Mkuu, kwanza nikuombe radhi kwa kuchelwa kujibu hoja yako na kama ujuavyo jana ilikuwa oyaoya pale Pestana, hivyo kidogo nilichelewa kulala sababu ya whatever-Vant...[emoji28]
Nikirudi kwenye hoja ya msingi ni kwamba, Dodoma unaweza fungua Mini Supermarket kwenye maeneo yafuatayo.
Kama utapata eneo pale Wajenzi, njiapanda ya kwenda kwa Kasim Majaliwa panapo gawanyika na njia ye kuelekea Chang'ombe, kama unaelekea Mipango ukitokea mjini.
Pia ukiweza kupata eneo la biashara yako kule mitaa ya St.John itafaa zaidi.
Na ukipata jengo maeneo ya Kito Bar, kama unatokea Police Central, kuelekea Mlezi.
Na ukipata eneo pale mitaa ya Stella, Nkuhungu mkabala na kanisa LA Roman itakuwa shangwe tupu.
Kwa kifupi maeneo ni mengi, na ikiwa kweli unania ya kufanya biashara, basi nakushauri utembelee mitaa hiyo na ufanye utafiti.
Karibu sana Dodoma...