Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

!
!
Watu Hawachagui Raisi Kwenye Uchaguzi Huu. Unapotaja Reli Sijui Ndege Elimu Bure Na Ushuzi Mwingine Kama Huo Ni Mwenyekiti Gani Wa Mtaa Ataweza Kununua Kwa Ajili Ya Mtaa Wake?
Kuna Wasomi Wengine Hovyo Sana Aisee
YAAANI KWA AKILI HZI BORA MZEEE WAKO ANGEPIGA MASTERBUTION TUUUU.SHULENI ULISOME UJINGA CC FAIZA FOX
 
Pascal Mayalla siamini katika hoja yako. JPM hawezi kuzuia upinzani kushiriki siasa kwani atakua kinyume na sheria ya vyama vingi.

Anachotakiwa kufanya ni kutoa kauli kwa watendaji wake wanaominya demokrasia.

By the way, upinzani ni imara kiasi gani?
Mkuu Freema Agyeman, hii hoja yangu sio hoja ya kiimani kuhitaji kuamini au kutoamini, as if hili ni jambo la kiimani, la kufikirika tuu, kusema JPM hawezi kuzuia upinzani kushiriki siasa kwa sababu ni kinyume cha sheria ya vyama vingi, hivyo unakiri ni watendaji wake ndio wanaominya demokrasia hivyo yeye ndie awakemee?!. Please usitake tufungue the pandora box la demokrasia yetu, its a like a can of worms, ukiisha open, you can control, kwa kuanzia tuu katiba ndio iliyoruhusu mikutano ya kisiasa, unamjua aliyezuia ni nani?, kwa sheria ipi?, kwa mamlaka gani?. Kwa taarifa tuu, JPM anaweza kufanya kila kitu!, akiamua kuruhusu huu nchezo wa siasa uchezwe fair, anaweza. Sisi sio mafarisayo tunganganie taratibu, sheria na kanuni.

P.
 
Hapa ndiposa mnishangazapo baadhi watanzania. Mwasema tufuate katiba na taratibu tulizojiwekea ili kujenga mfumo imara wa kuheshimu katiba na sheria, wakati huo huo mnashauri Rais avuruge ufuataji wa sheria na katiba katika suala ambalo linatoa nafasi kubwa kwa watanzania kujua umuhimu kufuata katiba, sheria na taratibu nyingine tulizojiwekea. Mna malengo gani enyi baadhi ya watanzania!?
Mkuu, Paskali, ni lini hasa unataka uione Tanzania inaanza kufuata taratibu, sheria na katiba kwa kumaanisha hasa kama siyo wakati wa awamu hii ya tano!?🙂🙂🙂
Mkuu TUJITEGEMEE, kwanza naomba kukiri, hoja yako ni very valid, mimi nikiwa miongoni mwa washabiki wa kufuatwa kwa katiba, sheria, taratibu na kanuni, lakini kwa vile kuna mambo makubwa katiba imekiukwa na tumeyakubali, then kukiuka sheria, taratibu na kanuni katika kutoa haki ni jambo jema.
Nimetolea mfano baba kucheza na watoto na kuwaacha watoto wamshinde.
Tufuate katiba, sheria, taratibu na kanuni, katika makubwa, lakini pia tumuunge mkono rais wetu Magufuli pale anapokiuka katiba, sheria, taratibu na kanuni kwa nia njema ya kulisaidia taifa, hili la uchaguzi ni miongoni mwake.
Rais Magufuli ni Mkweli Daima!. Jee Tumuunge Mkono Rais Wetu ...

P.
 
Mkuu Freema Agyeman, hii hoja yangu sio hoja ya kiimani kuhitaji kuamini au kutoamini, as if hili ni jambo la kiimani, la kufikirika tuu, kusema JPM hawezi kuzuia upinzani kushiriki siasa kwa sababu ni kinyume cha sheria ya vyama vingi, hivyo unakiri ni watendaji wake ndio wanaominya demokrasia hivyo yeye ndie awakemee?!. Please usitake tufungue the pandora box la demokrasia yetu, its a like a can of worms, ukiisha open, you can control, kwa kuanzia tuu katiba ndio iliyoruhusu mikutano ya kisiasa, unamjua aliyezuia ni nani?, kwa sheria ipi?, kwa mamlaka gani?. Kwa taarifa tuu, JPM anaweza kufanya kila kitu!, akiamua kuruhusu huu nchezo wa siasa uchezwe fair, anaweza. Sisi sio mafarisayo tunganganie taratibu, sheria na kanuni.

P.
Nakubaliana nawewe 1000%, Nashangaa kumsikia Lipumba akisema Rais Magufuli aingilie uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aingilie wakati yeye ndiye anacheza hizo rafu? Jiulize Referee anapomkwatua mtu uwanjani, aliyekwatuliwa akamuomba huyo referee ajipe adhabu au ajitoe uwanjani. Inawezekanaje, Zaidi anaweza kukuchekea tu na kujidai ni bahati mbaya lalini lengo lake limetimia.
 
