Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Chakushangaza zaidi mtungi wangu una Gage ya kuonyesha kama Gas ipo kiasi gani ila sikuwahi hata kuangalia sababu mtungi upo chini ya Meza, Kila nikitaka kuuvuta niangalie ipo kiasi gani basi najipa moyo mbona mzito bado ipo, nikijisahau tu ndio yanatokea yakutokea [emoji3]
Hcho kifaa (regulator) ulinunua sh ngapi
 
kinapatikana wapi??
Kwa aina hii ya regulator nenda kariakoo pale shimoni. Na kwenye maduka ya wahindi wanapouza hizi jiko za plate mbili na kadhalika wanakuwa nazo kuna fake lakini so kuwa makini sana.
 
Unasema hupiki mara nyingi, huwa unakula nini?
Ishawahi kunitokea hii, usiku napika zangu chips ndiyo nimeweka hata hazijaiva jiko si likazima, aargh ni usiku na sikua na pesa nilichofanya nikatoa viazi kwenye mafuta nikalala na njaa tu😬🙌

Na nahisi hata sahivi inakaribia kuisha gas gani tangu November 2020 hadi leo ipo tu mmh , japo huwa sipiki mara nyingi ila...
 
Mie mara nyingi tu.

Ila mara nyingi nakuwa nishajipanga maana huwa naihesabia tarehe. Na ikiwa mambo hayako vizuri kununua mtungi mwengine naponea kwenye electricity cooker. Ila siku hio mapishi huwa mwepesi......like chips na mayai tu baas
 
Dawa uwe na mitungi miwili kulingana na mahitaji yao. Kwa mfano, me huwa natumia miwili ile ya kilo kumi na tano.

Ukiisha mmoja sikai kusubiria sanaaa nitakaa kama wiki mbili au tatu nitakwenda kujaza ili iwe standby. Ila kwa sasa nataka kwenda chukua ule mkubwa kabisa.

Nina Mkubwa na mdogo
Ila yote ikiwa na gas natumia yote
Huku mboga kule chai [emoji23][emoji23]

Nimeona nisijaze tu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom