Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Toka saa nane umeinza sasa ni saa 11:30, mbona huendelei, muwe munaindika mkimaliza then mnaipostHii inaisha ndani ya siku hizi mkuu wala haimakizi wiki
ni wivu tu 😏Ndiyo maana mnaingia kwenye UE na course work za single digits a.k.a 0-9 out of 40 kwa sababu ya kuendekeza mambo ya kutiki na kutotiki😬😬 soma kijana
Na wewe ndiye wale wale tu😏 soma ndugu fainali uzeenini wivu tu 😏
Sawa Sawa .....Namalizia mkuu nimeamua kufanya hivyo ili isichoshe wasomaji
"hofu ni ugonjwa mbaya.."Na wewe ndiye wale wale tu😏 soma ndugu fainali uzeeni
Sawa endelea kuautomatikalisha mkuu usije jutia utakapokuaja kuwa na G.P.A ya Gentleman 😀Mkuu hayo mambo ni automatically mkuu ili kuwepo na morale
Nikiona neno "to be continued"napata shaka kwa storyHatimaye Ametiki(Based on true story)
Ilikua mwaka 2016 katika chuo cha elimu ya biashara(CBE) Tawi la Mbeya nilikuwa mwaka wangu wa pili nikichukua stashahada ya usimamizi wa biashara (diploma in Businesses administration). Nikiwa nimeketi kwa pembeni kipindi hicho ndo kuna wanafunzi wapya walio kua wanaripoti. Nilimuona binti mmoja ambaye alikuwa akitoka Eneo la utawala kufanya usajili lilikua ingizo jipya Chuo hapo, binti huyo yeye alikuwa mzuri mwenye kufanana na mabinti wa kimasai kulingana na mkao wake, tembelea pamoja na umbo na rangi yake.
Sikufuatilia sana nilimuona na kumfananisha na maasai.
Siku kadha kupita wakiwa wanaelekea siku za mwisho za Orientation binti huyo nilimuona amekaa peke yake sehemu nikaona si vyema kumuacha nikasigea karibu yake na kuanza mazungumzo japo kidogo.
Mimi: Mambo vipi sister
Yeye: Safi (Aliitikia salamu huku akiniangalia na kuonyesha nusu tabasamu nusu kuchukia kama nimevuruga mpango wake wa kukaa peke yake yaani sikumuekewa)
Mimi: samahani kwa kukuingilia je, itakuwa dhambi kwa mimi kukaa na wewe hapa?
Yeye: Hapana
Mimi: Samahani wewe ni mwenyeji wa Arusha eti
Yeye: Ndio mimi mwenyeji wa Arusha wilaya ya Karatu.
Nilimuuliza maswali hayo sababu akifanania na maasai. Nikaanza kwa kumuuliza Jina akagoma kunitajia, Nikaona hapa niende direct kuomba mawasiliano ikabidi nimfungukie unaweza nisaidia mawasiliano yako.
Yeye alikataa katukatu na kusema hawezi nipa Mawasiliano yake nilijitahidi kumdanganya akasema labda yeye achukue namba zangu nami bila hiyana nikamupatia.
Hapo tunapiga stori kidogo nikaachana nae nikawa nimemuacha amekaa. Siku zilipita ilikuwa nadra kumuona sababu lecture rooms tulitofautiana na wala hakuwahi nitafuta kwenye simu. Siku zikaenda kama mwezi mmoja yupo chuo nikaonana naye alikuwa amekaa alipenda kukaa peke yake mara nyingi nikamfata nikampasa salam akaitikia.
Nikauliza mbona kimya hata hukunitafuta akasema nitakutafuta muda bado haujafika. Basi nikamuuliza tena Jina akasema mda ukifika nitamfahamu alidai mda bado.
Tulipiga story kidogo akanyanyuka kuondoka nikamuuliza mbona unaondoka akasema anawahi kipindi nami nikamuacha.
Kama bahati CR wao alikuwa ni jamaa tulie fahamiana kwa mda mfupi sababu akitoka mkoa mmoja na mimi hivyo tulishare Kabila. Ilibidi nimtumie yeye kumfuata na kumueleza kua anisaidie kupata namba za binti fulani nikamuelekeza sifa za huyo binti ili ajaribu kupata mawasiliano yake, alisema atamtafta ili amfahamu. Baada ya siku kadhaa alisema amemuona sema hajapata kumfahamu Jina wala hajapata mawasiliano yake maana binti yupo serious sana.
Siku zikapita CR akasema amepata namba zake hivyo atanipatia.
Dahh kwakweli nilifurahi sana ilibidi nikomae na huyo CR ili nipate namba.
Siku moja nipo geto CR akanitumia namba 075XXXXXX4 Akaniambia Jina kanaitwa ka Adelina.
To be continued...
Mkuu Inatakiwa niweke interval flani ila ipo full mkuu.
Na overconfidence pia ni mbaya mkuu! Ndiyo nnachokiona kwako😉"hofu ni ugonjwa mbaya.."
Watanzania tusiogope ,tupo vizuri.💪😁
😂 😂 😂Hii story kama ni kweli basi dogo bado hujaiva yani mara mbili zote umebaki na kipa na umepaisha mpora kizeembe