Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Revola

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2015
Posts
1,516
Reaction score
1,338
Wakuu, habari za jioni,

Katika maisha, mtu anaweza kuwa na kariba ya kawaida kabisa kiasi cha mtu mwingine kutojua au kutozoea tabia yake, hali inayoweza kusababisha kudharauliwa. Hata hivyo, baadaye watu hao huweza kugundua kwamba mtu waliyemdhani si wa kawaida kabisa na mawazo yao yanabadilika.

Iliwahi kunitokea siku moja nilipoenda ofisi fulani na kuwakuta wafanyakazi wote wakiwa wanawake. Nilipowasalimia, mmoja tu alijibu, tena kwa nyodo sana. Nilipowaambia kwamba nilihitaji bahasha zilizoachwa na bosi wao, waliniangalia kwa dharau. Wakati huo, nilikuwa nimevaa mavazi rahisi—pensi na sandle—na waliniuliza, "Wewe unazichukua kama nani?" Nikajibu kuwa nimeagizwa, lakini bado walinidharau na kuniambia, "Haya chukua, wahi daladala zimejaa sasa hivi."

Kumbe nilikuwa nimekuja na BMW nje ya ofisi. Walipokuwa wakijiandaa kuondoka, nikashuka ngazi na kwenda kwenye gari langu. Nilipofika kwenye eneo la kuegesha, walionekana kushangaa. Kwa heshima, nikawaambia, "Ingieni niwasogeze." Walikubali, lakini ndani ya gari walikuwa kimya kama wamemwagiwa maji. Walianza kucheka na kutabasamu huku wakifurahia upepo wa AC. Mmoja aliyekaa mbele aliniomba namba yangu ya simu, lakini sikufanya juhudi zozote za kuendelea mazungumzo naye, nikalipotezea tu.

Je, wewe umewahi kudharauliwa na watu, familia, au marafiki kutokana na mwonekano au hali fulani katika harakati za maisha?
 
Mimi kazi yangu ina jina kubwa sanaa.Sasa watu wanafikiri nalipwa mamilioni masikini ya Mungu ,kumbe nakunja mia tisa na chenji kabla ya makato mpaka kurudi laki nne na kitu mfukoni.Basi watu mara waniombe niwaazime milioni kumi,mara niletewe prado linauzwa,mara mgeni rasmi wa kuongoza harambee.Kadi za harusi ndio hazina idadi.Kumbe ni masikini mwenye jina kubwaaaa.
 
Mzee wa kanisa?
 
Japo nilimbembeleza Sana anihudumie lakini alikataa kata kata,kisa aliniambia nisubiri nje ataniita aliponiita sikumsikia nikasubiri weee,nilivyoona muda unazidi kwenda nikamfuata vipi mbona huniiti ndo akaniambia aliniita sikwenda hivyo hanihudumii!! Bembeleza wapi ukiangalia hapo nimeshapoteza muda mrefu kumsubiri na inshu ilipaswa kuisha siku hiyo hiyo,baadae ndo akajitokeza dada mmoja akanifanyia inshu yangu fasta tu hata dakika tano hazikuisha nikaondoka zangu!
Inaendelea au?! Acha pombe
 
FB_IMG_1719557793598.jpg
 
Japo nilimbembeleza Sana anihudumie lakini alikataa kata kata,kisa aliniambia nisubiri nje ataniita aliponiita sikumsikia nikasubiri weee,nilivyoona muda unazidi kwenda nikamfuata vipi mbona huniiti ndo akaniambia aliniita sikwenda hivyo hanihudumii!! Bembeleza wapi ukiangalia hapo nimeshapoteza muda mrefu kumsubiri na inshu ilipaswa kuisha siku hiyo hiyo,baadae ndo akajitokeza dada mmoja akanifanyia inshu yangu fasta tu hata dakika tano hazikuisha nikaondoka zangu!
Hadithi yako inatufundisha nini kulingana na mada husika
 
Mimi kazi yangu ina jina kubwa sanaa.Sasa watu wanafikiri nalipwa mamilioni masikini ya Mungu ,kumbe nakunja mia tisa na chenji kabla ya makato mpaka kurudi laki nne na kitu mfukoni.Basi watu mara waniombe niwaazime milioni kumi,mara niletewe prado linauzwa,mara mgeni rasmi wa kuongoza harambee.Kadi za harusi ndio hazina idadi.Kumbe ni masikini mwenye jina kubwaaaa.
Hii ndo inayonitokea mpaka nimepoteza baadhi ya watu makini sana katika maisha yangu kwa kudhani nina roho mbaya sijali ukaribu wetu kisa tu walipokuja kunikopa mamilioni niliwaambia sina 😂😂😂 wangejua mi mwenyewe kajamba nani wangenionea huruma maskini ya Mungu 😂 kweli usione ukadhani!!
 
Back
Top Bottom