Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Jiwe kachizi, laiti angejua asingesumbuka na upinzani kwa kutumia nguvu bali akatumia akili angekua sa hivi ana support ya kila mtu. Ujuaji wake umemfanya sa hivi kabaki anapendwa na wanaomuogopa au vilaza tu. Mtu yeyote mwenye akili timamu anamuona ovyo, ndiyo atashinda kwa nguvu au hata bila nguvu nyingi atashinda kwa kua vilaza ndiyo the majority Tanzania ila hatuendi popote, anazidi kujinufaisha mwenyewe tu nchi ipo palepale au inazidi kugawanyika. Ovyo sana yule jamaa level za yule tako wa venezuela, anahisi anafanya sawa kumbe anavuruga
 
Mohamed Said,

Asante sana Mzee Mohamed Said, uchambuzi wa kisayansi kabisa huu, na jibu li wazi, "intervening cause".
Huyo aliyeweka hiyo "intervening cause" anaogopa nini kama anajiamini chama chake kimefanya kazi nzuri katika hii miaka 4? Kampeni yote aliyofanya kwenye mikutano ya hadhara ambayo washindani wake amewakataza, makala za redio na TV zinazomwimbia sifa kedekede, nini kinamtisha mbele ya watu ambao alishawaziba pumzi?
 
Mohamed Said,

Sikubaliani sana na hii hoja.

Huu ni mwendo wa kuviziana; mtu mwenye nguvu, nia mbaya na dhamira kubwa akiamua kukutega kwa namna yoyote atakupata tu. Kwenye uchaguzi mdogo wa Korogwe msimamizi si alitoroka ofisi ili asipokee fomu za wagombea lakini ya ccm akaipokelea chooni? Wasimamizi wa uchaguzi huu waliitwa Ikulu for the first time in history na karibu na uchaguzi! Bila shaka kikubwa walichoitiwa ni uchaguzi.

Prof. Lumumba amedai kuwa hawajaitwa kwa ajili ya maendeleo vinginevyo hicho kikao kingefanyika mara baada ya uchaguzi 2015! Bila shaka yoyote pia moja ya mambo yaliyofanyika kwenye mkutano huo ni kuwafundisha namna ya kutumia sheria kukibeba chama chenye serikali. Kwa mkakati huo mgombea akijaza ACT Wazalendo ni kosa; chama hicho hakipo. Katibu wa Itikadi wa ccm alikuwepo kwenye mkutano huo na kwa jinsi Mbunge zilizotumika zilivyokuwa "shallow and trivial" sitashangaa kama zimebuniwa Lumumba.

Na baada ya kukubaliana hivyo bila shaka uliwekwa utaratibu wa kufanya wagombea wa ccm kupunguza hayo makosa madogo madogo yatakayotumika kuwaengua washindani wao. Na kwa vyovyote vile, hata wangefanya hayo makosa ccm hawawezi kuenguliwa!.
 
Pongezi kwako P kwa andiko zuri.
Na maswali 2 kwako.
(1) ni kweli kua huna kadi ya chama?
(2) umeyaandika haya kutoka moyoni mwako?
Mkuu Mbeba Maono,
Kwanza asante kwa pongezi zako.
1. Sio tuu ni kweli sina kadi ya chama chochote cha siasa, bali sijawahi kujiunga na chama chochote, sio mfuasi wa chama chochote na sio mshabiki wa chama chochote.

Kwa sasa niko over 50, baada ya kuhudumu kwenye habari kwa miaka 30, sasa ni wakati wa kustaafu hivyo nami najipanga kurudisha kidogo kwenye jamii kwa kuwatumikia wananchi, nana Bora kabisa ya kuwatumikia wananchi ni kujitolea kuwa mtumishi wao.

Kwa vile kwa Tanzania ili kuwatumikia wananchi ni lazima ujiunge na chama cha siasa, hivyo nami nikistaafu uandishi wa habari, nitalazimika kujiunga na chama cha siasa kuwatumikia wananchi, kama wakati huo ukifika Tanzania tutakuwa tumeruhusu mgombea binafsi, then mimi nitasimama kama mgombea binafsi kuwatumikia wananchi.

2. Hili la kuandika kutoka moyoni naomba nisilijibu bali nikufundishe kitu na wewe ili next time kuna maswali ukijiuliza unajijibu mwenyewe sio mpaka kuuliza.

Namna ya kujua kama mwandishi ameandika kutoka moyoni au amejiandikia tuu kwasababu anaweza kuandika, ni kupitia kwako wewe msomaji moyo wako umekuambia nini baada ya kusoma bandiko hili.

Kuusikilizia moyo kwenye maandishi ya mtu kunaitwa "reading in between the lines " huu ni uwezo wa kusoma andiko na kujua mwandishi alidhamiria nini, ukimaliza kusoma na kutafakari ni wewe mwenyewe ndio utagundua kama mwandishi alidhamiria or was just paying lip services.
P
 

Hoja ya mafuta nayo ni dhaifu....

Jenga hoja ya kushawishi na kueleweka, sio habari za mafuta.
 
Pascal Mayalla,
.Mkuu unapotoka hapa. Vyama vya upinzani kama havikufanya training kwa wagombea wao hilo sio tatizo la Chama Cha mapinduzi. Hatuwezi kuwa na viongozi ambao hawawezi hata kujaza form za kugombea nafasi za uongozi. Ndio sababu kubwa Mwalimu Enzi zake alipeleka watu Gumbaro ili waendane na wakati. Uchaguzi utafanyika na JPM hawezi kuingilia. Vyama vya upinzani wajipange upya hapa kazi tu.
 
Kuishi kwingi kuona mengi tunaposema uongozi haujalibishwi tunamanisha kutokumjalibisha mtu katika uongozi Mkubwa Kama RAIS Tanzania ni kubwa kuriko RAIS rakini kwasababu tunachagua kwakufanya majalibio acha tusoteshwe kwenye inchi yetu wenyewe tumepokwa hata ile kusema hili Hapana inamana hata Huko ccm hawayaoni Haya wanamuona magufuli Kama kashuka toka mbinguni Kumbe tupo nae miaka yote hata nyumba zetu aliuzia hawala na ndugu zake. Dah Ngoja niishie Hapa japo inatia uchungu Sana
 
Pascal Mayalla,
Aache ukandamizaji. Asiongoze nchi hii kwa mihemko yake ambayo kwa sasa inazidi kushangiliwa na vibaraka wachumia tumbo waliomzunguka, wakiwamo hata wasomi ambao wanajipendekeza kwa kujinasibu kuwa waliokotwa 'jalalani'.
Anakotupeleka bado kidogo kutaifanya nchi yetu ifikie hali ile waliowahi kuwa nayo SA, Zimbabwe, Mozambique, Angola, Guinea Bisau, Cape Verde etc.ambayo Tanzania (iliyoongozwa na Nyerere) ilisaidia kuwakomboa. Mgonjwa wa malaria sugu anahitaji tiba ya haraka na SIO kumuomba aonje kwanza Dawa. AMEN
 
Nimekuuliza hayo maswali makusudi tu ili kupima uelewa wako kwenye suala mzima la sheria za uchaguzi. ila kwa nilichojibiwa moja kwa moja Inaonyesha ndugu yangu Umekunywa maji ya bendera ya kijani na njano.
Nimekuwa mchambuzi wa kanuni na taratibu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na 2019 kwenye Redio FM za huku kwetu. Kwahiyo sio mgeni kama unavyonifikiria.
 
nikuteue nikupe nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani - Pascal haya maneno uliyasoma na kuyachambua kwa ufahamu wa kiasi gani, imagine upo kwenye hii ajira na umeipokea - What will u do?
 
Umenikumbusha bao la mkono
 
Who knows km yy no1 ndo alitoa maekekezo hayo na yanamfurahisha? Kumbuka alishawahi kusema hataki upinzani ktk wake. Nakumbuka vizuri kaka pascal uliwahi muuliza katumia sheria gani kufuta mikutano ya siasa na alikujibu blaa blaa kwamba mayala kwao ni njaa, ss huyo hawezi kuingilia haya maana yanamfurahisha na inawezekana yana baraka zake.
 
Pascal Mayalla,

Muhimu sana kuacha uchaguzi uwe huru. Upinzani ukishinda sehemu flani inamaanisha wananchi wanawaamini. Labda wamefanya vitu vya maana.


Serikali ijikite kuleta maendeleo, maji, umeme, barabara, elimu, Afya, baadaye makazi bora, kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, wakulima wawe wakubwa, ili watoe ajira kwa vijana.

Time is most important asset for human being, (binadamu). How your use time, money,where, when, in what projects is very important, Crucial.

Serikali itumie muda wake kwa mambo yatayowasadia Watanzania wengi.

Wapinzani wakipata viti asilimia tano, kumi, sio kesi.

Muhimu ku- avoiid distractions, kutoyumbishwa, kuwekewa vikwazo.
Serikali should, must, is necessary, inabidi to focus on important issues.
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…