukushukuru??!!

Ila Kikwapa halisi hakiondoki kwa dodoki.
Yeye ananishukuru hadi leo wanafunzi walijua mimi ndo nimemsaidia. Waalimu walishamjua tatizo lake ila walishindwa namna nzuri ya kumsaidia. Nakumbuka madam mmoja yy alikuwa akimuona jamaa anaanza kumtukana na kumkejeri kwa jinsi anavyotoa harufu. Madam alipojua alinishukuru sana.
Infakiti wanakupa vikwapa wengi ni wavivu wa kuoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…