Wanabodi,
Tangu kuanza kwa pilika pilika za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sijawahi kuzungumza lolote kutokana na kuwa bize na shughuli za kitaifa, kwanza ni Wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika kitaifa mjini Bariadi Mkoani Simiyu na kufuatiwa na Wiki ya Azaki iliyomalizika jana Jijini Dodoma, hivyo leo ndio nimepata fursa kuendelea na zile makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa".
Mada kuu kuhusu makala ya leo ni hizi figisu figisu za uchaguzi serikali za mitaa zilizopelekea Chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema, kujitoa kikifuatiwa na Chama cha ACT.
This is not good at all kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.
Sitaki kuingia ndani kwenye technicalities zilizopelekea wagombea wa upinzani kuenguliwa, bali natoa wito kwa rais Magufuli aingilie kati hali hii au yeye mwenyewe kama rais wa JMT, au kupitia kwa Waziri Jaffo wa Tamisemi, ayafute makosa yote ya wagombea wote wa vyama vyote walioenguliwa kwa sababu zozote, ziwe ni za kweli za halali au ni figisu, watoe amnesty kila aliyegombea apitishwe tuu hivyo hivyo despite all the odds ili Tanzania tuingie kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu Mwakani kwa Ushindani wa haki, uwazi na Usawa kwa vyama vyote kutendewa haki sawa, hivyo waliosusa wote warudi.
Ushindi mnono na mtamu ni ule ushindi unaotokana na ushindani wa haki unaopatikana uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, level ground na sio uwanja tange, wala sio ushindi wa mezani!.
Kwa observation yangu, kwa kasi ya rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, JPM, kwa haya tuu aliyowafanyia Watanzania kwa miaka hii minne tuu tangu alipoingia madarakani, na mambo anayoendelea kuyafanya kila uchao, ni mambo mkubwa kuliko rais mwingine yoyote ayeyewahi kufanya, ukimuondoa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyetupatia uhuru na kutujengea Umoja, Upendo na Mshikamano wa Watanzania kuwa kitu kimoja, Taifa moja lenye umoja, lisilo na ubaguzi wa udini, ukabila, rangi, jinsia na hali.
Kutokana na kasi ya rais Magufuli kutuletea maendeleo ya vitu vya kuonekanika, Midege, Reli ya SGR, Mabarabara nchi nzima, madaraja ya Juu kwa Juu, Mradi wa umeme wa Stigler , Tanzania ya Viwanda, Elimu Bure, Vituo vya Afya kila kuna, etc, etc, just to mention but few, vinaipa CCM fursa ya ushindi wa kishindo cha wazi kabisa katika uchaguzi wowote nchini Tanzania kati ya sasa hadi 2025, hivyo mamlaka zinazosimamia uchaguzi huu, waruhusuni wagombea wote waliopitishwa na vyama vyao wapite tuu bila kujalisha kama wanekidhi sifa na vigezo, ili tuu kuruhusu ushindani wa haki, ushindani wa uwazi na mshindi apatikane kihalali katika uchaguzi huru na wa haki.
Nakumbuka nilipokuwa Baba Kijana, nilikuwa nikicheza na watoto wangu michezo mbalimbali kama kukimbia, mnashindana kukimbia, ili kumjengea mtoto ari ya kushinda, wewe unakimbia kidogo kidogo ili usimshinde mtoto ukamvunja moyo, unamuacha mtoto akupite na akushinde na akiisha shinda, anafurahi kweli kweli kuwa amemshinda baba!. Hivyo tukubali tukatae, kwa hali ya sasa ya siasa zetu na hii kasi ya JPM, ili Tanzania tuendelee kuwa ni nchi ya vyama vingi, kuna maeneo CCM inabidi tuu ijifanye baba anacheza na watoto kwa kuwaachia tuu washinde, vinginevyo ni tunarudi kwenye nchi ya chama kimoja!.
