Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Pascal tatizo LA CCM hawakuicheza vizuri, kila MTU anajua kuwa huwa wanaiba kura na Jafo amekiri kwa kuziita"figisu". Bahati mbaya sana wamepitiliza, yaani walitakiwa wabakishe wachache wa kuzugia! Hapa ndio walichemka.

Huu sio wizi ni upumbavu na ukichaa wa kisiasa! Tafiti zote zinaonyesha CCM ndio wana wafuasi empty headed kuliko hata vile vyama 11 visivyo na uwakilishi Bungeni! Kwahio hawakutakiwa ku-deviate saaana kutoka kwenye ukweli huu maana hata Leo hii tukisema tuitishe CV za Wagombea wote na tukafanya analysis lazima Wapinzani wataibuka na Wasomi wengi zaidi
 
Tushakujua kuwa wewe ni ccm maana kipindi majina yamekatwa hukuongea chochote sasa umesikia tamko la jafo unajifanya kushauri
Bora umemwambia wazi. Pascal ni mhuni wa kisiasa, ni mwandishi mtafuta fursa wa kiwango cha juu. Anaandika kwa kulembalemba ili aonekane mwema kwa kaka yake. Ni eneo gani nchini ambako CCM yake haijatoa maelekezo kwa watendaji kukata majina ya Wapinzani? Leo anajifanya mwema anauma na kupuliza? Aache unafiki, kama ni mkweli auseme ukweli wote na siyo mafumbo na kujitafutia sifa binafsi.
 
Nguruvi3,
Kwa sababu Watawala wanaamini Waongozwa ni kama Kuku, wanahitaji kulazimishiwa dawa kwa manufaa yao wenyewe, ukiwaacha waamue wanavyotaka watakufa kwa kideri.
 
Namshangaa Magufuli kwa kuua Demokrasia. Ila Magufuli si anachapa kazi? Sasa kwa nini anaogopa wapinzani? Jamani wao pia ni Watanzania. Hebu ajiweke kwenye viatu vya ATC,CHADEMA n.k.Halafu CCM ifanyiwe kama anavyowafanyia.
Kwa kweli simuelewi anachokiogopa ilhali anachapa kazi.
 
Nimekumbuka jinsi Serikali ya awamu ya tano ilivyoanza vizuri hadi wapinzani wakakosa jambo la kukosoa nao wakaunga mkono hata kusahau figisu za uchaguzi mkuu 2015. Ndipo sasa najiuliza maswali yasiyoisha.

Kulikuwa na haja gani ya kuzuia shughuli za kisiasa.

Kulikuwa na haja gani ya kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

Kulikuwa na haja gani ya kuingiza utamaduni mpya wa kutekana, kuuana.

Kulikuwa na haja gani ya kufunguliana kesi za kubambikizana za kisiasa.

Kulikuwa na haja gani ya kufanya biashara ya kununua wabunge, madiwani, Wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa upinzani.

Kulikuwa na haja gani ya kupitishana bila kupingwa kwenye chaguzi ndogo na kuiba kura

Kulikuwa na haja gani ya kuzima bungelive.

Kulikuwa na haja gani ya kufunga midomo ya viongozi wa kiroho na kuwaingiza kwenye dhambi ya kuacha wito walioitiwa wa kuonya, kuasa na kutoa kwenye jamii na viongozi maono wanayopewa na Mungu juu ya mustakabali wa nchi yao.

Na maswali mengi mengi mengi yasiyo na majibu. Hata hivyo naamini kama kuna utashi wa kisiasa, kiroho na ubinadamu bado Tanzania inaweza kurudi kwenye misingi ya kuasisiwa kwake kama Taifa.
 
