Tarehe 17 Juni ni Siku ya 29 ya Kupambana naKuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani. Watuwanasema kwamba China ina karata za turufutatu za kujitangaza, ya kwanza ni reli ya mwendokasi, ya pili ni ya usafiri wa anga za juu, na yatatu ni udhibiti wa majangwa. Ikiwa mojawapoya nchi ambazo zimeathiriwa sana na kueneakwa jangwa, China imeanzisha njia ya kuzuia nakudhibiti kuenea kwa jangwa ambayoinazingatia sheria za mazingira ya asili na hali yanchi, na imefanikiwa kuzuia kuenea kwa jangwana kupunguza maeneo ya jangwa kwa pamoja. Tangu mwanzoni mwa karne hii, karibu robo yamaeneo mapya yanayopandwa miti yapo China, na kiwango cha mchango wake kwa maeneomapya ya kijani kinashika nafasi ya kwanza duniani.
Hivi karibuni, Rais Xi Jinping wa China alitembelea Bayannaoer katika Mkoaunaojiendesha wa Mongolia ya Ndani. Kuzuiakuenea kwa jangwa na ujenzi wa mradi wakiikolojia wa misitu ya ulinzi wa "KaskaziniTatu" kulikuwa kazi muhimu katika ziara yake. Mradi wa "Kaskazini Tatu” unamaanisha "mradimkubwa zaidi wa upandaji miti duniani"uliojengwa katika maeneo ya kaskazini-magharibi, kaskazini, na kaskazini-masharikimwa China, kuanzia Xinjiang upande wamagharibi na kuishia Heilongjiang upande wamashariki. Baada ya zaidi ya miaka 40 ya juhudizisizolegalega, ukanda huo wa zamani wa"dhoruba ya mchanga" sasa umekuwa "UkutaMkuu wa Kijani" unaoenea maelfu ya maili.
Pia kuna "Ukuta Mkuu wa Kijani" barani Afrika.Afrika ni eneo linaloathiriwa na jangwa zaididuniani, huku asilimia 45 ya ardhi zikiwa katikahali ya ukame. Ukihamasishwa na mradi wakiikolojia wa "Kaskazini Tatu", Umoja waAfrika ulizindua mpango wa "Ukuta Mkuu waKijani wa Afrika" mwaka 2007. Hapo awali, lengo lake lilikuwa ni kujenga ukanda wa msituwa ulinzi wenye urefu wa kilomita 8,000 kwenye ukingo wa kusini wa Jangwa la Sahara na kurejesha hekta milioni 100 za ardhi zenyejangwa. Kufuatia Lengo la Maendeleo Endelevula Umoja wa Mataifa, Ukuta huu Mkuu waKijani unabeba majukumu zaidi, na wigo wake umeendelea kupanuka, ukichukua karibu maeneoyote kame na nusu kame ya Afrika, na nchizinazohusika pia zimeongezeka kutoka 11 zaawali hadi 20 hadi sasa. Hivi leo, Ukuta Mkuuwa Kijani wa Afrika umekuwa hatua muhimukwa Afrika kutekeleza malengo ya maendeleoendelevu ya Umoja wa Mataifa, kuchukuliwakama ulinzi wa kijani kwa maendeleo endelevuya kijamii na kiuchumi ya Afrika.
Ikiwa ni moja ya nchi za kwanza kujiunga naMkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambanana Kuenea kwa Jangwa, China imekuwaikihimiza kikamilifu utekelezaji wa Mkataba huokatika miongo kadhaa iliyopita, na imeshirikianana Mauritania, Ethiopia, Nigeria na nchinyingine za Afrika kubadilishana nazo uzoefuwa kiteknolojia wa China wa kuzuia na kudhibitikuenea kwa jangwa, ili kuchangia mpangomkubwa wa Ukuta Mkuu wa Kijani wa Afrika, na kuinua uwezo wa nchi za Afrika katikakuzuia na kudhibiti hali ya jangwa.
Mwaka 2021, Rais Xi Jinping alipendekezaMpango wa Maendeleo Duniani wakatialipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa. Usalama wa chakula, mabadiliko ya hali yahewa na maendeleo ya kijani ni maeneo muhimuya ushirikiano wa Mpango huo, na kupunguzaukame, kutambua usimamizi endelevu wa ardhi, na kujenga Afrika ya kijani ni maana zakezinazofaa. Afrika haipaswi kukosekana kwenyeramani ya maendeleo endelevu duniani.
Kuanzia mradi wa "Kaskazini Tatu” hadimpango wa "Ukuta Mkuu wa Kijani wa Afrika", ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuzuiana kudhibiti kuenea kwa jangwa ni jambo kubwatukufu ambalo linatekelezwa na vizazi vya sasana kunufaisha vizazi vijavyo. Katika miaka yahivi karibuni, mabadiliko ya hali ya hewa yasiyoya kawaida yamesababisha kuongezeka kwavumbi na hali ya hewa kavu kote duniani. Kwa hivyo, hatupaswi tu kulinda matunda ya kuzuiana kudhibiti kuenea kwa jangwa, lakini pia kutafuta maendeleo ya hali ya juu kwa moyo wa"kusukuma juu mawe kwenye mlima". Katikaenzi mpya, inaaminika kuwa China na Afrikakwa pamoja zinaweza kuunda muujiza mpya wakuzuia na kudhibiti kuenea kwa jangwa, kutoamchango chanya katika kufikia lengo la Umojawa Mataifa la kutokuwa na ardhi nyingineinayofifiwa kuwa jangwa ifikapo 2030 nakupunguza 50% ya ardhi zinazobadilika kuwajangwa duniani mwaka 2040, na kuonyesha kiinicha Mpango ya Maendeleo Duniani.