Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Wakuu, habari za jioni,

Katika maisha, mtu anaweza kuwa na kariba ya kawaida kabisa kiasi cha mtu mwingine kutojua au kutozoea tabia yake, hali inayoweza kusababisha kudharauliwa. Hata hivyo, baadaye watu hao huweza kugundua kwamba mtu waliyemdhani si wa kawaida kabisa na mawazo yao yanabadilika.

Iliwahi kunitokea siku moja nilipoenda ofisi fulani na kuwakuta wafanyakazi wote wakiwa wanawake. Nilipowasalimia, mmoja tu alijibu, tena kwa nyodo sana. Nilipowaambia kwamba nilihitaji bahasha zilizoachwa na bosi wao, waliniangalia kwa dharau. Wakati huo, nilikuwa nimevaa mavazi rahisi—pensi na sandle—na waliniuliza, "Wewe unazichukua kama nani?" Nikajibu kuwa nimeagizwa, lakini bado walinidharau na kuniambia, "Haya chukua, wahi daladala zimejaa sasa hivi."

Kumbe nilikuwa nimekuja na BMW nje ya ofisi. Walipokuwa wakijiandaa kuondoka, nikashuka ngazi na kwenda kwenye gari langu. Nilipofika kwenye eneo la kuegesha, walionekana kushangaa. Kwa heshima, nikawaambia, "Ingieni niwasogeze." Walikubali, lakini ndani ya gari walikuwa kimya kama wamemwagiwa maji. Walianza kucheka na kutabasamu huku wakifurahia upepo wa AC. Mmoja aliyekaa mbele aliniomba namba yangu ya simu, lakini sikufanya juhudi zozote za kuendelea mazungumzo naye, nikalipotezea tu.

Je, wewe umewahi kudharauliwa na watu, familia, au marafiki kutokana na mwonekano au hali fulani katika harakati za maisha?
Hapana
 
Aisee, ni majuzi tu nimenunua kijumba flani hvi Chenye vyumba vinne vya wapangaji Kodi elfu 40. Sasa bwana ikatokea mpangaji mmoja akawa ametoroka siku ambayo kaahidi kunilipa kodi bila mimi kujua.

Sasa siku hiyo asubuhi nipo kijiweni na wana sina hili wala lile simu inaingia kupokea ni sauti ya kike, demu anabembeleza anataka chumba ameshaoneshwa kakipenda sasa mimi namuuliza chumba gani hiko tukawa hatuelewani, akanipigia tena nikamuelewa basi nikawa nimengamua jamaa wa kile chumba kahama na dalali wamempeleka huyu binti akaone hko chumba.

Yule dada akawa anabembeleza kwa adabu kubwa anaomba aanze na kodi ya miezi miwili kutokana na hali yake si nzuri nikawa nimemkubalia tukapanga jioni tuonane anilipe hiyo hela baada ya kazi.

Jioni ikafika akanielekeza mahali alipo na mimi muda huo nilikuwa nakunywa pombe na wanangu basi chaapu nikachukua pikipiki yangu chafuchafu hadi eneo alipo huyo dada, nikafika pale na kwa namna alivokuwa amesimama ile waiting mood nikawa nimejua ni yeye nikawa nimempita kidogo nikapaki fupa langu nikaanza kazi ya kumuita sasa, kila nikimuita yeye ndo kwanza hanisikii yupo bize na simu yake huku anatingisha nywele, kila nikimuita ananiangalia tu sometimes ananiangalia chini hadi juu, mwisho wa siku akanambia wewe kaka hebu sema shida yako ukiwa hapo nakusikia. Basi ikanibidi nijishushe sana ndiyo akasogea. Nikaanza kumlaumu si vizuri kumdharau mtu namna hiyo, akaanza maneno ya Shombo na dharau.
Kwa utaratibu na unyenyekevu mkuu nikamwambia mimi ndo yule mwenye nyumba umenambia tukutane hapa!!! Yule demu aliona aibu sana akaanza kunishangaashangaa....nikachukua afu 80 nikasepa zangu.....
 
