Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza tatizo na kulitatua ili apate umaarufu zaidi. Sitashangaa nikisika Dr Abasi akisema “Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli amewasamehe wote waliojaza fomu kimakosa”.

Je, rais akifanya hivyo atakuwa katimiza wajibu wa sheria ya Uchaguzi? Kwa kifupi na kiungwana Pascal anajaribu kuzungumzia uwepo wa Tume huru na Katiba mpya kitu ambacho hakuna Rais mstaafu au aliyeko madarakani anayetaka CCM imfie mikononi mwake. pascal
 
Ku dili na mawe ni shida sana, ni kwanini Jafo amesema majina yatabandikwa hata kama vyama vimejitoa?
Kama wana vigezo vyote majina yao yatabandikwa. Ni utaratibu na kanuni za uchaguzi. Wao hawafuati porojo za vyama kujitoa ingawaje wenye majina yatakayobandikwa wana hiari ya kufanya kampeni au la. Kimbembe kitakuwa endapo watashinda, Chadema itawatambua? Itawafukuza? Tunasubiria!
 
Je rais akifanya hivyo atakuwa katimiza wajibu wa sheria ya Uchaguzi?....kwa kifupi na kiungwana Pascal anajaribu kuzungumzia uwepo wa Tume huru na Katiba mpya kitu ambacho hakuna Rais mstaafu au aliyeko madarakani anayetaka CCM imfie mikononi mwake pascal
CCM kutokuwa madarakani si kifo chake Bali utakuwa muda mzuri wa kukiimarisha chama. Chama tawala kikikaa madarakani muda mrefu kinapoteza dira na kufanya kazi kwa mazoea.
 
Mkuu Paskali, hii post yako ya Leo nimelazimika kuipa like zaidi ya 100

Umeanza kututhihirishia kuwa umeanza kurudi kuwa Paskali wa enzi zile na umebaini kuwa ukiwa mtu wa "Praise and worship for Magufuli " kwa kila kitu, tunalipoteza Taifa letu

Big up sana Mkuu
 
Magufuli lengo lake nchi ilirudi kwenye utawala wa chama kimoja, na kwa mwaka 2020 Hakuna mbunge wa upinzani atakae rudi bungeni labda Mbatia sababu ni mtu wa syteam, mi naona tuache iwe ivyo kama anavyotaka muheshimiwa rais na praise team kina Mzee Mwanakijiji.

Labda tukirudi mfumo wa chama kimoja na fikra zinazolingana nchi yetu itakuwa kama ulaya kimaendeleo
 
Pascal Mayalla siamini katika hoja yako. JPM hawezi kuzuia upinzani kushiriki siasa kwani atakua kinyume na sheria ya vyama vingi.

Anachotakiwa kufanya ni kutoa kauli kwa watendaji wake wanaominya demokrasia.

By the way, upinzani ni imara kiasi gani?
 
Sitaki kuingia ndani kwenye technicalities zilizopelekea wagombea wa upinzani kuenguliwa, bali natoa wito kwa rais Magufuli aingilie kati hali hii au yeye mwenyewe kama rais wa JMT, au kupitia kwa Waziri Jaffo wa Tamisemi, ayafute makosa yote ya wagombea wote wa vyama vyote walioenguliwa kwa sababu zozote, ziwe ni za kweli za halali.
Hapa ndiposa mnishangazapo baadhi watanzania. Mwasema tufuate katiba na taratibu tulizojiwekea ili kujenga mfumo imara wa kuheshimu katiba na sheria, wakati huo huo mnashauri Rais avuruge ufuataji wa sheria na katiba katika suala ambalo linatoa nafasi kubwa kwa watanzania kujua umuhimu kufuata katiba, sheria na taratibu nyingine tulizojiwekea. Mna malengo gani enyi baadhi ya watanzania!?
Mkuu, Paskali, ni lini hasa unataka uione Tanzania inaanza kufuata taratibu, sheria na katiba kwa kumaanisha hasa kama siyo wakati wa awamu hii ya tano!?🙂🙂🙂
 
Mambo mengi ya Nchi kwa sasa yame kuwa yakiendeshwa kwa Hisani ya Mtu mmoja ,Katiba tuliyo Apa kuilinda ipo likizo hasa kwa Dhana uliyo igusia ktk bandiko lako kwa namna ulivyo muomba Mh Mtukufu sana wa Nchi.

Na hizi ndio fikra za Watawala walio Madarakani ,ktk kuwaletea Wananchi wao Maendeleo。
 
Nchi inahitaji maendeleo ya watu ...tumejichelewesha sana kusaka kiki za demokrasia kwani ndio upuuz waliotaka tuufikirie.
Ndege zinatumiwa na only 0.8 ya Watanzania.
Daraja la juu la ubungo litanisaidia Nini mkulima wa chikichi Kigoma?
Daraja la baharini linamsaidiaje mtu wa Newala?
Magufuli amewekeza kwenye vitu visivyo na faida.
Miradi yenye faida Ni ya maji, barabara, na umeme.
Lakini miradi Kama ya Coco Beach Ni u hunsa kabisa
 
Yani ccm wangesoma case study ya Gsddafi،aliwafanyia Kila kitu ila aliwaminya katika Uhuru wao. Kwaio yote mazuri hayakuonekana na wakamuua.

Sasa reli, madaraja, mabarabara hayataonekana ktk hizi figisu.

Kuna tetesi za ugonjwa badala ya kusikitika watu walifurahi hio ilokua indicator mbaya. Hatujifunzi. Owky hakuna marefu yasio na mwisho
Swali zuri sana! Unasema unajenga reli nzuri, meli, ndege safi, flyover, umeme rufiji nk na kuhisi unapendeka sana. Lakini anajitokeza "mwehu" mmoja anaanzisha uzushi kuwa u mgonjwa taabani au umetangulia mbele ya haki na hao uliodhani wanakupenda wanageuka washangiliaji au wanatabasamu kwa habari hizo bado utaendelea kusema hayo uliyofanya ndio mahitaji ya wananchi wako? Huwezi kubaki na fikra hizo kama unatumia akili.
Huo mfano wa Gaddafi ndio sahihi kabisa, na hilo linadhibitisha kuwa kama uchaguzi ni wa haki na huru uwezekano wa CCM kuambulia hata 30% ni mashaka.
Pascal, hivi kiongozi mtaani kwangu namjua ni mpenda rushwa, kiburi na hana maono utendaji wa Magufuli unambebaji katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa?
CCM wamejiwahi, walikuwa wanagaragazwa haijapata kutokea katika historia yake.
 
Back
Top Bottom