Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Jaffo alie kwa lipi??wewe susa sie twala
Mkuu Jingalao, huu usemi japo mchungu lakini ndio ukweli wenyewe, kama ilivyo kwa penzi ni kama kiti cha basi, unaposhuka, anakaa mwenzio, na ganda la mua la jana, chungu aona kivuno, ukisusa, wao wala!. Kabla hata ya uchaguzi, CCM itakuwa imeshinda ushindi wa mezani kwa more than 75%, uchaguzi ni kukamilisha tuu ile 25%.
P
 
Pascal Mayalla,
Nakubaliana na hoja yako ya kuwaombea wagombee hata kama wamekosea. Na wamesamehewa. Ila tuwashauri wajenge taasisi iliyo na network imara ya utendaji. Sio kila mara will depend on mercy.
 
pascal sidhani kama hivyo unavyovielezea vinagusa maisha ya mwananchi wa kawaida. Na kama ccm inaamini itapanda ushindi wa kishindo basi waruhusu uchaguzi huru waone kitakachowakuta.
 
Mkuu Zawadin, kama sababu za kujitoa ni kitendo cha wagombea wao kukatwa, sasa wagombea wote wamerudishwa, kwanini waendelee kujitoa?.
P
Kwa sasa sina hakika kama wataendelea na msimamo wa kujitoa; ila hawa wajitoe wasijitoe ule mkakati wa kuhakikisha chama tawala kinachukua ushindi, kwenye hayo maeneo ambayo wapinzani wamesimama bado upo pale pale. Niliposema too late nilikuwa naliona hilo. Wapinzani walitakiwa kuwa na msimamo mapema na sio kubadilisha gia angani. Wakitaka uzoefu wawaulize wapinzani kule Zanzibar watajua what CCM is.
 
Nirudi kwa Paskali..inawezekana vipi leo unatuambia kua Serikali ya CCM huku Katiba ikitamka kua ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Mkuu Bishweko, kwanza asante kwa swali zuri tena ni swali la msingi sana na jibu la swali hili ndilo linaifanya CCM ishinde chaguzi zote na CCM itatawala milele Tanzania, unless katiba ya sasa ibadilishwe.

Kwa mujibu wa Katiba, Serikali ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni serikali ya Watanzania wote sio serikali ya mtu wala serikali ya chama fulani.

Ndio maana katiba ikatamka kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea, yuko huru kushiriki kugombea uongozi toka wa serikali za mitaa hadi serikali kuu. Hiyo ndio ilikuwa dhima ya mtunga katiba.

Wakati wa Chama kimoja, kukaibuka shana ya chama kushika hatamu za uongozi wa serikali, party supremacy hivyo tukawa na chama dola. Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ilitengenezwa katika msingi huo ambapo Bunge la Chama kimoja CCM, lilijigeuza a constituency assembly na kuipitisha Katiba hiyo within 45 minutes, hivyo kuwa na katiba ya JMT yenye mfumo wa chama dola. Chama ndicho kinashika hatamu za kuongoza serikali.

Tulipoparamia mfumo wa vyama vingi tulipaswa kwanza kuibadili katiba kuondoa chama dola na kujenga mfumo wa parliamentary supremacy, kwa Bunge ndilo liwe supremacy kwasababu Bunge ndio wawakilishi wa watu. Hili halikufanyika.

Hivyo tuna nchi ya vyama vingi na katiba ya neno vyama vingi lakini ni katiba ya chama kimoja tena ni chama dola, CCM, na ndio maana CCM itatawala milele.

Haki ya wananchi kushiriki kwenye siasa imeporwa kwa kulazimisha ili kuchaguliwa ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa, hivyo kujiunga na chama cha siasa ni lazima uwe mwanachama.

Serikali inaundwa na chama kilichoshinda uchaguzi Mkuu na chama hicho kinashinda kutokana na kuinadi ilani yake ikakubaliwa. Kwa sasa chama kilichoshika serikali ni CCM hivyo hii serikali ya Tanzania, japo kikatiba na kwa jina ni Serikali ya JMT ila kiukweli ni serikali ya CCM.