Mimi kazi yangu ina jina kubwa sanaa.Sasa watu wanafikiri nalipwa mamilioni masikini ya Mungu ,kumbe nakunja mia tisa na chenji kabla ya makato mpaka kurudi laki nne na kitu mfukoni.Basi watu mara waniombe niwaazime milioni kumi,mara niletewe prado linauzwa,mara mgeni rasmi wa kuongoza harambee.Kadi za harusi ndio hazina idadi.Kumbe ni masikini mwenye jina kubwaaaa.
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Haya mambo yapo ila yako ni
downloadfile.jpg
 
Kanisani kwetu walikuwa wananichukulia poa,siku amekuja pastor mzungu mimi ndio nikawa natafsiri English to swahili
Baada ya hapo kanisani hadi watoto wadogo waliniheshimu
NB English ya kwenye biblia msiichukulie poa ni noma
 
Nilijiungaga na kikundi fulani cha kidini.Walikua wabaguzi kwa wageni.Baada ya miezi kadhaa siku moja nikaenda na kimkweche changu.
Wakanipa hongera kwa kununua gari,nikawaambia sio mpya ninayo siku nyingi.

Hata hivyo siku hiyo nilishangaa,kusikitika na kujifunza kitu.
Wale walokole bila aibu walionesha upendo mkubwa sana kwangu
😂😂😂 watu wanakuheshimu kutokana na vitu ulivyonavyo
 
Mimi bwana ni mtu ambaye sipendi kutumia cheo cha mtu au nafasi ya mtu kupata unafuu

Sasa kuna kipindi nilimuwekea dereva mmoja dhamana hlf akakimbia,dah ikabidi niwekwe mimi ndani,ilikuwa pale kituo cha msimbazi miaka ya nyuma,baba yangu alikuwa mkuu wa wilaya,basi bwana nikawekwa ndani kwa masaa kama matatu,baadae mshua anakuja ndio najulikana kwamba mimi ni mtoto wa mkuu wa wilaya

Askari amechachawa,anasema sasa mbona hukusema kama wewe mtoto wa mkuu wa wilaya? Nikabaki natabasamu tu.

Pili siku moja nipo zangu shule ya tambaza wakati tunakaa upanga,nimeenda pele kujisomea mwenyewe,sasa nikakuta warembo wapo elimu ya sekondari kama sio A level basi ni O level

Nikaenda toilet,sasa nadhan baada ya kuondoka walikuja kukagua madesa yangu wakagundua kwamba nipo level za chuo kikuu,,nikawaona namna wanavyoniangalia ni kama wanataka kunipa maua yangu,nikapiga mikausho mikali nikaendelea kupiga kitabu
 
Wakuu, habari za jioni,

Katika maisha, mtu anaweza kuwa na kariba ya kawaida kabisa kiasi cha mtu mwingine kutojua au kutozoea tabia yake, hali inayoweza kusababisha kudharauliwa. Hata hivyo, baadaye watu hao huweza kugundua kwamba mtu waliyemdhani si wa kawaida kabisa na mawazo yao yanabadilika.

Iliwahi kunitokea siku moja nilipoenda ofisi fulani na kuwakuta wafanyakazi wote wakiwa wanawake. Nilipowasalimia, mmoja tu alijibu, tena kwa nyodo sana. Nilipowaambia kwamba nilihitaji bahasha zilizoachwa na bosi wao, waliniangalia kwa dharau. Wakati huo, nilikuwa nimevaa mavazi rahisi—pensi na sandle—na waliniuliza, "Wewe unazichukua kama nani?" Nikajibu kuwa nimeagizwa, lakini bado walinidharau na kuniambia, "Haya chukua, wahi daladala zimejaa sasa hivi."

