Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

Unatia sukari.. Unapiga, unakomba na mboga siku imeisha..

Ni vizuri kiwa na jiko la gesi lenye option ya kutumia na umeme.. Mipango ikiisha huku unahamishia huku.
 
Ishawahi kunitokea hii, usiku napika zangu chips ndiyo nimeweka hata hazijaiva jiko si likazima, aargh ni usiku na sikua na pesa nilichofanya nikatoa viazi kwenye mafuta nikalala na njaa tu😬🙌

Na nahisi hata sahivi inakaribia kuisha gas gani tangu November 2020 hadi leo ipo tu mmh , japo huwa sipiki mara nyingi ila...
🤣🤣🤪
 
Kuwe na mitungi inayoonyesha kiasi cha gesi kilichobakia kama Luku
 
Dawa uwe na mitungi miwili kulingana na mahitaji yao. Kwa mfano, me huwa natumia miwili ile ya kilo kumi na tano.

Ukiisha mmoja sikai kusubiria sanaaa nitakaa kama wiki mbili au tatu nitakwenda kujaza ili iwe standby. Ila kwa sasa nataka kwenda chukua ule mkubwa kabisa.
 
Hivi hakuna kifaa kitakachowekwa kwenye mtungi kuonyesha gas inavyopungua?
Kipo. Ni regulator zenye gauge......
images%20(9).jpg
 
Kabisa mkuu wahenga waliotoa huo msemo hawakukosea aisee

Chakushangaza zaidi mtungi wangu una Gage ya kuonyesha kama Gas ipo kiasi gani ila sikuwahi hata kuangalia sababu mtungi upo chini ya Meza, Kila nikitaka kuuvuta niangalie ipo kiasi gani basi najipa moyo mbona mzito bado ipo, nikijisahau tu ndio yanatokea yakutokea [emoji3]
 
Hahaha acha tu yani sasa ukute upo choka mbaya sasa!
 
Back
Top Bottom