Hili niliwahi kulizungumzia

P
 
'Kutokana na kasi ya rais Magufuli kutuletea maendeleo ya vitu vya kuonekanika, Midege, Reli ya SGR, Mabarabara nchi nzima, madaraja ya Juu kwa Juu, Mradi wa umeme wa Stigler , Tanzania ya Viwanda, Elimu Bure, Vituo vya Afya kila kuna, etc, etc, just to mention but few, vinaipa CCM fursa ya ushindi wa kishindo cha wazi kabisa katika uchaguzi wowote nchini Tanzania kati ya sasa hadi 2025, hivyo mamlaka zinazosimamia uchaguzi huu, waruhusuni wagombea wote waliopitishwa na vyama vyao wapite tuu bila kujalisha kama wanekidhi sifa na vigezo, ili tuu kuruhusu ushindani wa haki, ushindani wa uwazi na mshindi apatikane kihalali katika uchaguzi huru na wa haki'.

Nimekuelewa vizuri mkuu Pascal Mayalla
Hili haliwezi kutokea kwa CCM.
Wanasema ukila nyama ya mtu huwezi acha
 
Dunia inaenda kwa kasi sana...Ni kweli kila uongozi uliochaguliwa unatekeleza miradi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake..Rais Magufuli amefanya mengi kama ulivyoyataja....nachokiona katika Ulimwengu wa sasa ambao serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) inajidanganya nacho ni Kwamba haijui dunia ya sasa inaenda kasi na inashikwa hatamu na vijana..Vijana wa Leo wengi hawahitaji ndege, barabara,reli wala kitu kingine...vijana wa sasa wanahitaji ajira, wanahitaji kuwa na uhuru wa kupata taarifa na kutoa maoni yao kwenye mitandao na sehemu zingine ...JK hakufanya yote hayo ambao Magufuli amefanya lkn alijua kuendana na vijana (dunia ya sasa )

Vijana wa sasa kwamba hawakiitaj chama cha mapinduz ila wanaona wanataka changamoto mpya, yaani babu na bibi zao walikua CCM baba na mama zao ni CCM kwenye hii dunia sasa na wao wawe CCM haitoshi...kasi ya Mabadiliko ya kiulimwengu inakataa kuipenda CCM.

Ghaddaf alitoa kila kitu NCHINI kwake lakini vijana katika Ulimwengu wa kiteknolojia walisema haitoshi, tunahitaji uhuru wa kujieleza wa kutoa maoni yetu ...

KIZURI CHAJIUZA ,KIBAYA CHAJITEMBEZA .
 
Acha uongo kusema ulikuwa bize. wakati kila mara ulikuwepo humu kufufua nyuzi zako mfu!!
Mkuu Flulanga, kila mtu mwenye kujua kusoma na kuandika anaweza kusoma chochote na kuandika chochote, ila binadamu tumetofautiana uwezo wa kuandika na kuelewa, wengine wanaweza kuandika chochote muda wowote hata akiwa kwenye dala dala, sisi wengine ili kuandika baadhi ya vitu unahitaji kutulia kutafakari ndipo uandike, wiki jana nzima nilikuwa Dodoma na Azaki.

Hakuna nyuzi may, kitu ukiisha kiandika kinaendelea kuwa hai hivyo hata ufukuaji wa makaburi sio kufufua wafu bali kuwatia uhai kwa kusikiliza sauti zao.

P
 
Bora umemwambia wazi. Pascal ni mhuni wa kisiasa, ni mwandishi mtafuta fursa wa kiwango cha juu. Anaandika kwa kulembalemba ili aonekane mwema kwa kaka yake. Ni eneo gani nchini ambako CCM yake haijatoa maelekezo kwa watendaji kukata majina ya Wapinzani? Leo anajifanya mwema anauma na kupuliza? Aache unafiki, kama ni mkweli auseme ukweli wote na siyo mafumbo na kujitafutia sifa binafsi.
Mkuu Bila Bila, mimi ni mkweli daima na nilichokisema humu ni ukweli mtupu.
P
 
Busara imemezwa na 'mabavu'. Kila mtu wakiwemo watendaji wa serikali ngazi zote wanapimwa kwa mfumo wao wa 'mabavu' wanaoutumia kuongoza. Ikiwa hujafanya 'mabavu' wewe si mtendaji hodari. Wala huhitaji kufanya utafiti kujua haya. Yanasemwa na kusifiwa na viongozi wakuu wakisifia wanaotumia mabavu na kukosoa wasiofanya hivyo.

