Ushirikiano wa China na Afrika waonyesha mfano bora wa kuendeleza ustawi wa pamoja

Ushirikiano wa China na Afrika waonyesha mfano bora wa kuendeleza ustawi wa pamoja

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Wakati mwaka mpya unapoanza, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ameanza ziara yake ya kwanza nje ya nchi kwa mwaka 2025 kwa kutembelea bara la Afrika, akiendeleza utamaduni wa diplomasia unaotimiza miaka 35.

Ziara hii inaonyesha ahadi ya kudumu ya kuimarisha ushirikiano na Afrika na kuboresha mshikamani kati ya mataifa ya Dunia ya Kusini. Pia ziara hiyo inatokana na msingi uliowekwa katika Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwaka jana, ambapo rais wa China Xi Jinping alipendekeza kuwa uhusiano wa pande mbili kati ya China nan chi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China kufikia ngazi ya uhusiano wa kimkakati.

Pia rais Xi alipendekeza kuwa uhusiano wa jumla wa China na Afrika ufikie ngazi ya jamii ya China na Afrika katika hali zote yenye hatma ya pamoja katika zama mpya.

Hatua hiyo inaashiria mafanikio makubwa ya uhusiano kati ya China na Afrika, ikionyesha nia thabiti ya China ya kuendelea kuinua ushirikiano wa China na Afrika kufikia ngazi mpya.

Chini ya kanuni ya kuaminiana, matokeo halisi, uhusiano mwema na nia nzuri, miradi ya ushirikiano kati ya China na Afrika imeoa mchango mkubwa katika maendeleo endelevu ya bara hilo.

Katika nusu ya muongo uliopita, kampuni za China zimezisaidia nchi za Afrika kujenga na kuboresha zaidi ya kilomita 10,000 za reli, karibu kilomita 100,000 za barabara kuu, madaraja 1,000, bandari 100 na kilomita 66,000 za nyaya za kusambaza umeme, ambavyo vyote vimetoa njia za kuliunganisha bara la Afrika.

Licha ya miundombinu, China pia inafanya kazi na Afrika kuchochea mageuzi ya kijani ya bara hilo kupitia uwekezaji katika umeme wa maji, nishati ya upepo na jua, na kukabiliana na changamoto kuu katika teknolojia ya kilimo na usalama wa chakula.

Katika muongo uliopita, China imejenga vituo 24 vya majaribio ya teknolojia ya kilimo barani Afrika na kueneza zidi ya teknolojia za ubora wa juu 300 za kilimo, hatua iliyosaidia kuongeza mavuno ya mazao kwa kiasi cha asilimia 30 mpaka 60, na kunufaisha zaidi ya wakulima milioni moja katika nchi za Afrika.

Kama nchi wanachama wa Dunia ya Kusini, China na Afrika zimeunganisha nguvu ili kuendeleza mapendekezo muhimu ya maendeleo, yakiendana na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) na Eneo la Biashara Huria la Afrika. Ushirikiano huu umetengeneza fursa kwa nchi za Dunia ya Kusini kuwa na maingiliano zaidi na mnyororo wa thamani wa dunia, kufungua njia za mageuzi ya kiviwanda, utoaji wa nafasi za ajira, na maendeleo ya miundombinu.

Ushirkiano kati ya China na Afrika umeenda mbali zaidi ya masuala ya kiuchumi, pande hizo mbili zimekuwa na mtazamo wa pamoja wa kuboresha mfumo ulio sawa na jumuishi wa uongozi wa dunia, mfumo ambao unaongeza sauti ya nchi za Dunia ya Kusini katika jukwaa la kimataifa. Lengo hili la pamoja limeonekana katika juhudi mbalimbali za pamoja zinazolenga kuimarisha uwakilishi na ushawishi wa nchi zinazoendelea katika taasisi muhimu za kimataifa.

China ilikuwa nchi ya kwanza kueleza wasiwasi uungaji mkono wake kwa uanachama wa Umoja wa Afrika katika Kundi la Nchi 20 (G20). Kwa kuiunga mkono Afrika kuingia kwenye kundi hilo, China sio tu inaongeza hadhi ya Afrika kimataifa, lakini pia inaimarisha sauti ya Dunia ya Kusini katika masuala muhimu kama mabadiliko ya tabianchi, afya ya dunia, kuondokana na umasikini na mageuzi ya kibiashara.

Katika dunia inayokabiliwa na nguvu za kisiasa na umwamba, umuhimu wa uhusiano kati ya China na Afrika umekuwa wazi zaidi, kwani unasimama kama mwanga wa usawa, maendeleo ya pamoja na ustawi wa pamoja.

Uhusiano huu si wa mabadilishano, bali unajumuisha lengo la utaratibu wa dunia ulio wa haki na usawa. Kwa pamoja, China na Afrika ziko katika nafasi nzuri ya kutetea usawa wa kimataifa, uhalisia wa uhusiano wa pande nyingi, na maslahi ya Dunia ya Kusini.
 
China hana urafiki wowote wa kweli na Africa. Ni chui mbaya aliyevaa ngozi ya kondoo.. Anahitaji malighafi za Africa na kutafuta makazi ya kudumu kwa wananchi wake pamoja na soko
Miaka 30 ijayo atajivua gamba na tutalia kilio cha kusaga meno
 
Back
Top Bottom