Ushuhuda: Biashara ya mchele ni ngumu mno!

Katanga Sokoni zipo za aina nyingi sana mkuu, sijajua ni karanga gani unazungumzia
 

Ni mtama upi unatoka???
 

Mkuu mimi naye naitaji kujaribu kuipeleka uko congo ila kwa jf ni platform nzuri imenikutajisha na ww apo naomba msaada wako niweze kufika
 
Mtaji wa laki saba pekee hautoshi kabisa kufanya biashara ya mchele, ni ndogo sana.

Ushauri wangu tu, pambana kwanza upate meza hapo Sokoni, uza chochote cha rejareja chenye mtaji mdogo (hata kama ni nyanya), kisha anza kuuza mchele kwa reja reja (hata kama utakopeshwa kwa mali kauli na wauzaji wakubwa) huku ukiongeza 'thamani' (wauzaji wazuri wa mchele watakuwa wamenielewa).

Lengo la kufanya hayo ni nini?
1. Kukuza mtaji wako.
2. Kujenga mtandao mpana wa kibiashara (wauzaji wakufahamu na wateja wakufahamu)
3. Kujenga uzoefu wa kibiashara.
 
Bro hizi manual kazi ni ngumu , cheza na mtandao upate hela boss ..!! Hzi ni ngumu mno , unatakiwa upoteze hela nyingi Sana ili ukae kwenye mstari , au upate mtu wa kukushika mkono , Dar es salaam vijana wengi wanapoteza mda Sana ,ni mji unaohtaji akili nyingi Sana kama huna proffessional ya maana lazima mji ukufurahshe
 
Biashara za bongo zinakuwa ngumu kwa sababu ya watu wakati(Madalali),hawa jamaa wamekuwa kikwazo kila sekta nashauri kuwe na govern body kwa hawa watu maisha yetu yataweza kuwa rahisi zaidi.
Dalali by universal Code anatakiwa kupata si zaid ya 20% ya mauzo kama kamisheni. Hawa wabongo ni resale agents maana wanauza na kutaka kufunga au kuclose deal na zaidi ya 80% profit hapo bado hajataka na cha juu.

Madalali ndio moja ya sababu kubwa sana ya hii inflation tunayopitia bongo.
 
Ukinunua mchele usiende kuuza sokoni, wale madalali nao wanataka wapige cha juu, shusha mzigo wako kisha ingia kitaa jwa wenye maduka ambao ndio wauzaji wa mwisho
Hawa mafala nao siku hizi wameanza tabia za kibinafsi wananunua kwa watu wanaowajua.
 
Wacha weeeeee.

Mekumith[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Haya ushapewa mchongo huo hapo changamkia fursa.
 
Halafu mchele mzuri kabisa huku Turiani, Morogoro (kwenye mashine) ni elfu moja mkuu so next time usihangaike mpaka Mbeya ambako ni mbali
 
Nadhani wamemshauri vizuri kulingana na mtaji wake wa laki saba kwamba anaweza kupata gunia 10 za mtama na pia ikatosha kwa usafiri mpaka sokoni. Mchele hizo hizo gunia 10 lazima awe na zaidi ya milioni moja.
 
Nilichojifunza pia biashara yoyote ile ni mtaji ukiwa na elimu husika ya biashara mtaji NI muhimu saana ni ngumu sana kuanza na laki 7 then uje ufikishe million 100 ni ngumu sana wakuu
Hilo nalo ndio tatizo lako la pili pia. Usijenge fikra za mtaji mkubwa wakati ndiyo unaanza. Mtaji wako wa kwanza ni wazo, umefanikiwa, wa pili ni uthubutu umefanikiwa wa tatu ni rasilimali watu umeamua kujikatisha tamaa. Hapo ndipo unapotakiwa kutengeneza network na ujasiri, hapo ndipo ubunifu wa kutafuta wateja wa kudumu, usitegemee kupata faida mara hiyo hiyo ya kwanza wakati bado hujajuana na wateja. Kuna muda inabidi uendelee ili mtaji ukue na ukishazoeana na wateja utakuwa unachukua mzigo kwa mali kauli tu baada ya kujengeka kwa imani, pili tumia resources ulizonazo kutengeneza soko, mfano unaingia kwenye magroup ya whatsapp ya mapambo, wapishi yaani yale yanayohusika na maharusi unajitangaza biashara ya mchele, ingia magroup ya kilimo na mifugo, whatsapp, fb, hata account yako instagram unajitangaza, ukishaanza kukomaa kibiashara unamtafuta graphic designer anakutengenezea posters.

Hata hili lalamiko lako uliloandika jf unaweza kwenda kwenye matangazo ya biashara ndogondogo jf ukilifanya kuwa fursa ya unauza biashara ya mchele na kufanya delivery kwa gharama za mteja.








 
Mosi hongera sana kwa kujaribu [emoji109][emoji122][emoji122][emoji122]

Pili, hakuna jambo lolote especially biashara isiyokuwa na changamoto. Hivyo chukulia changamoto kuwa ni sehem ya biashara.

Tatu, umeingia kwenye nafasi isiyoendana na mtaji wako.

Ushauri
Kwa mtaji ulionao, rudi katika step za mwanzo za biashara hio (kulima) ikiwa moyo wako bado unawaza mchele, japo wengi wanakushauri ukaze lkn ukweli mchungu, UTAPOTEZA hata huo mtaji ulionao ikiwa utaendelea kukomaa hapo.


Yaani wasikutie kabisa moyo ukaendelea kubaki hapo,
 
Mkuu usikate tamaa...umenikumbusha 2013 nilipofanya biashara ya kununua mahindi maporini na kwenda kuuza sokoni ...nliambulia tsh 1000 faida baada ya kutoa gharama zote..kwa hasira nkaenda kununua sayona ya jero nipoze machungu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…