Chaguzi hizi zimevurugwa kwa sababu ya watu wote walio katika madaraka kutaka kupata sifa ya kuwa 'viongozi bora'. Wakaiga mfumo wa uongozi uliopo sasa wenye sifa na kuacha busara pembeni. Unawezaje kukubali kwamba miaka karibu 30 ya chaguzi hizi kuna kundi halijui kujaza fomu na hivyo kukosa sifa na kundi jingine ni smart 100%? Miaka karibu 30 ya chaguzi hizi tunatumia mchakato kuwazuia wagombea na kuwanyima wananchi haki ya kuchagua viongozi wao! Miaka zaidi ya 60 ya uhuru na elimu ya msingi kwa wote tunajisifia kuwa kuna watu hawajui kujaza fomu tulizozisanifu wenyewe kwa lugha yetu inayozungumzwa na wananchi wetu!

Bahati mbaya pia kuna maagizo ya bayana na ya nyuma ya pazia kuhakikisha ushindi kwa kundi fulani. Hii inawapa taabu sana watendaji wanaotaka angalau kutumia busara kidogo waliyobakiza. Ni ujinga kufikiria kuwa utakuwa kiongozi mzuri mwenye mafanikio ikiwa utashinda changuzi ngazi zote kwa asilimia 98%. Hata manabii hawakupendwa kiasi hicho lakini wamebaki kuwa na sifa bora mpska leo. Mfalme Daudi na Mfalme Selemani walikuwa na wapinzani. Je hawabaki kuwa wafalme wenye kumbukumbu nzuri kwa watu wote?
 
w
Kama wana vigezo vyote majina yao yatabandikwa. Ni utaratibu na kanuni za uchaguzi. Wao hawafuati porojo za vyama kujitoa ingawaje wenye majina yatakayobandikwa wana hiari ya kufanya kampeni au la. Kimbembe kitakuwa endapo watashinda, Chadema itawatambua? Itawafukuza? Tunasubiria!
wanakuaje na vigezo? ikiwa kwanza wamekosea kuja fomu.. pili hawana chama? je? wagombea binfsi wameanza kuruhusiwa tz? ama kweli siku ya kutembea uchi ndio hiyo hiyo utakutana na mkweo .fedhea kubwa hii
 
Wanabodi,

Tangu kuanza kwa pilika pilika za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sijawahi kuzungumza lolote kutokana na kuwa bize na shughuli za kitaifa, kwanza ni Wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika kitaifa mjini Bariadi Mkoani Simiyu na kufuatiwa na Wiki ya Azaki iliyomalizika jana Jijini Dodoma, hivyo leo ndio nimepata fursa kuendelea na zile makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa".

Mada kuu kuhusu makala ya leo ni hizi figisu figisu za uchaguzi serikali za mitaa zilizopelekea Chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema, kujitoa kikifuatiwa na Chama cha ACT.
This is not good at all kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.

Sitaki kuingia ndani kwenye technicalities zilizopelekea wagombea wa upinzani kuenguliwa, bali natoa wito kwa rais Magufuli aingilie kati hali hii au yeye mwenyewe kama rais wa JMT, au kupitia kwa Waziri Jaffo wa Tamisemi, ayafute makosa yote ya wagombea wote wa vyama vyote walioenguliwa kwa sababu zozote, ziwe ni za kweli za halali au ni figisu, watoe amnesty kila aliyegombea apitishwe tuu hivyo hivyo despite all the odds ili Tanzania tuingie kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu Mwakani kwa Ushindani wa haki, uwazi na Usawa kwa vyama vyote kutendewa haki sawa, hivyo waliosusa wote warudi.

Ushindi mnono na mtamu ni ule ushindi unaotokana na ushindani wa haki unaopatikana uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, level ground na sio uwanja tange, wala sio ushindi wa mezani!.

Kwa observation yangu, kwa kasi ya rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, JPM, kwa haya tuu aliyowafanyia Watanzania kwa miaka hii minne tuu tangu alipoingia madarakani, na mambo anayoendelea kuyafanya kila uchao, ni mambo mkubwa kuliko rais mwingine yoyote ayeyewahi kufanya, ukimuondoa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyetupatia uhuru na kutujengea Umoja, Upendo na Mshikamano wa Watanzania kuwa kitu kimoja, Taifa moja lenye umoja, lisilo na ubaguzi wa udini, ukabila, rangi, jinsia na hali.

