Ushuhuda kutoka kwa Shehe Omari Mnyeshani

Uchawi unafanyika sana tena mwingine ni wa nia za ovyo kiasi ya kwamba ukiambiwa utashangaa, lakini always kuna nguvu fulani ya asili huwa inaleta ukinzani. Na wachawi wanaelewa kwamba uchawi hauwezi kutawala dunia kwa asilimia 100
Mkuu, kuna uchawi wa nia njema? Mimi nijuavyo uchawi ni uovu, ni ubaya.
 
Nimeamua kuuandika kwa vile upo YouTube, lakini sikubaliani wala kupingana na msimuliaji.

Ni ushuhuda wa bwana mmoja anayejiita Shehe Omari Mnyeshani, Mchawi wa "zamani".

Anadai kuwa kabla ya kuukimbia uchawi, alikuwa Mwenyekiti wa wachawi Tanzania na nje ya Tanzania.

Ikiwa anayoyaongea yana ukweli, basi nchi yetu inahitaji "ukombozi" wa Kimungu. Lakini ikiwa tu ayasemayo ni ya kweli.

Anadai kuwa kabla ya kuachana na uchawi, kuna mwaka walifanya tambiko la Kitaifa la kuizindika nchi, tambiko ambalo lilifanyikia mkoani Lindi. Shughuli hiyo iliwahusisha wachawi wote wa Tanzania. Nafikiri ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 90, kama sijakosea.

Katika hilo tambiko, waliazimia mambo kadhaa, ikiwemo la Waziri Mkuu wa Tanzania kutokushika madaraka ya Urais.

Kwamba, haijalishi Waziri Mkuu atajitahidi kiasi gani, haitakaa itokee awe Raisi wa JMT. Akishaushika tu Uwaziri Mkuu, na Urais anakuwa ameshaukosa. Kama ndivyo, na ikiwa nguvu kubwa kuliko ya wachawi haitaingilia kati, Majaliwa hayakuwa Rais wa JMT. Vile vile, isingewezekana kwa John Malecella, David Msuya, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda kukushika Urais wa Tanzania. Wote hao walishashika nafasi za Uwaziri Mkuu.

Hilo tambiko lilikuwa na athari kwa mkoa wa Lindi, kwamba watu wake hawatakuwa na uwezo mzuri kiakili.
Ardhi ya Lindi ilitolewa kama kafara kufuatia hilo tambiko la kichawi kufanyikia huko.

Inasemekana kuna kipindi Serikali iliweka jitihada ya kuwasisitiza watu wa huko kutumia chumvi ya viwandani ili kuwaongezea uwezo wa kufikiri, kwa kudhaniwa kuwa ni ukosefu wa madini muhimu ndiyo uliokuwa ukiwapelekea watoto wa huko kuwa chini kimasomo. Lakini kwa mujibu wa huyo mchawi wa zamani, ni kwa sababu Lindi ilitolewa kama Kafara wakati wa hilo tambiko.

Wachawi wa Lindi walijulishwa kabla ya hilo tambiko kuwa hayo madhara yatawatokea wana Lindi, na wakataka likafanyikie Tanga au Tabora lakini wachawi wa hiyo mikoa wakajitetea kuwa nao walishatoa michango yao siku za nyuma. Wachawi wa Lindi japo hawakutaka mkoa wao uwe duni, walishindwa kulikwepa hilo la tambiko kufanyikia kwao.

Jambo lingine aliloliongelea ni uchaguzi wa 1995. Anadai kuwa katika rada yao ya kichawi, waligundua kuwa mtu aliyekuwa amekusudiwa na Mungu awe Rais wa Tanzania kipindi hicho ni Jackson Makweta. Lakini walipobaini kuwa Makweta anaweza akawa kero kwao, waliamua kupambana naye kwa kumwondolea wazo la Urais, na wakafanikiwa.

Aliyeyasema hayo ni Shehhe Omari Mnyeshani!

