Mkuu, hii nime mention kabisa tayari sehemu na maeneo kadhaa kwenye comments zilizo tangulia.#3, hiyo inaweza zidi zaidi ya hapo,,
Hapa mwanza kuna sehem huwa naenda mida ya jion kupata sahan moja ya matunda mix,, ni buku tu sahan moja,,
Aiseh anapiga pesa yule,,
[emoji19]
AiseeUjuwe sijawahi kuona sehemu ya kuuzia Tai. Hapa Dodoma mjini ikitokea kijana akaitazama hii fursa kwa jicho kama langu hakika ninaamini ataweza kuingiza faida isio pungufu ya 10 elfu per day.
Kwanza nisema kwamba sisi wanaume ni wavivu sana (sio wote) wa kubadilisha Tai, lakini wanaume wengi in town kazi zao zinawalazimisha kuvaa Tai. Lakini wanaume haohao ukiwasogezea Tai tena ambazo tayari zimefungwa, ni wepesi sana wa kuzinunua.
Kwamfano, kijana akiamua kunua Tai za mtumba tena za grade 1, nina hakika haziwezi zika zidi shilingi 1 elfu kwa kila kipande.
Kisha ukizifua Tai hizo vyema na ukazinyoosha kwa pasi vizuri na kisha ukazifunga vyema kila moja ikavutia, nina hakika kila kipande cha Tai utauza kwa shilingi isiyo pungua 5 elfu.
Na ili kijana afanye biashara yake vizuri, basi hapa nina shauri kijana atengeneze metal skeleton iliyo nadhifu na kisha zipange pale bidhaa zako.
Hii biashara inahitaji mtaji mdogo sana usio zidi 300 elfu.
[emoji120][emoji120]Mkuu, niliulizwa swali kama hili, ingawa halifanani na hili kwa eneo kubwa.
Ebu pata nafasi upitie post namba 57/58
Mkuu, kijiografia Dodoma imegawanyika kwa makundi kadhaa.[emoji120][emoji120]
Mkuu, ebu kwanza fanya zowezi moja ambalo pengine linaweza likakufaa kwa siku ya ijumaa.Bro inabidi nikufind
Katika pitapita, pamoja na kuhangaika kwangu hasa kwenye kipindi tatanishi cha awamu hii ni:-
1. Sitaki kuwaza kufanya biashara kubwa inayo zidi 1M kwasababu mimi bado ninamaisha ya kawaida.
2. Sitaki kuwaza biashara kubwa kwasababu ninahisi huu sio wakati muafaka kwa kuwekeza fedha nyingi.
3. Nimeamua kufanya kitu ambacho kwanza kitanifanya nimlipe 20 elfu ili nipate kitambulisho chake na nisibughudhiwe nao.
4. Sitaki kuruhusu masikio yangu yakubaliane na mitazamo ya watu ambao watanivunja moyo ama hata kumicheka.
5. Nikifanya utafiti wowote na nikajiridhisha kufanya ujasiriamali, sinto ruhusu kusikiliza ushauri wa walio shindwa.
............. Nitaendelea badae, maana naona saizi whatever-vant imeanza kukamata hatamu....[emoji28][emoji28]
Watu wengi sana tumekuwa tukijikuta tunashindwa kufanya maaamuzi muhimu Katika Maisha tu Kwa kuogopa "WATU WATANIONAJE "No 4&5 huyo ni mimi kabisa
Shukrani Sana kiongozi.. Wala hujachelewa kabisa. Hahaaaaa hiyo whatever K-vant hiyooo ooogh...Mkuu, kwanza nikuombe radhi kwa kuchelwa kujibu hoja yako na kama ujuavyo jana ilikuwa oyaoya pale Pestana, hivyo kidogo nilichelewa kulala sababu ya whatever-Vant...[emoji28]
Nikirudi kwenye hoja ya msingi ni kwamba, Dodoma unaweza fungua Mini Supermarket kwenye maeneo yafuatayo.
Kama utapata eneo pale Wajenzi, njiapanda ya kwenda kwa Kasim Majaliwa panapo gawanyika na njia ye kuelekea Chang'ombe, kama unaelekea Mipango ukitokea mjini.
Pia ukiweza kupata eneo la biashara yako kule mitaa ya St.John itafaa zaidi.
Na ukipata jengo maeneo ya Kito Bar, kama unatokea Police Central, kuelekea Mlezi.
Na ukipata eneo pale mitaa ya Stella, Nkuhungu mkabala na kanisa LA Roman itakuwa shangwe tupu.
Kwa kifupi maeneo ni mengi, na ikiwa kweli unania ya kufanya biashara, basi nakushauri utembelee mitaa hiyo na ufanye utafiti.
Karibu sana Dodoma...
Hahaaha...
! Malinyi
Aisee!!Malinyi wanalima sana mpunga ila jiandae kupambana na wasukuma wenye ng'ombe maeneo ya Iragua, Itete na Mtimbira wanaopenda kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya watu.
Asantee Sana.. Nitakutafuta pia unipe kiwanja sehemu rafiki kwa ajili ya makazi.. Najua wewe ni jungu kuu................[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Mkuu, karibu sana Dodoma
Wale wafugaji wanakata sana miti na kuharibu misitu hasa maeneo ya Sofi Mission ukiwa unaelekea Malinyi hadi kando kando ya mto Fulua. Mamlaka husika inabidi ziwachukulie hatua wale jamaa.Aisee!!
Mwezi uliopita nilikuwa pale Iragua nikakutana na hiyo stori ya Wasukuma nilichoka.
Ila kuna sehemu niliwakuta Warundi wanalima sana nyanya. Mkuu manengelo nadhani utafanikiwa maana wale wafugaji wanapenda waisikie lugha ya kwao tu
Ni kweli mkuu, niliambiwa wenyewe wanavamia eneo na kuanza kulifyeka bila kujulisha mamlaka. Kuna uoto wa asili wameuharibu sana. Kuna miti imeadimika sana kama vile mipingo, mivule, n.k. sehemu nyingi za nchi yetu lakini kule nimeikuta imejiotea hovyo hovyo tu...Wale wafugaji wanakata sana miti na kuharibu misitu hasa maeneo ya Sofi Mission ukiwa unaelekea Malinyi hadi kando kando ya mto Fulua. Mamlaka husika inabidi ziwachukulie hatua wale jamaa.
Viwanja vipo kwa wingi mkuu, karibu sana