Ushirikiano wa China na Afrika kuimarika kutokana na athari ya ushuru uliowekwa na Marekani

Ushirikiano wa China na Afrika kuimarika kutokana na athari ya ushuru uliowekwa na Marekani

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG111567400238.jpg


Ushuru uliowekwa na Marekani unaweza kuwa na athari mbaya kwa nchi zinazoibuka kiuchumi kama China nan chi za Afrika, lakini wakati huohuo, hatua hiyo ya Marekani itawezesha ushirikiano wa nguvu zaidi kati ya China na Afrika katika biashara na uwekezaji kwenye seta muhimu za uzalishaji, nishati safi na teknolojia ya kidijitali.



Lester Bouah, mkurugenzi mkuu wa Kuhamasisha Uwekezaji na mkuu wa Kituo cha Nishati katika Idara ya Biashara, Viwanda na Ushindani nchini Afrika Kusini anasema, ushuru uliowekwa na Marekani umekuwa na athari kubwa kwa Afrika Kusini, ambayo Marekani ni moja ya masoko yake makubwa ya magari, bidhaa za kilimo na madini, huku sekta ya magari ikitoa fursa kubwa ya ajira nchini Afrika Kusini.



Kwenye mkutano wa Uwekezaji uliofanyika katika Ubalozi wa Afrika Kusini nchini China hivi karibuni, Bw. Bouah alisema ushuru uliowekwa na Marekani hauna msaada kwa mtu yoyote, na hakuna kinachoweza kupatikana kutokana na nyongeza hiyo ya ushuru, na kwamba anatarajia Wamarekani wataamka na kutambua kuwa, kuna jambo ambalo haliko sawa, akisisitiza kuwa utandawazi kamwe hauwezi kuzuiliwa\.

Bouah anasema, licha ya biashara, Afrika Kusini inaweza kuwa mwanzilishi wa uwekezaji wa China kuingia katika kanda ya Afrika kusini mwa Sahara, na hii inatokana na mfumo wake wa kibenki, miundombinu na soko, na kueleza umuhimu wa nafasi inayoendelea kuongezeka ya Pendekezo la Ukanda mmoja, Njia Moja.



Pia ameeleza kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini katika magari ya nishati mpya pamoja na akili bandia, na kuongeza kuwa, hivi sasa anatumia teknolojia ya DeepSeek ili kuwezesha kazi zake kwa ufanisi.



Bouah pia amesisitiza umuhimu wa kuwa na mfumo wa biashara wenye msingi wa kanuni, na kuongeza kuwa, kukosekana kwa mfumo huo kuna athari mbaya kwa nchi zinazoendelea. Amezitaka nchi zinazoibuka kiuchumi kama zile za kundi la BRICS kufanya kazi pamoja ili kudumisha maingiliano yao ya kiuchumi na biashara ya kimataifa.



Ofisa mwandamizi wa uwekezaji katika Mfuko wa Maedeleo wa China na Afrika, na pia mwakilishi wa ofisi hiyo nchini Afrika Kusini, Yu Qing, ameeleza fursa ya manunuzi katika soko la Afrika ambayo itatoa nafasi zaidi kwa bidhaa za China, suluhisho la kidijitali na ujenzi wa miundombinu. Amesema, wakati minyororo ya ugavi duniani inapitia marekebisho ya kimfumo, viwanda vya China navyo vinabadili mipango yao, kufungua njia mpya kwa ushirikiano wa kiviwanda kati ya China na Afrika, hususan katika sekta zinazotumia zaidi nguvukazi kama vitambaa, vifaa vya kielektroniki, na vipuri vya magari.



Song Wei, profesa katika Shule ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia katika Chuo Kikuu cha Kigeni cha Beijing anasema, kwa ajili ya maendeleo ya baadaye ya Afrika, kuimarisha uratibu kati ya China na Afrika na kuboresha ushirikiano kati ya nchi za Dunia ya Kusini, hususan kupitia majukwaa kama mfumo wa BRICS, kutakuwa na umuhimu mkubwa sana.



Anasema uhusiano wa kunufaishana kati ya nchi za Dunia ya Kusini unawakilisha fursa muhimu sana kwa Afrika. Kwa upande mmoja, nchi za kundi la BRICS zinaweza kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kuimarisha uhusiano wao katika uwekezaji na biashara. Na kwa upande mwingine, sera za kivumbuzi kama vile kutuliza thamani ya sarafu ya nchi husika na hatua za kuwezesha biashara, vitaimarisha zaidi ushirikiano wa nchi hizo.
 
Back
Top Bottom