Japo sijakubali wala kukataa, nina maswali kadhaa kuhusu hayo madai yake.

1. Ni kweli kuwa watu wa Lindi wana uwezo mdogo kiakili? Mbona Mama Salam Kikwete na marehemu Bernard Membe ni watu wa Lindi lakini wako vizuri upstairs?

2. Unafikiri kwa hoja yake kuwa katika tambiko la mwisho la kuisindika Tanzania kichawi walikubaliana kuwa mtu aliyeshika nafasi ya Uwaziri Mkuu asifanikiwe kuwa Rais wa JMT, inaweza kuwa na mashiko?

3. Kwa mujibu wa simulizi yake, Makweta ndiye aliyekusudiwa na Mungu awe Rais wa JMT 1995. Unafikiri Makweta angefanya vizuri kumzidi Mkapa?

4. Japo masimulizi yake hayawezi kuthibitishwa Kisayansi, unafikiri nguvu za giza zina nafasi kwenye utawala wa Tanzania?

Hapo chini ni moja ya shuhuda zake

Part 14 inaelezea chimbuko la mbio za mwenge Tanzania, na part 15 inahusiana na zindiko la Lindi
Wanaweza fanya tambiko la kuzuia ufisadi serikalini? Na kuongeza uwajibikaji?

Au kwenye kuleta maendeleo uchawi hauwezi?
 
Part 14 inaelezea chimbuko la mbio za mwenge Tanzania na part 15 inaelezea tambiko likilofanyika Lindi mwaka 1990
 
Attachments

  • PART14_MWENYEKITI_WA_WACHAWI_TZ__SHEKHE_ALIEOKOKA_NILIUA_MKE_NA_KUISHI_NAE_TENA_UCHAWI__NIMESO...mp4
    42.9 MB
  • PART15_MWENYEKITI_WA_WACHAWI_TZ__SHEKHE_ALIEOKOKA_NILIUA_MKE_NA_KUISHI_NAE_TENA_UCHAWI__NIMESO...mp4
    43.5 MB
1. Umewasingizia hao watu. Hao ni Lindi kweli kweli. Mama kwete unaona yupo vizuri. Are you serious? Are you normal?
Mama Kikwete yupo vizuri mkuu. Vinginevyo, asingeolewa na Mzee Kikwete.

Isitoshe, hilo tambiko lilifanyika mwaka 1990 hivyo halikumwathiri yeye. Waliaoathirika ni wale waliozaliwa baada ya hilo tambiko.
 
Hizi story utazisikia sana kwenye vijiwe vya walokole!
Hapo wanapumbazwa watu ili wauziwe mafuta, na maji!
Shenzy typ!@#$%@#$
 
Mkuu, kuna uchawi wa nia njema? Mimi nijuavyo uchawi ni uovu, ni ubaya.
Katika falsafa ya uchawi hakuna nia njema wala mbaya duniani, kila nia ni ina makusudi na manufaa kwa mwenye nia. Ndomana wachawi hawamwamini mtu hata wao hawaaminiani
 
Nimeamua kuuandika kwa vile upo YouTube, lakini sikubaliani wala kupingana na msimuliaji.

Ni ushuhuda wa bwana mmoja anayejiita Shehe Omari Mnyeshani, Mchawi wa "zamani".

Anadai kuwa kabla ya kuukimbia uchawi, alikuwa Mwenyekiti wa wachawi Tanzania na nje ya Tanzania.

Ikiwa anayoyaongea yana ukweli, basi nchi yetu inahitaji "ukombozi" wa Kimungu. Lakini ikiwa tu ayasemayo ni ya kweli.

Anadai kuwa kabla ya kuachana na uchawi, kuna mwaka walifanya tambiko la Kitaifa la kuizindika nchi, tambiko ambalo lilifanyikia mkoani Lindi. Shughuli hiyo iliwahusisha wachawi wote wa Tanzania. Nafikiri ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 90, kama sijakosea.