Mambo mengi ya Nchi kwa sasa yame kuwa yakiendeshwa kwa Hisani ya Mtu mmoja ,Katiba tuliyo Apa kuilinda ipo likizo hasa kwa Dhana uliyo igusia ktk bandiko lako kwa namna ulivyo muomba Mh Mtukufu sana wa Nchi.

Na hizi ndio fikra za Watawala walio Madarakani ,ktk kuwaletea Wananchi wao Maendeleo。
View attachment 1259103
Hivi sura ya mtu ina uhusiano na akili zake?
 
kwahivyo aliwatuma wakosee ili a stage tukio.
Bravo...
Huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza tatizo na kulitatua ili apate umaarufu zaidi. Sitashangaa nikisika Dr Abasi akisema “Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli amewasamehe wote waliojaza fomu kimakosa”.
 
Mkuu, yaani MKAPA na KIKWETE hakuna walichofanya eti? Punguza mahaba yako dhidi ya huu utawala wa KI IMLA unatuchosha sasa.
 
baada ya Gaddafi kufa uhuru ukapatikana qa kutosha....[emoji3][emoji3][emoji3]

Jf is full of comedianz
Yani ccm wangesoma case study ya Gsddafi،aliwafanyia Kila kitu ila aliwaminya katika Uhuru wao. Kwaio yote mazuri hayakuonekana na wakamuua.

Sasa reli, madaraja, mabarabara hayataonekana ktk hizi figisu.

Kuna tetesi za ugonjwa badala ya kusikitika watu walifurahi hio ilokua indicator mbaya. Hatujifunzi. Owky hakuna marefu yasio na mwisho
 
Nilisema "too late" CHADEMA walipojitoa na nasema leo "too late" kumshauri Rais aruhusu wagombea waloenguliwa. Kwa CHADEMA ilikuwa too late kwa sababu baadhi ya wagombea walishapitishwa na hivyo kwenye karatasi ya kupigia kura watakuwemo na hii ndo mbinu ya chama tawala. Ni too late kwa Rais kwa sababu vyama vimeshatangaza kususia uchaguzi. Maji yakishamwagika hayazoleki. Kwa haya mengine naunga mkono hoja.
Mkuu Zawadin, kama sababu za kujitoa ni kitendo cha wagombea wao kukatwa, sasa wagombea wote wamerudishwa, kwanini waendelee kujitoa?.
P
 
Ni Kweli Sheria Zimewekwa Ili Zifuatwe Ila Ajabu Ni Kwamba Vyama vya Chadema na A.c.t Wametangaza Kujitoa Kwenye Huo Uchaguzi, Ila Bado Waziri Wa Tamisemi Analazimisha kubandika Majina Ya Wagombea Ambao Vyama Vyo Vimejitoa Kwenye Huo Uchaguzi.

Swali:
Ikiwa Chama Kimejitoa kwenye Uchaguzi, Hao Wagombea Ambao Bwana Jaffo Anadai Bado Majina Yao Yatakuwepo Kwenye Karatasi Ya Kupigia Kura Bila Kujari Kama Vyama Vyao Vimejitoa Watasimama Kama Wagombea Wa Chama Gani?.

Au Siku Hizi Tanzania Tuna Wagombea Binafsi?.
Mkuu Mkwaha, kugombea ni kwa hiyari mbili,
1.Hiyari ya mgombea na kuomba udhamini wa chama
2. Hiyari ya chama kushiriki na kutoa udhamini kwa wanachama wake.

Ukiisha jaza fomu na kuiwasilisha kwa msimamizi
wa uchaguzi, hizo hiyari mbili za kujitoa zitakuwa bado zipo ila kuna utaratibu wa kuandika barua
1. Kama ni mgombea anajitoa anaandika barua kwa msimamizi na kutoa taarifa jina lake linaondolewa.
2.Kama ni chama kinajitoa, kinaandika barua kwa msimamizi kuondoa udhamini wake kwa wagombea wao wanaondolewa.

Baada ya kuwasilisha fomu, kujitoa hufanywa kwa utaratibu huo na sio kujitoa kwa kuitisha press conference kutangaza kujitoa. Jee Chadema na ACT wamefuata taratibu za kujitoa?.

Kama Chadema na ACT hawajaandika barua individual kwa kila msimamizi kuondoa udhamini wa wagombea wao na serikali jana imesema inawapitisha wote. Wakiisha pitishwa na kujitoa bila kufuatwa taratibu, bado wanakuwa ni wagombea halali.

Kuanzia kesho majina yanapelekwa kwenye print out ya ballot papers Ballot papers zikitoka na majina, hakuna tena kujitoa. Hivyo Chadema na ACT zitakuwa zimejitoa kwa press conference lakini zitashiriki uchaguzi kwa lazima. At this stage hakuna tena kuweka mpira kwapani.