Kutokana na kasi ya rais Magufuli kutuletea maendeleo ya vitu vya kuonekanika, Midege, Reli ya SGR, Mabarabara nchi nzima, madaraja ya Juu kwa Juu, Mradi wa umeme wa Stigler , Tanzania ya Viwanda, Elimu Bure, Vituo vya Afya kila kuna, etc, etc, just to mention but few, vinaipa CCM fursa ya ushindi wa kishindo cha wazi kabisa katika uchaguzi wowote nchini Tanzania kati ya sasa hadi 2025, hivyo mamlaka zinazosimamia uchaguzi huu, waruhusuni wagombea wote waliopitishwa na vyama vyao wapite tuu bila kujalisha kama wanekidhi sifa na vigezo, ili tuu kuruhusu ushindani wa haki, ushindani wa uwazi na mshindi apatikane kihalali katika uchaguzi huru na wa haki.

Nakumbuka nilipokuwa Baba Kijana, nilikuwa nikicheza na watoto wangu michezo mbalimbali kama kukimbia, mnashindana kukimbia, ili kumjengea mtoto ari ya kushinda, wewe unakimbia kidogo kidogo ili usimshinde mtoto ukamvunja moyo, unamuacha mtoto akupite na akushinde na akiisha shinda, anafurahi kweli kweli kuwa amemshinda baba!. Hivyo tukubali tukatae, kwa hali ya sasa ya siasa zetu na hii kasi ya JPM, ili Tanzania tuendelee kuwa ni nchi ya vyama vingi, kuna maeneo CCM inabidi tuu ijifanye baba anacheza na watoto kwa kuwaachia tuu washinde, vinginevyo ni tunarudi kwenye nchi ya chama kimoja!.

Hivyo natoa wito kwa serikali ya CCM, chini ya Jemedari wake, JPM, kiukweli labisa, hata kabila ya uchaguzi, CCM tayari imeishashinda kwa ushindi wa kishindo sio tuu huu
Uchanguzi wa Serikali za Mitaa, bali hadi Uchanguzi Mkuu ujao wa mwakani 2020 kutokana na sababu za ki political social dynamics ya Magufulification, lakini ili CCM iweze kuufurahia huo ushindi kwa fursa ya kweli na hivyo kusheherekea ushindi huo, kazima CCM ishinde kwenye ushindani wa kweli na sio kuchukua mpira kwapani, au kufanya figisu ushindani wasuse, wewe upewe ushindi wa mezani.

Nakuomba Rais Magufuli na Waziri Jafo, jifanyeni kama mnacheza na watoto, wafungulieni njia watoto wote washiriki kwenye uchaguzi huu kwa uhuru na kwa haki sawa kwa vyama vyote despite mapungufu walionayo ili hata uchaguzi Mkuu wa mwaka kesho, wakati Watanzania watakapo irejesha Tanzania kwenye mfumo wa Chama kimoja CCM, iwe ni Watanzania wenyewe ndio wameamua kupitia uchaguzi huru na wa haki ulioendeshwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi ulioendeshwa kwenye uwanja sawa na tambarare, na sio CCM ishinde katika ule ushindani wa kugombea kisu cha makali kuwili, huku mshindani mmoja ameshika kwenye mpini. Hivyo CCM ishinde kihalali kwa Miami wa kazi nzuri ya rais JPM na sio kwa sababu ndio iliyokamata mpini.

Tena kwa maoni yangu uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaosimamiwa na TAMISEMI ndio uwe wa mwisho, tubadili sheria zetu za uchaguzi, uchaguzi zote zisimamiwe na sheria moja, chini ya Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, zuio la mikutano ya siasa liondolewe, wagombea huru waruhusiwe ili hata watu kama akina sisi tusio wanachama wa chama chochote, tuweze kushiriki kugombea, hivyo uchaguzi wa 2025 tuchague viongozi wa serikali za mtaa, madiwani, wabunge na rais kwa siku moja. Hoja kuwa zitakuwa kura nyingi haina mashiko. Kwenye uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kila mpiga kura anapiga kura 5 kuchagua
  1. Diwani,
  2. Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
  3. Mbunge wa Bunge la JMT
  4. Rais wa Zanzibar
  5. Rais wa JMT
Hivyo Tanzania tukiamua kufanya uchaguzi huru na wa haki, unaofusta mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia ya ukweli, tunaweza. Mimi naamini kabisa kwa mambo makubwa na mazuri ya Rais Magufuli anayoyafanya, We have nothing to loose rais Magufuli akiruhusu demokrasia ikashamiri, akatoa haki sawa kwa vyama vyote kufanya siasa ikiwemo kuondoa zuio la mikutano ya siasa, bado rais Magufuli anaweza kuyaleta maendeleo yote aliyokusudia at the same time huku akiruhusu demokrasia nayo ishamiri, ila ukweli utaendelea kubaki ni ukweli daima kwa katiba hii na kasi hili ya rais Magufuli, CCM bado itaendelea kutawala Tanzania milele.