Ziliwekwa taratibu ili zifuatwe. Ukishindwa kiziguata, unaondolewa tu. Hata Bunge la Congress la Marekani sasa liko kwenye mchakato wa kutaka kimuondoa Rais Trump madarakani kwasababu amekiuka utaratibu. Simple!
Bunge letu pia lingekuwa na watu wenye akili na waledi na wanaojari maslahi ya nchi yetu hiki kitu kilitakiwa kiwe kimefanywa hapa Tanzania maana mbele ya katiba yetu magufuli ameshapoteza uhalali wa yeye kuendelea kuwa rais
 
Namshangaa Magufuli kwa kuua Demokrasia. Ila Magufuli si anachapa kazi ? Sasa kwa nini anaogopa wapinzani ? Jamani wao pia ni watanzania. Hebu ajiweke kwenye viatu vya ATC,CHADEMA n.k.Halafu CCM ifanyiwe kama anavyowafanyia.
Kwa kweli simuelewi anachokiogopa ilhali anachapa kazi.
Magufuli is incompetent individual, He is PhD holder still hawezi kuelewa anaitwa rais kwa sababu wananchi wa Tanzania wametoa cheo hicho kupitia katiba ya JMT na wananchi hao hao na kupitia katiba hiyo hiyo wameruhusu mawazo shindani ili kuchochea maendeleo yao.kwa lugha nyingine rais na wapinzani wote ni watoto wa baba na mama mmoja yaani Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ila mtu anayejiita PhD ameshindwa kuelewa jambo dogo kiasi hiki.
 
Unajua Maana Ya Udhamini?.
Kwanini (Mfano) Mbunge au Diwani Akifutiwa Uwanachama Na Chama Chake Ana Kosa Sifa Ya Kuwa Na Hicho Cheo?.
Mkuu Mkwaha kama wewe ni mgumu wa kuelewa sio kosa langu. Nimejieleza vizuri. Lakini utofauti wa mawazo unakubalika hasa katika nchi yetu ya kidemokrasia Mama Tanzania.
 
Hawana vigezo, ndio maana hawakupitishwa mwanzo kabisa.
Kweli. Ila hao wachache wachache waliobaki na wamekidhi watapitishwa. Ila nawashauri wasijihusishe na michakato yote ya kampeni ili kuheshimu maamuzi ya vyama vyao ya kujitoa. So unakumbuka hata CUF enzi za Maalim ilikuwa hivyo na zikapigwa KURA ZA MARUHANI?
 
Nchi inahitaji maendeleo ya watu ...tumejichelewesha sana kusaka kiki za demokrasia kwani ndio upuuz waliotaka tuufikirie.
Hata sasa hakuna maendeleo ya watu yanayofanywa. Tumeshindwa kuboresha elimu; Maabara za vyuo vikuu zimebaki magofu; Vyuo vikuu bado wanafundisha titration ya acid na base, sakiti sambamba na mfuatano; halafu tunasema Kuna maendeleo ya watu? Tunajengewa reli na waturuki halafu tunataka maendeleo ya watu? Ni aailimia ngapi ya bajeti huenda kwenye utafiti nchi hii?
 
Swali moja la muhimu la kujiuliza

walioenguliwa/waliokatwa Je wameonewa au ilikua haki yao kukatwa??

tusilete mifano ya zamani ya baba na mtoto hapa twende kwenye reality..

Kama wameonewa lazima wana sababu (zisikilizwe) ila kama hawajaonewa

sioni sababu ya wao kusamehewa eti hata kama wanamakosa warudi tuuu (ujinga huuu haupo)

kama haki imetendeka wakae wajipange kususa/kuzira hakufanyi wengine wasipate haki yao kisa wewe tu umesusa/umezira

wafikirieni na ambao wamepita kwa vigezo vyote then uje umpambanishe na mtu kisa tu kapewa upendeleo..

Kama mnataka washinde kama mfano wako paskali,UCHAGUZI usiwepo na mseme Mtaa flani aongoze flani

Mtaa flani aongoze flani pangeni kabisa viongozi FUTENI uchaguzi ila sio kuleta upendeleo sehemu zisizo hitaji upendeleo

Hata mashuleni tumesoma na vilema,viwete ila linapokuja swala la mtihani hatuangaliii wewe kilema,wewe kiwete

tunaangalia utajaza nini kwenye mtihani wako as long as wote tuna mikono na tuna akili sawa (upungufu wa viungo hauwezi kukufanya wewe ukapewa upendeleo.