P
 
'Kutokana na kasi ya rais Magufuli kutuletea maendeleo ya vitu vya kuonekanika, Midege, Reli ya SGR, Mabarabara nchi nzima, madaraja ya Juu kwa Juu, Mradi wa umeme wa Stigler , Tanzania ya Viwanda, Elimu Bure, Vituo vya Afya kila kuna, etc, etc, just to mention but few, vinaipa CCM fursa ya ushindi wa kishindo cha wazi kabisa katika uchaguzi wowote nchini Tanzania kati ya sasa hadi 2025, hivyo mamlaka zinazosimamia uchaguzi huu, waruhusuni wagombea wote waliopitishwa na vyama vyao wapite tuu bila kujalisha kama wanekidhi sifa na vigezo, ili tuu kuruhusu ushindani wa haki, ushindani wa uwazi na mshindi apatikane kihalali katika uchaguzi huru na wa haki'.

Nimekuelewa vizuri mkuu Pascal Mayalla
Mkuu Upendo daima, asante kwa kunielewa kwa sababu kiukweli kabisa wanaonielewaga humu jf ni wachache, only those wenye uwezo to read in between the lines.
Thanks.
P
 
Uzalendo halisi na wa ni kuzungumza kwa kutumia lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
Sababu za kutosafiri nje ni uzalendo uliotukuka wa kubana matumizi, na sio issue za lugha, kama ni lugha ya Malikia, inapanda sana, ameitumia hadi kwenye Ph.D thesis yake.
P
Thesis yake iko kwenye maktaba gani? Pale UDSM haipo
 
Paskali wewe kama mwandishi mwandamizi nlidhani unafahamu kuwa mkuu hapendi ushindani na hawezi kuruhusu hilo jambo litokee hata kidogo
Mkuu Kimeloki, mimi kama mwandishi mwandamizi, nafahamu jinsi Mkuu alivyo msikivu na anavyo change for the better




P
 
Habari njema zimeanza, Waziri katangaza wagombea wote walioenguliwa kwa kujaza fomu vibaya warudishwe.
Huu sio mwanzo mbaya, sasa tunawasubiri Mbowe na Zitto kutangaza kuruhusu timu zao kuingia dimbani.
P
Mkuu Pascal , nitawashangaa sana Wapinzani wakikubali kurudi kwenye uchaguzi.

Waziri Jaffo hakueleza kama ilikuwa ni halali au makosa kuwarudisha walioenguliwa

Bila kujua kwanini walienguliwa na sheria ilitimizwa au kukiukwa vipi tangazo lake ni ''premende'' ili Wapinzani warudi kwa lengo la kutimiza taswira ya uchaguzi na kuhalalisha matokeo waliyonayo.

Tayari CCM imeshinda kwa asilimia 58 kwa wagombea wake kupita bila kupingwa.
Hapa unaweza kuona udanganyifu. Wapinzani walinyimwa fomu na kwingine kukatwa mapanga.
Halafu wasimamizi wakakimbia vituo kupokea fomu. Hilo tu limetoa 58%

Katika hizo 42% zilizobaki wapinzani wakishinda sana kwa uchaguzi huru ni asilimia 50% ambayo itawapa CCM 50 nyingine za 42%. Kwa maana 21%

Ukichukua 21 ukajumlisha na 58 unapata 79 ambayo bila shaka ni ushindi wa kishindo.

Lakini pia CCM na Jaffo wanaweza kushinda hiyo 42% kwa 90% ambayo takribani 36%
36 % +58 %= 94 % Ushindi wa kishindo.

Ikiwa haijulikani sababu za kuenguliwa, hakuna maana ya kuendelea na uchaguzi kwa hisani ya Waziri Jaffo. Uchaguzi ni tukio la kisheria siyo matakwa ya Jaffo au huruma.

Waziri anawafanya Watanzania majuha sana!
 
Hatua muhimu kuliko zote

1. Tume huru ya uchaguzi
2. Siasa ziruhusiwe majukwaani kwa mujibu wa katiba
3. Katiba ya Jaji Warioba

Wasikubali kushiriki uchaguzi wowote bila hayo mambo matatu.
 
Una 'Sarcasm' ya hali ya juu sana . Hapo uliposema 'midege' umenifurahisha Mkuu. Midege si inaonekana wanaogopa nini
 
Mkuu kuna mambo mawili. Mosi, muda wa kujitoa. Je, walijitoa kwa wakati? Pili, mgombea kama mgombea amewasilisha barua ya kujitoa? Kama hajawasilisha barua hiyo, unamuondoaje? Kumbuka kuna kanuni na taratibu za kufuata kuhusu hili. Na hili mkuu ndilo wanalokosea Chadema. Wanafikiri kila kinafanyika tu (atavism).
Mkuu Sweet Tablet, asante sana kwa objectivity yako kwenye hili. Issue ya kufuatwa kwa sheria, taratibu na kanuni katika ujazwaji fomu ni jambo la muhimu sana, Tanzania sasa tuna e-government more than 10 years now, fomu zote ziwe zinajazwa online, kama kuna kosa lolote linakuwa detected na submission haiwezi ku go through hadi kila kitu kikamilike kama online applications.

Chama pekee chenye ofisi kila mtaa ni CCM only hivyo kimewajazia fomu wagombea wake na kuzihakiki. Kwa chama kisicho na ofisi hata ya wilaya, unategemea nini, ndio maana tumewaombea wote waruhusiwe.
P
 
Back
Top Bottom