Ushuhuda: Biashara ya mchele ni ngumu mno!

Mkuu mimi naye naitaji kujaribu kuipeleka uko congo ila kwa jf ni platform nzuri imenikutajisha na ww apo naomba msaada wako niweze kufika
sawa!kule biashara sio mbaya ila changamoto ni nyingi sana, hasa kwa mgeni, kuanzia usafiri toka kigoma, njoo pm
 
Halafu mchele mzuri kabisa huku Turiani, Morogoro (kwenye mashine) ni elfu moja mkuu so next time usihangaike mpaka Mbeya ambako ni mbali
Mkuu naweza pata hiyo connection? Kutoka Dar mpaka huko ni shingapi? Na je usafiri wa kuleta Dar unapatikana kwa urahisi?
 
Nimechukua ushauri wako japo kuna changamoto nyingi mpaka kupata meza, mtaji n.k nimeulizia na wenye meza wanataka kuanzia miezi 4+
 
Mkuu ningejua hizo harakati za mtandao nisingekua napambana huku I wish na Mimi nijue hizo issue za mtandao
 
Wakuu wapi nitapata mkopo wa laki 5 au 3 nitaweka vyeti bond
 
Nenda kwa mamantilie jaribu kuongea nao pengine wanaweza kununua kutoka kwako. Au jaribu kusikilizia wapi kuna shuhuli ya ubwabwa unaweza kuwapelekea wakaununua.



Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]

Yes hasa kariakoo wale wanapika kg nyingi per day na wapo wengi sana

Akitengeneza connection kule atafanya biashara
 
Sidhani kama bado kuna karanga za kutosha maana huu msimu hazikukubali
 
Mkuu usikate tamaa...umenikumbusha 2013 nilipofanya biashara ya kununua mahindi maporini na kwenda kuuza sokoni ...nliambulia tsh 1000 faida baada ya kutoa gharama zote..kwa hasira nkaenda kununua sayona ya jero nipoze machungu
Dah we jamaa wewe [emoji23]
 
Aisee..

Miaka ya mwisho ya tisini, nilijiingiza kwenye biashara ya mchele, unakusanya maeneo ya Kagongwa, wilaya ya Kahama, halafu unapeleka kuuza Rwanda, miaka hiyo Faranga 1 ni sawa na shillingi 2 za TZ,

Nlianza na tu Tani tuwili tu, sababu Rwanda wananunua vigunia vya sandarusi vya kilo 50, kwao ndio standard ya manunuzi
Hapo na tugunia 40, usafiri ni unamlipa dereva wa semi trela anavipanga nje juu ya kontena.

Nimefika Kigali maeneo ya Majerwa ambapo ndio magari yote yanasimama, naisubiria Semi ifike, nimekaa gesti siku mbili, na ugeni ule natumia tuu, burusheti na Primus kwa sana, kumbe nakula hela ya ziada na sijui lini nitauza mchele, baada ya mchele kufika, nikachukua sample kama kilo 5 nazungusha kwenye maduka, duuh noma kweli naonekana mgeni kabisa mpaka wajeshi wakanibabatiza mjini miaka hiyo, maana kumbe wananiangalia naingia duka hili natoka mara duka hili nikakalishwa chini, nikahojiwa na nikatoa passpoti na kujieleza huku na kibegi changu cha sample ndio wakaniamini na kuniachia.

Nikampata Mzee wa kinyarwanda anataka vigunia 25, nikamletea lakini bei hata sio hivyo nzuri, hapo nimeshachoka nikakubali, sasa mbinde kuifata hela kila siku, zaidi ya wiki nafuatilia hela, gharama ndio zinazidi, na nikamalizia vigunia vingine kwa Mama mwingine wa Kiganda, kwa hasara tu, nikasema sirudii tena ndio ikawa mwisho kufanya biashara hizi hazieleweki.......

Sijui kwa sasa biashara ikoje kupeleka mchele Rwanda...
 
Katika Maisha, suala la kukata tamaa ni dhambi kubwa Sana! Hata hivyo imelinganishwa na Mtu alisafiri hadi katikati ya msitu halafu akajichimbia shimo la kutosha na kujizika mzima mzima, haiko hivyo. Hakuna biashara/kazi nyepesi Duniani lazima upambane hadi tone la mwisho la damu. Utawaza kwenda kijijini kulima ukidhani kuwa kilimo ni jambo jepesi, LA hasha!! Unaweza ukalima vizuri tu halafu usipate chochote Je, utaenda wapi baada ya hapo? Nakushauri, Kwa kuwa ulishaanza hiyo biashara usiiache, hizo ni changamoto za AWALI tu, huko mbeleni utapata akili tu.
 
😂Si mchezo...hii biashara sijawahi kuifanya exactly ila nimetoka kuifuatilia juzi juzi tu, huko huko Mbeya.ndani ndani huko kunaitwa Kamsamba, ni biashara yenye mbinde kdg na ukifanya masihara unachezea za uso...namshukuru mkuu Insigne kwa kunipa connection na kwenda kunitoa tongo tongo pande hizo...nimejifunza vitu vingi nikiwa na ndugu yangu...

Tunajipanga tena mambo yakiwa mazuri tunategemea kurudi msimu wa mavuno ya mpunga ukianza...bro huo mtaji wako kwa hii biashara hutoboi, mimi nilipiga hesabu nikiwa na mtaji wa milioni 10 nikajikuta napata faida ya laki mbili (200,000/) hapo hujatoa gharama za usafiri na chakula, na malazi...Noma Sanaa ila inawezekana
 

Keep going usikate tamaa hakuna kitu kirahisi[emoji1376][emoji1376][emoji1376]tunakomaa mpaka kinaeleweka
Yani kuna mda huoni kitu mbele giza tu keep going
Kitu umekosa ni mentor kwenye biashara yako otherwise hio biashara sio ngumu ni biashara kama nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…