Ushuhuda kutoka kwa Shehe Omari Mnyeshani

Ushuhuda kutoka kwa Shehe Omari Mnyeshani

Bado simulizi la Kafara lililofanyika Lindi.
Hilo lilikuwa kubwa kupita lile la Bagamoyo.

Ni simulizi la kutisha sana.
Nitaliweka hapa muda sio Mrefu.

Tukae mkao wa kula.

Safari ya Lindi ilianza huku msoma Dua akiwa anatembea kwa kushikiliwa na wakati mwingine kubebwa mzegamzega.

Ni kwamba anatembea huku anasoma Dua ya Shetani. Anatembea na Kuzimia njia Mzima na kubebwa.

Itaendelea.
 
Wakati zindiko la Bagamoyo lilifanywa na Wachawi Vigogo Saba tu. Yaani (7)

Zindiko la Lindi lilijumuisha Wachawi Nguli mia moja(100) wa kutoka karibu kila mkoa.
Na wasaidizi (40)

Safari ya kuelekea Lini ilifanyika Kichawi. Yaani kwa msaada wa Majini.

Nini kilifanyika huko Lindi.
Itaendelea

Je Mshana.Jr, alikuwepo? Itaendelea.,
 
Nimeamua kuuandika kwa vile upo YouTube, lakini sikubaliani wala kupingana na msimuliaji.

Ni ushuhuda wa bwana mmoja anayejiita Shehe Omari Mnyeshani, Mchawi wa "zamani".

Anadai kuwa kabla ya kuukimbia uchawi, alikuwa Mwenyekiti wa wachawi Tanzania na nje ya Tanzania.

Ikiwa anayoyaongea yana ukweli, basi nchi yetu inahitaji "ukombozi" wa Kimungu. Lakini ikiwa tu ayasemayo ni ya kweli.

Anadai kuwa kabla ya kuachana na uchawi, kuna mwaka walifanya tambiko la Kitaifa la kuizindika nchi, tambiko ambalo lilifanyikia mkoani Lindi. Shughuli hiyo iliwahusisha wachawi wote wa Tanzania. Nafikiri ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 90, kama sijakosea.

Katika hilo tambiko, waliazimia mambo kadhaa, ikiwemo la Waziri Mkuu wa Tanzania kutokushika madaraka ya Urais.

Kwamba, haijalishi Waziri Mkuu atajitahidi kiasi gani, haitakaa itokee awe Raisi wa JMT. Akishaushika tu Uwaziri Mkuu, na Urais anakuwa ameshaukosa. Kama ndivyo, na ikiwa nguvu kubwa kuliko ya wachawi haitaingilia kati, Majaliwa hayakuwa Rais wa JMT. Vile vile, isingewezekana kwa John Malecella, David Msuya, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda kukushika Urais wa Tanzania. Wote hao walishashika nafasi za Uwaziri Mkuu.

Hilo tambiko lilikuwa na athari kwa mkoa wa Lindi, kwamba watu wake hawatakuwa na uwezo mzuri kiakili.
Ardhi ya Lindi ilitolewa kama kafara kufuatia hilo tambiko la kichawi kufanyikia huko.

Inasemekana kuna kipindi Serikali iliweka jitihada ya kuwasisitiza watu wa huko kutumia chumvi ya viwandani ili kuwaongezea uwezo wa kufikiri, kwa kudhaniwa kuwa ni ukosefu wa madini muhimu ndiyo uliokuwa ukiwapelekea watoto wa huko kuwa chini kimasomo. Lakini kwa mujibu wa huyo mchawi wa zamani, ni kwa sababu Lindi ilitolewa kama Kafara wakati wa hilo tambiko.

Wachawi wa Lindi walijulishwa kabla ya hilo tambiko kuwa hayo madhara yatawatokea wana Lindi, na wakataka likafanyikie Tanga au Tabora lakini wachawi wa hiyo mikoa wakajitetea kuwa nao walishatoa michango yao siku za nyuma. Wachawi wa Lindi japo hawakutaka mkoa wao uwe duni, walishindwa kulikwepa hilo la tambiko kufanyikia kwao.

Jambo lingine aliloliongelea ni uchaguzi wa 1995. Anadai kuwa katika rada yao ya kichawi, waligundua kuwa mtu aliyekuwa amekusudiwa na Mungu awe Rais wa Tanzania kipindi hicho ni Jackson Makweta. Lakini walipobaini kuwa Makweta anaweza akawa kero kwao, waliamua kupambana naye kwa kumwondolea wazo la Urais, na wakafanikiwa.

Aliyeyasema hayo ni Shehhe Omari Mnyeshani!

Japo sijakubali wala kukataa, nina maswali kadhaa kuhusu hayo madai yake.

1. Ni kweli kuwa watu wa Lindi wana uwezo mdogo kiakili? Mbona Mama Salam Kikwete na marehemu Bernard Membe ni watu wa Lindi lakini wako vizuri upstairs?

