Ahaz1863
Member
- Apr 4, 2012
- 8
- 0
Utangulizi
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na changamoto ya ushiriki wa wananchi katika kufuatilia na kuwajibisha viongozi wa serikali katika jamii zao. Hii imepelekea ufujaji wa radimali za umma katika sekta ya kilomo na kudhohofisha usalama wa chakula.
Wananchi ni nguzo muhimu sana katika maeeleo ya taifa hasa kama itashiriki na kushirikishwa kilamilifu katika maeneo yafuatayo:
1. Kupanga na kuibua vipaumbele katika sekta ya kilimo.
2. Kusimamia mipango waliyopanga inayohusu kilimo.
Kwa mustakabali huo wananchi kama watashiriki kikamilifu itaongeza umiliki wa miradi iliyoibuliwa katika jamii zao kwakuona inawahusu kwa maendeleo yao. Lakini kutokana na ushiriki hafifu wa wananchi miradi mingi ya kilimo imekuwa ikipelekwa kwenye vijiji husika na wananchi kuiacha bila kuisimamia na kupelekea hasara kubwa kwani moradi hii huwa haidumu kwa muda mrefu.
Mfano miradi ya mikopo ya matrekta na vifaa vya kilimo imekuwa ikiishia kuwa hasara kwakuwa hakuna anayeona kama mrafi ni kwa manufaa ya jamii nzima aidha kwasababu hawakushirikishwa wakati wa uletaji mradi au uibuliwaji wake.
Nini kifanyike ili kuboresha ushiriki na ushirikishwaji.
1. Viongozi wa serikali katika ngazi zote wanapaswa kuhakikisha wanawashirikisha wananchi wakati wa ipangaji bajeti na uibuliwaji wa mipango katika marneo yao.
2. Wananchi wanapaswa kuhakikisha wanashiriki kila mikutano ya mitaa, vijiji na vitongoji ili kujua mipango inayoendelea katika maeneo yao.
3. Wananchi kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa uwajibikaji wa viongozi ili kubaini ujujaji wa radilimali hasa katika sekta ya kilimo.
4. Wananchi kutoa taarifa katika vyombo husika hasa wanapobaini uharibufu wa mali, uvujaji wa rasilimali na mayumizi mabovu ya rasilimali za umma.
5. Wananchi kuhakikisha mipango inatekelezwa kwa mujibu wa mpqngo uliopo, mfano kama bei elekezi ya mbolea ya CAN ni 60,000 kwa mfuko wahakikishe inauzwa kwa bei hiyo katika maduka ya pembejeo.
Kwa kufanya mambo yaliyoainishwa hapo juu kilimo kitaboreshwa kwa kiasi kikubwa kupelekea faida zifuatazo.
1. Sekta ya kilimo kuongeza uzalishaji na kuhakikisha usalama wa chakula nchini.
2. Kukuza kiwango cha uwajibikaji wa viongozi wa umma na wananchi kwa ujumla kwa kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa kufuta mpango ulippangwa.
3. Kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa wote wanaokuwa wamebainika kutumia rasilimali za umma kinyume cha mpango uliowekwa.
4. Kukuza uwazi hasa katika utekelezaji wa miradi ya kilimo katika jamii

Upvote
0