Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Ninakuaga na heater Ile ya birika

Huwa sikosi mkate na peanut butter .

Gesi ikiisha tu wakati napika nachemsha zangu maji ya Moto namix na viungo nalalia chai

Simpo tu
 
Mimi hiyo siku nimepania wali nazi, samaki nazi...

Nimekuna nazi 3 nimechuja. Nimekatakata bamia na nyanya chungu...nimeloweka mchele...

Ile nimeweka sufuria tu ya mboga nianze kupika jiko likazima. Na nilikuwa na sh. 30,000 tu ya kunifikisha mwisho wa mwezi.

Nililiaaaaa........
 
Imeisha muda si mrefu hapa alafu nimetoka kuinjika maharage ya kukopa kwa Mangi. Akiba nina 1000 tu... hapa navizia watu walale nikaokote mbao nichemshe nje huko na moto wa kuni maana hali sio hali
 
Mimi hiyo siku nimepania wali nazi, samaki nazi...

Nimekuna nazi 3 nimechuja. Nimekatakata bamia na nyanya chungu...nimeloweka mchele...

Ile nimeweka sufuria tu ya mboga nianze kupika jiko likazima. Na nilikuwa na sh. 30,000 tu ya kunifikisha mwisho wa mwezi.

Nililiaaaaa........
Hahahaha,
Ulienda kujaza ili umalizie pishi lako.
 
Hakuna. Yaani niliweka tui na vikorombwezo kwenye friji nikaenda kununua chips nikala.

Nilikuja pika siku 2 baadae baada ya kutumiwa na ya kutolea
Gesi ikiisha huwa inakata stimu kweli.

Kwangu mimi huwa inapenda kuisha nikiwa sina hela au nina hela kiasi kidogo.
 
Acha tu mkuu,, hivi sijui huwa vinaambiana, unakuta mkaa umeisha,mafuta kula yameisha, sukari, mchele kagesi nako unapika mara kanaanza kusinzia daah!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Alafu mfukoni una buku tu
 
Jamani gesi ni nishati inayorahisisha mapishi kwa haraka.

Ila ina kero yake jamani wakati ndio unapika inaweza isha ghafla na pengine kwa wakati huo huna hela ya kununua tena au unanunua mbali.

Unaanza hangaika na kuwasha mkaa nk.

Hebu tueleze ilikuwaje.

Si bora hata uwe na huo mkaa,mimi mara mbili nimeishia kula mboga kabla hata sija kamilisha mapishi...
 
Back
Top Bottom