2. Unafikiri kwa hoja yake kuwa katika tambiko la mwisho la kuisindika Tanzania kichawi walikubaliana kuwa mtu aliyeshika nafasi ya Uwaziri Mkuu asifanikiwe kuwa Rais wa JMT, inaweza kuwa na mashiko?

3. Kwa mujibu wa simulizi yake, Makweta ndiye aliyekusudiwa na Mungu awe Rais wa JMT 1995. Unafikiri Makweta angefanya vizuri kumzidi Mkapa?

4. Japo masimulizi yake hayawezi kuthibitishwa Kisayansi, unafikiri nguvu za giza zina nafasi kwenye utawala wa Tanzania?

Hapo chini ni moja ya shuhuda zake

Part 14 inaelezea chimbuko la mbio za mwenge Tanzania, na part 15 inahusiana na zindiko la Lindi

Part 16 ni mwendelezo wa masimulizi ya tambiko la Lindi
Watanzania tuungane kumlilia Mungu atuokoe na watoto wetu.

Shetani ameshika usukani
 
Mmoja alidhamiria kufunga goli dakika ya 89:59, wpmwingine aliingia bungeni akatoa hoja earphone zipigwe marufuku kwakuwa zinasababisha uziwi kwa watumiaji
Mama Salma Kikwete hawajawahi kuwa nazo kwa kumakinika ingawa alikjwa mwalimu shule ya msingi
 
Hawa wanaojiita wachawi hakuna cha uchawi wala nini, hao ni wajanja fulani tu wa kuunganisha dot na kucheza vizuri na historia.

Kwenye hili la waziri mkuu kutokuwa raisi, Ukiangalia historia ya Tanganyika baada ya uhuru ni kweli hakuna waziri mkuu aliyewahi kuwa raisi.
Sasa kwenye uhalisia huo unaweza kutengeneza hadithi lukuki za kimtizamo (dini, uchawi, laana n,k) na watu wakaamini.

Kwa hiyo huyu naye ni wale wale wa kurubuni watu kwa story za kutunga kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Mkuu
Najua unajua kwa nini umeweka huu utetezi wako makini hapa.

Babeli inaenda kuanguka. Mtatumia njia saba kutawanyika
 
Inaelekea huu upole wa WaTz ni kazi ya nguvu za giza! Yaani hadi chaguo la Mungu wamelishinda? Je huyo mtu ccm? Naona wanaifaidisha ccm tu na wezi wake.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Ni Kweli, si bure. Watanzania wanatumikishwa bila wao kujua. Wamepigwa upofu wa kifikra na kuwa kama "mazezeta" japo si mazezeta
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Bado simulizi la Kafara lililofanyika Lindi.
Hilo lilikuwa kubwa kupita lile la Bagamoyo.

Ni simulizi la kutisha sana.
Nitaliweka hapa muda sio Mrefu.

Tukae mkao wa kula.

Safari ya Lindi ilianza huku msoma Dua akiwa anatembea kwa kushikiliwa na wakati mwingine kubebwa mzegamzega.

Ni kwamba anatembea huku anasoma Dua ya Shetani. Anatembea na Kuzimia njia Mzima na kubebwa.

Itaendelea.
Ukishaliweka unishtue, tafadhali🙏
 
Ooh pwani wavivu hawataki kulima ardhi tele ina rutuba nenda kalime wewe Tena unapewa shamba Bure Kisha ulete mrejesho.
Pana kikundi walitumia milioni hamsini heka mia kulima uvuta wakavuna debe tatu.
Bora hao hata walivuna debe 3, kuna waliosahau kama hata walinunua mashamba huko
 
Maeneo yote waliyofanya matambiko nchini hayana maendeleo.
Bagamoyo, Lindi, Tanga, Tabora na Kigoma
Mbona Kilimanjaro walipandisha mwenge kileleni siku ya uhuru na maendeleo yapo au ndio nuru ya mwenge inaangazia wachaga wanaiona hela?

Arusha napo azimio na mnara wake uliopo kati kati ya bara la Afrika na bado watu wanatoboa kimaendeleo.

Au tuseme haya matukio mawili sio matambiko ila hayo matukio mengine ndio matambiko. Tukisema hivyo huoni kama tutakuwa tunajitetea tu juu ya uvivu wa watu wa hayo maeneo mengine?.

Haya mambo yapo ila umasikini ni matokeo ya uvivu tu.
 
Point! Tupe muongozo. Tunaanzaje?
Ikiwezekana kwa uchache wetu tukaazimia kuwa kila siku ya ijumaa, au jumamosi au jumapili au jumatatu tujiweke wakfu kutokula siku nzima na kuiombea nchi yetu. Ipo siku haya yatakoma
 
Ikiwezekana kwa uchache wetu tukaazimia kuwa kila siku ya ijumaa, au jumamosi au jumapili au jumatatu tujiweke wakfu kutokula siku nzima na kuiombea nchi yetu. Ipo siku haya yatakoma
Point. Lazima kuchukua hatua. Kutegemea mabadiliko bila kufanya chochote ni sawa na kutarajia kuvuna maembe kwenye mti wa mkuu.
 
Back
Top Bottom