"Ushimen" hivi ndivyo nimeamua kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa

"Ushimen" hivi ndivyo nimeamua kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa

Asante sana mkuu...
Nilizaliwa tarehe 21 March 1981.
Bilashaka nimekujibu vyema
Dah..kumbe hata kuishi bado hujaanza?..Safi sana mkuu...hata hivyo umekwepa mishale ya kutosha....Wewe komaa huko wakati huku Mimi nakuombea ndani ya siku 365 zijazo uunde robot lako mwenyewe hapo workshop ....libebe keki yako ya kuanzia maisha at 40 [emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Happy birthday brother.... kila siku huwa unanivunja mbavu zangu..uishi miaka mingimingi,,,naomba nikuone bday man tupia kapicha brother [emoji28]


Kwanini unapenda masikhara?
Kwa jiji la dodoma unadhani fursa gani zipo nzuri kuzifanya???

Unadhani Nini kifanyike kupunguza Hali ngumu ya maisha ya vijana wengi hususan wahitimu wa vyuo vikuu??

Ungepewa nafasi ya kuwa rais Sera yako ingekuwa ipi???




Sent using Jamii Forums mobile app
1. Nitaweka picha badae kidogo
2. Sijui kwanini napenda sana maskhara, nadhani hivyo ndivyo Mungu aliniumba.
3. Dodoma fursa naziona nyingi sana za ujasiriamali. Na nikimuona ama kusikia kijana amekosa kitu cha kumuingizia walau 20 elfu wakati ana mtaji wa 500 elfu.... hakika ninamshangaa sana.
4. Mimi ni muumini wa kufanya kazi kwa bidii, na ninaamini yeyote anae fanya kazi kwa bidii lazima atapata faida.
Kwa vijana wanao maliza university na kukosa ajira, hao naweza nikasema kwamba wamekua na mawazo ya kuajiriwa kuliko kujiajiri. Na mwisho wa siku wanaogopa kukaanga mihogo kwasababu tu wanaona aibu kwamba ana degree.
5. Ningepewa nafasi ya kuwa Rais, hakika nisinge kubali kwasababu mimi sio mpenda siasa, sipendi uongo na nipo straight forward.
 
Back
Top Bottom