Kumbe nilikuwa nimekuja na BMW nje ya ofisi. Walipokuwa wakijiandaa kuondoka, nikashuka ngazi na kwenda kwenye gari langu. Nilipofika kwenye eneo la kuegesha, walionekana kushangaa. Kwa heshima, nikawaambia, "Ingieni niwasogeze." Walikubali, lakini ndani ya gari walikuwa kimya kama wamemwagiwa maji. Walianza kucheka na kutabasamu huku wakifurahia upepo wa AC. Mmoja aliyekaa mbele aliniomba namba yangu ya simu, lakini sikufanya juhudi zozote za kuendelea mazungumzo naye, nikalipotezea tu.

Je, wewe umewahi kudharauliwa na watu, familia, au marafiki kutokana na mwonekano au hali fulani katika harakati za maisha?
We jamaa ni muongo, kwamba walikwambia uwahi daladala zimejaa
 
Mimi kazi yangu ina jina kubwa sanaa.Sasa watu wanafikiri nalipwa mamilioni masikini ya Mungu ,kumbe nakunja mia tisa na chenji kabla ya makato mpaka kurudi laki nne na kitu mfukoni.Basi watu mara waniombe niwaazime milioni kumi,mara niletewe prado linauzwa,mara mgeni rasmi wa kuongoza harambee.Kadi za harusi ndio hazina idadi.Kumbe ni masikini mwenye jina kubwaaaa.
Umenikumbusha niliwahi kuitwa mchongo wa uafisa masoko kampuni ya uturuki nikajua yess hapa ndio nimetoboa kumbe uafisa wenyewe unapewa vyombo vya plastiki ukauze halafu unapewa kamisheni🐼
 
Mimi bwana ni mtu ambaye sipendi kutumia cheo cha mtu au nafasi ya mtu kupata unafuu

Sasa kuna kipindi nilimuwekea dereva mmoja dhamana hlf akakimbia,dah ikabidi niwekwe mimi ndani,ilikuwa pale kituo cha msimbazi miaka ya nyuma,baba yangu alikuwa mkuu wa wilaya,basi bwana nikawekwa ndani kwa masaa kama matatu,baadae mshua anakuja ndio najulikana kwamba mimi ni mtoto wa mkuu wa wilaya

Askari amechachawa,anasema sasa mbona hukusema kama wewe mtoto wa mkuu wa wilaya? Nikabaki natabasamu tu.

Pili siku moja nipo zangu shule ya tambaza wakati tunakaa upanga,nimeenda pele kujisomea mwenyewe,sasa nikakuta warembo wapo elimu ya sekondari kama sio A level basi ni O level

Nikaenda toilet,sasa nadhan baada ya kuondoka walikuja kukagua madesa yangu wakagundua kwamba nipo level za chuo kikuu,,nikawaona namna wanavyoniangalia ni kama wanataka kunipa maua yangu,nikapiga mikausho mikali nikaendelea kupiga kitabu
Huyo polisi inaonekana alilaumu sana baada ya nyie kuondoka
 
Ila kwakweli first impression inamata sana ndio maana matapeli pale posta mpya wana suti kali unaingia mkenge mwenyewe,kwahiyo huyo mtoa mada sio kwamba muongo ni kweli kabisa,watu wanakuchukulia jinsi wanavyokuona

Nakumbuka wakati mzee amehamishiwa wilaya ya kinondoni tukaenda kuishi oysterbay,sasa pale hatupo mbali sana na coco beach,so unaweza tupia yebo yebo tu kisha unajisogeza tu beach

Nimekaa zangu beach,nikamuona mrembo anapita nikamuita,sasa wakati huo miguu yangu ilikuwa imezibwa na kigogo cha mnazi,demu kusogea si ndio akaniona nimevaa yebo yebo huwezi amini demu akasepa,,kimoyo moyo nacheka we hujui mimi ni mtoto wa kishua

Kwahiyo kwa kifupi jinsi gani unajiweka ndio watu wanakupa hadhi yako
 
Back
Top Bottom