Point yako Pascal Mayalla sikubaliani nayo na kama RAIS ni GREAT THINKER hawezi iruhusu wala ikubali.
 
Bunge letu pia lingekuwa na watu wenye akili na waledi na wanaojari maslahi ya nchi yetu hiki kitu kilitakiwa kiwe kimefanywa hapa Tanzania maana mbele ya katiba yetu magufuli ameshapoteza uhalali wa yeye kuendelea kuwa rais
Tatizo ni nani wa kulianzisha na kwa kipengele gani. Marekani wamelianzisha wapinzani wa Democrat.
 
Huwezi kuendesha nchi wala kuhudumia taifa lako kwa kutegemea hela ya kubana matumizi ya mafuta, hizo ni fikra za kifukara kabisa na za kibwege.
Sina hakika kama unafikiria vizuri mpagilio wa hoja zako hata kama una mapungufu ya kukosa staha katika uwasilishaji wa hoja.

1. Unasema "....na tuweze kusafirisha bidhaa zetu kwa wepesi, zifike kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kwa wakati...." Wakati huo huo unaponda uboreshaji wa makutano ya Ubungo. Hivi hujui makutano haya upitisha bidhaa zitokanazo na shughuli za watu wa bara zikiwemo na mazao ya wakulima. Hivi unajua mkulima wa nyanya Iringa, viazi Mbeya mchicha,ndizi, na kabichi Morogoro anaathirika kwa kiasi gani kifedha kutokana na foleni ya Pale UBUNGO!?

2.Unasema"..... Mimi serikali iboreshe miundombinu c, tupate pembejeo kwa gharama nafuu, tulime kwa wingi (massive production) ili tuweze ku enjoy economies of scale...".

A) Hivi Serikali inachokifanya UBUNGO, ujenzi wa SGR,uboreshaji wa viwanja vya ndege na kujenga vipya, vivuko na meli kuboreshwa na kuongezwa,ujenzi wa barabara na mambo mengi kama hayo, siyo uboreshaji wa miundombinu!? Hivi mnajua mnachokitaka lakini ama mko JF kukusanya 'thanks'?

B) Utapataje pembejeo kwa gharama nafuu ili ulime kwa wingi wakati fedha nyingi za kigeni unazimalizia kununua nishati isiyo na tija kwa matumizi ya foleni, ikiwemo na ya hapo Ubungo!?
Likes ama siku hizi thanks zinazotokana na matumizi yako ya lugha isiyo na staha hazikusaidii wewe, mkulima wa chikichi Kigoma wala hazisaidii Taifa letu Tanzania. Ukweli zinakudhalilisha.
 
Mkuu Mkwaha kama wewe ni mgumu wa kuelewa sio kosa langu. Nimejieleza vizuri. Lakini utofauti wa mawazo unakubalika hasa katika nchi yetu ya kidemokrasia Mama Tanzania.
Nimekuuliza hayo maswali makusudi tu ili kupima uelewa wako kwenye suala mzima la sheria za uchaguzi. ila kwa nilichojibiwa moja kwa moja Inaonyesha ndugu yangu Umekunywa maji ya bendera ya kijani na njano.
 
Acha ashinde tu bila kushindana kwa maana yeye ndio yeye na apangiwi na hashauriwi, Mr never told!
 
Pascal Mayalla usifikirie kuwa huyo unayempamba hivyo ni mjinga kwa kiasi unachomfikiria. Yeye binafsi anatambua kuwa yote ni Propaganda ndiyo maana anatumia nguvu za ziada na za hovyo.
Ingekuwa hayo yote unayoyataja yameleta tija hata robo asingekua analiogopa sanduku la kura kwa kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom