Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kula chipsi achana na kachumbari weka tomato n chill basMimi niliwahi kula chipsi Mahali asee! Niliuguwa tumbo wiki nzima naendesha tu. Mpaka Leo chipsi naogopa kula za vibandani na migahawani kama sumu.
Nyanya asilimia 90 ni zile reject.
Ogopa sana nyanya zilizopangwa na vitunguu vya kupangwa lazima waweza mbovu pia....Niliona wanaziblend pale kariakoo sokoni [emoji119][emoji119]
Wachafu,vyombo waosha ktk maji machafu na misahani ya plastiki hovyo.Muhimu: Sio migahawa yote, Ni baadhi ya migahawa
kwa takriban miaka sita niliweza kula vyakula mtaani migahawani pindi niwapo kazini asubuhi na mchana na hapa naleta mrejesho kwa yaliyonipata.
Ni mara nyingi sana nimewahi kuharisha kwa kula vyakula vya migahawani , tumbo kuuma, n.k.
baada ya miaka sita niliona niwe narudi tu nyumbani nakula chakula cha nyumbani, kiukweli matatizo ya kuharisha, tumbo kuuma, yamebaki kuwa historia
Vyakula vinavyouzwa migahawani ili kutengenezea watu faida vinaweza kuwa hatari sana hasa ukizingatia hakunaga kitengo kinachokagua usalama wa vyakula.
Mfanyabiashara anachowaza ni faida, ni kama kwenye nguo unaweza ambiwa hii nguo ni original, unalipi ila ukifua mara 2 ama mara 3 shughuli imeisha hapo, basi ndivyo ilivyo kwenye biashara hata za vyakula, wapo wanaojali faida zaidi,
Hasa kwenye nyama hapa uwe makini mno! kuna namna ya kupata nyamma za bei rahisi ili kupata faida kubwa, usipokuwa makini hapa utazila sana.
Suala la faida linafanya hata chakula cha jana kama hakikuuzika basi kinachanganywa na cha kesho yake.
kuhusu kujali usafi wakati wa mapishi nako kuna wengine usafi ni sifuri kwakweli, hata sitaki kuyazungumza ila uchafu anaekula ni mteja na jiyo yote ni sababu anaekula ni mteja.