Katika hilo tambiko, waliazimia mambo kadhaa, ikiwemo la Waziri Mkuu wa Tanzania kutokushika madaraka ya Urais.

Kwamba, haijalishi Waziri Mkuu atajitahidi kiasi gani, haitakaa itokee awe Raisi wa JMT. Akishaushika tu Uwaziri Mkuu, na Urais anakuwa ameshaukosa. Kama ndivyo, na ikiwa nguvu kubwa kuliko ya wachawi haitaingilia kati, Majaliwa hayakuwa Rais wa JMT. Vile vile, isingewezekana kwa John Malecella, David Msuya, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda kukushika Urais wa Tanzania. Wote hao walishashika nafasi za Uwaziri Mkuu.

Hilo tambiko lilikuwa na athari kwa mkoa wa Lindi, kwamba watu wake hawatakuwa na uwezo mzuri kiakili.
Ardhi ya Lindi ilitolewa kama kafara kufuatia hilo tambiko la kichawi kufanyikia huko.

Inasemekana kuna kipindi Serikali iliweka jitihada ya kuwasisitiza watu wa huko kutumia chumvi ya viwandani ili kuwaongezea uwezo wa kufikiri, kwa kudhaniwa kuwa ni ukosefu wa madini muhimu ndiyo uliokuwa ukiwapelekea watoto wa huko kuwa chini kimasomo. Lakini kwa mujibu wa huyo mchawi wa zamani, ni kwa sababu Lindi ilitolewa kama Kafara wakati wa hilo tambiko.

Wachawi wa Lindi walijulishwa kabla ya hilo tambiko kuwa hayo madhara yatawatokea wana Lindi, na wakataka likafanyikie Tanga au Tabora lakini wachawi wa hiyo mikoa wakajitetea kuwa nao walishatoa michango yao siku za nyuma. Wachawi wa Lindi japo hawakutaka mkoa wao uwe duni, walishindwa kulikwepa hilo la tambiko kufanyikia kwao.

Jambo lingine aliloliongelea ni uchaguzi wa 1995. Anadai kuwa katika rada yao ya kichawi, waligundua kuwa mtu aliyekuwa amekusudiwa na Mungu awe Rais wa Tanzania kipindi hicho ni Jackson Makweta. Lakini walipobaini kuwa Makweta anaweza akawa kero kwao, waliamua kupambana naye kwa kumwondolea wazo la Urais, na wakafanikiwa.

Aliyeyasema hayo ni Shehhe Omari Mnyeshani!

Japo sijakubali wala kukataa, nina maswali kadhaa kuhusu hayo madai yake.

1. Ni kweli kuwa watu wa Lindi wana uwezo mdogo kiakili? Mbona Mama Salam Kikwete na marehemu Bernard Membe ni watu wa Lindi lakini wako vizuri upstairs?

2. Unafikiri kwa hoja yake kuwa katika tambiko la mwisho la kuisindika Tanzania kichawi walikubaliana kuwa mtu aliyeshika nafasi ya Uwaziri Mkuu asifanikiwe kuwa Rais wa JMT, inaweza kuwa na mashiko?

3. Kwa mujibu wa simulizi yake, Makweta ndiye aliyekusudiwa na Mungu awe Rais wa JMT 1995. Unafikiri Makweta angefanya vizuri kumzidi Mkapa?

4. Japo masimulizi yake hayawezi kuthibitishwa Kisayansi, unafikiri nguvu za giza zina nafasi kwenye utawala wa Tanzania?

Hapo chini ni moja ya shuhuda zake

Part 14 inaelezea chimbuko la mbio za mwenge Tanzania, na part 15 inahusiana na zindiko la Lindi
Anasema vitu ambavyo tayari vipo hasa hilo la waziri mkuu. Hakuna cha ziada alichosema;
 
Hii nchi kuwa na maendeleo ni hadi livunjwe kafara la umasikini.
Umasikini ni kafara la uhuru.
Ili tupate mkoloni aondoke ni lazma tuwe masikini
 
Back
Top Bottom