Hivyo natoa wito kwa serikali ya CCM, chini ya Jemedari wake, JPM, kiukweli labisa, hata kabila ya uchaguzi, CCM tayari imeishashinda kwa ushindi wa kishindo sio tuu huu
Uchanguzi wa Serikali za Mitaa, bali hadi Uchanguzi Mkuu ujao wa mwakani 2020 kutokana na sababu za ki political social dynamics ya Magufulification, lakini ili CCM iweze kuufurahia huo ushindi kwa fursa ya kweli na hivyo kusheherekea ushindi huo, kazima CCM ishinde kwenye ushindani wa kweli na sio kuchukua mpira kwapani, au kufanya figisu ushindani wasuse, wewe upewe ushindi wa mezani.
Nakuomba Rais Magufuli na Waziri Jafo, jifanyeni kama mnacheza na watoto, wafungulieni njia watoto wote washiriki kwenye uchaguzi huu kwa uhuru na kwa haki sawa kwa vyama vyote despite mapungufu walionayo ili hata uchaguzi Mkuu wa mwaka kesho, wakati Watanzania watakapo irejesha Tanzania kwenye mfumo wa Chama kimoja CCM, iwe ni Watanzania wenyewe ndio wameamua kupitia uchaguzi huru na wa haki ulioendeshwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi ulioendeshwa kwenye uwanja sawa na tambarare, na sio CCM ishinde katika ule ushindani wa kugombea kisu cha makali kuwili, huku mshindani mmoja ameshika kwenye mpini. Hivyo CCM ishinde kihalali kwa Miami wa kazi nzuri ya rais JPM na sio kwa sababu ndio iliyokamata mpini.
Tena kwa maoni yangu uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaosimamiwa na TAMISEMI ndio uwe wa mwisho, tubadili sheria zetu za uchaguzi, uchaguzi zote zisimamiwe na sheria moja, chini ya Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, zuio la mikutano ya siasa liondolewe, wagombea huru waruhusiwe ili hata watu kama akina sisi tusio wanachama wa chama chochote, tuweze kushiriki kugombea, hivyo uchaguzi wa 2025 tuchague viongozi wa serikali za mtaa, madiwani, wabunge na rais kwa siku moja. Hoja kuwa zitakuwa kura nyingi haina mashiko. Kwenye uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kila mpiga kura anapiga kura 5 kuchagua
- Diwani,
- Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
- Mbunge wa Bunge la JMT
- Rais wa Zanzibar
- Rais wa JMT
Hivyo Tanzania tukiamua kufanya uchaguzi huru na wa haki, unaofusta mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia ya ukweli, tunaweza. Mimi naamini kabisa kwa mambo makubwa na mazuri ya Rais Magufuli anayoyafanya, We have nothing to loose rais Magufuli akiruhusu demokrasia ikashamiri, akatoa haki sawa kwa vyama vyote kufanya siasa ikiwemo kuondoa zuio la mikutano ya siasa, bado rais Magufuli anaweza kuyaleta maendeleo yote aliyokusudia at the same time huku akiruhusu demokrasia nayo ishamiri, ila ukweli utaendelea kubaki ni ukweli daima kwa katiba hii na kasi hili ya rais Magufuli, CCM bado itaendelea kutawala Tanzania milele.
Naomba nimalizie kwa ile kauli ya thread hii
"Ushindi Mtamu ni Ushindi Unaopatikana kwa Ushindani Wa Haki Kwenye Uchaguzi Huru na Wa Haki, Unaendeshwa na Tume Huru na Shirikishi, na Unaofanyika Kwenye Uwanja Sawa wa Ushindani wa Kisiasa, Sio Ushindi wa Mezani!. Mheshimiwa Rais, Dr. John Pombe Magufuli, aka.JPM, Kasi Yako ya Maendeleo ya Tanzania Unaoifanya, Utailetea CCM Ushindi Kishindo Katika Uchaguzi Wowote, Tunakuomba Please Please Please, Ruhusu Tuu Ushindani wa Haki, Wazi na Usawa Kwa Vyama Vyote,
Utabarikiwa Zaidi na Zaidi, na Tanzania Tutabarikiwa.
Nawatakia Jumapili Njema
Na mimi nawahi kanisani
Misa ya Kwanza pale kanisa langu la St.Peters
Paskali