Hiki kitu nimeshuhudia kuna mtoto wa ndugu yangu anasoma shule flani ya msingi darasa la nne, ni shule ya mtaala wa kiingereza ila walimu ni wa hapa kwetu, huwa anafaulu vizuri tu lakini kuna maswali aliniletea nimsaidie ya social studies (maarifa ya jamii) sasa nikawa namweleza swali linamaanisha nini kwa kiswahili ili nione kama kaelewa ndio nimsaidie lakini alikuwa anapata wakati mgumu, ajabu ni kwamba nikimuliza maswali ya homework zake za zamani majibu ananipa vizuri ila nikumuuliza maana ya maswali niliyomuuliza inakuwa taabu kidogo.
Pia katika maswali nimeona kwa level ambayo yupo walimu wao wa hapa kwetu wana complicate sana mambo kwenye lugha hasa kwa kutumia misamiati migumu kidogo kwa mtoto wa darasa la tatu.
Kwa upande wa mtoto wangu, nae yupo darasa la nne shule yao ni ya mtaala wa kiingereza ila walimu wengi wametokea Zambia, kiukweli kwenye lugha hata kunipa tafsiri huwa sio tabu na walimu wao sio kwamba hizi kugha wamejifunzia ukubwani bali ni lugha za nchi yao kwa hio kuna njia rahisi zaidi wanatumia ili watoto waelewe.
kuna siku kulikuwa na mhubiri anaeongea kiingerea ilibidi awe anatafsiriwa na , basi mtoto wangu alikuwa nae anatafsiria wenzake vizuri kabisa kiukweli nilikuwa nafarijika, mtu kama kiingereza kimepanda kutafsiri ni ishu ndogo tu.
Mapendekezo:
Ni bora zaidi kumpeleka mtoto kwenye shule ya kiingereza yenye walimu ambao asili ya nchi zao kiingereza ni mojawapo ya lugha za taifa tangu utotoni mtu anaitumia. kama ni kumpeleka mtoto shule ambazo walimu ni wenye asili ya hapa kwetu ambako wengi huanza kujifunza kiingereza sekondari basi tuwe tunajihakikishia lugha wanaielewa vizuri.
Huu ujinga wa ki ngereza mtauacha lini?
Hao wazambia mbona ni hohehahe tu kama watanzania, wamalawi ndio usiseme yani ni choka tu.
Africa imejaa bogus peoples ila sio wewe mkuu.
Nilifikiri utaniambia labda mtoto anajua ms office, ana speed ya kuchapa ya hatari, anajua kusurf na kujitafutia mambo yake, anajua some basic of graphics design, anaweza kutengeneza katoons, anajua kutumia google map vizuri, anajua kutumia webquest,podcast, simulation.
kufanya troubleshooting collapsed softwares ndogo ndogo.
Anaweza kutumia app za kujifunzia hisabati,chinese, english nk
Anaweza ku set na ku reset android/ios phone, computer nk anaweza ku download na ku upload vitu mtandaoni, anaweza kutofautisha blog,wesite,forum nk ,
Anatimbua basic electronics devices.
Anaweza ku analyse sifa za udongo na namna unavyoathiri mazao,
anaweza kupanga lishe bora, anaweza ku manage timetable yake ya kila siku na kujitofautisha na wa kayumba bila kusimamiwa ?
Mambo mengi mengi hao watoto hawajui zaidi ya hicho kingereza.
Jaribuni kuangalia humo mitandaoni watoto wa wenzetu wanaojitambua wanafanya nini, wanaweza nini sio utopolo huu mnao unadi kila kukicha.
Watoto wenu hao hawawezi chochote cha maana ktk ulimwengu wa teknolojia.
Kuna shule moja huwa naitembelea yani nabaki tu kujiuliza na kuwashangaa wazazi malimbukeni jinsi ambavyo wanawapotezea muda watoto wao. Ile shule ni gereza la kuongea kingereza hamna cha zaidi kinachomyofautisha na mtoto wa kayumba ikiwemo uchafu lakini shule inakuwa ya 5 kiwilaya.
Kumbuka hizo shule zinatumia mtaala uleule wa kayumba usioendana na zama za sayansi na teknolojia .