Naomba nimalizie kwa ile kauli ya thread hii
"Ushindi Mtamu ni Ushindi Unaopatikana kwa Ushindani Wa Haki Kwenye Uchaguzi Huru na Wa Haki, Unaendeshwa na Tume Huru na Shirikishi, na Unaofanyika Kwenye Uwanja Sawa wa Ushindani wa Kisiasa, Sio Ushindi wa Mezani!. Mheshimiwa Rais, Dr. John Pombe Magufuli, aka.JPM, Kasi Yako ya Maendeleo ya Tanzania Unaoifanya, Utailetea CCM Ushindi Kishindo Katika Uchaguzi Wowote, Tunakuomba Please Please Please, Ruhusu Tuu Ushindani wa Haki, Wazi na Usawa Kwa Vyama Vyote,
Utabarikiwa Zaidi na Zaidi, na Tanzania Tutabarikiwa.

Nawatakia Jumapili Njema
Na mimi nawahi kanisani
Misa ya Kwanza pale kanisa langu la St.Peters

Paskali

Pascal a.k.a Njaa kali.
Katika michango na mada ambazo umewahi kuzileta hapa ukumbini hii nikiri kukupa kudo's...!!
Hakika inapendeza na imekaa vizuri.....naamini kama homeboy wako atakuwa ameipitia atagundua kwamba wakti mwingine huwa huongei pumba...!!! Naona Jafo ameanza kuifanyia kazi kwa kuamru wagombea wote walioneguliwa kwa technicalities za KIHUNI warudishwe kwa kufutiwa hayo makosa eti madogo madogo....!!!

Kwa mtazamo wangu bado hili halitaweza kutiba DONDADUGU iliyotengenezwa na Chama Twawala. Tangu mwanzo kabisa wa mchakato wa Uchgauzi wa SM kulikuwa na figisu nyingi sana ambazo zilikuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha WAPINZANI hawafurukuti...!!! Hata kama leo wagombea wote wa Vyama pinzani: CHADEMA, ACT WAZALENDO, NCCR-Mageuzi, CUF na UMMA wataruhusiwa kurudi kwenye kinyang'anyiro haitasaidii lolote...!!!
Lazima wapinzani wajue kwamba DAFTARI LA WAPIGA KURA WA UCHAGUZI huu wa SM siyo rasmi limejaa wapiga kura hewa kwa ajili ya kuibeba CCM....Hivo kitendo cha wapinzani kurudi uwanjani itakuwa ni kupoteza muda na pesa kwa Uchaguzi ambao ulisha andaliwa kwa ajili ushindi wa CCM...!!!

Laiti Wapinzani wangelijua kwanini Rais Magufuli aliamua kuwaita Watendaji wa Kata zote nchini kwenda Ikulu mwezi wa 8 ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi wa SM. Lazima kulikuwa na maelekezo maalumu kwa Watendaji hawa ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika hali yoyote ile. Nina hakika walishaambiwa kama ikitokea Mpinzani akashinda kwenye Kata ya Mtendaji ajihesabu hana kazi...!!!

Walichokiamua Wapinzani ni sahihi kabisa kwa vile tangu mwanzo Serikali ya Magufuli ya CCM haikutaka kuandaa Uwanja sawa wa mapambano(Fair Game on the same Pitch).....!! CCM walisha amua kuua upinzani kabla ya 2020 ili kenye Uchaguzi Mkuu wa wapinde bila kupingwa maana watakuwa hawana mpinzani...!!!
 
Back
Top Bottom