Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Jamani gesi ni nishati inayorahisisha mapishi kwa haraka.

Ila ina kero yake jamani wakati ndio unapika inaweza isha ghafla na pengine kwa wakati huo huna hela ya kununua tena au unanunua mbali.

Unaanza hangaika na kuwasha mkaa nk.

Hebu tueleze ilikuwaje.

Ngoma ilizima ndo naanza kusonga ugali alafu mida mibaya saa tano usiku
 
Hapo umeweka unga wa ugali kwenye maji yanayochemka na mgeni anasubiri chakula
 
Kuna hiyo siku nilitamani kupika wali na nyama. Nimepika wali fresh huku nyama inachemka sijaunga bado. Baada ya nyama kuiva basi niunge kaanga vikorombwezo ile kuongeza maji mchuzi uchemke ngoma ikakata, ile siku tulikula wali na supu nilitaman hadi kulia hapo ni usiku mwingi na sina hata kipande cha mkaa nilikoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana mi nilinunua plate tatu gas moja umeme,gas ikikata nahamia jiko la umeme
 
Mimi hiyo siku nimepania wali nazi, samaki nazi...

Nimekuna nazi 3 nimechuja. Nimekatakata bamia na nyanya chungu...nimeloweka mchele...

Ile nimeweka sufuria tu ya mboga nianze kupika jiko likazima. Na nilikuwa na sh. 30,000 tu ya kunifikisha mwisho wa mwezi.

Nililiaaaaa........
Pole sana yaliyokukuta ni makubwa sana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tununue majiko ya umeme ya plate 1 huuzwa 50,000

Hayo yanaokoa
 
Pole sana yaliyokukuta ni makubwa sana[emoji23][emoji23][emoji23]
Asante. Nilishapoa. Siku hizi nina mitungi miwili hivyo nina mtungi uliojaa gesi pembeni kwa ajili ya emergencies kama hizi
 
Mwezi wa Ramadan niliamka usiku tupike ugali tulikua na msela wangu.. uji unatokota gas ikazima!!tukanywa maji tukalala tukaendelea na swaum

Gas huwa inaisha ghafla hasa kama hela hamna
 
W
Nilikua napika wali ika zima .nika fanya kuugeuza nikala wa chini wa juu ulkua auja ivaa nka uacha [emoji856][emoji28][emoji28] maisha yalikua yame nipiga.
Wangeboresha kwa kuweka gauge kama gari jamani.
 
Back
Top Bottom