Ushuhuda kutoka kwa wanandoa waliowahi kuachana, hasa mliokuwa na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya

Ushuhuda kutoka kwa wanandoa waliowahi kuachana, hasa mliokuwa na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya

Kuna jamaa yangu anatumia gari ya mke wake kama guest inaniuma sana
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
 
Kwa umri nilionao.... Nimekuja kugundua.... Ukijaribu kummiliki Mwamamume.... Utaumia sana kihisia, kimwili, kisaikolojia, kimatendo, kifikra.... Utaumia Kila Kona. Utakuwa mtu wa mawazo na kununa muda wote. Nimeacha kabisa hii TABIA.
Uko sahihi kabisa
 
Mimi nimerelax mda wote shida Ni nyie watu msiopenda different opinions za wengine.
Thanks for ur wishes.
Unaonekana Kama uko dunia yako tofauti! Shtuka something is wrong
 
Yaliyotokana na tukio yalipelekea tukio la ugomvi mkubwa mkubwa sana kama two weeks ago.. Ndio maana. Naogopa kueleza sana maana mashuhuda iam sure wengi ni jf members kutokana na neighbohood ugomvi uliotokea...wengine wanaweza kuja na hints hapa...mimi nimeamua kujitenga mbali na muhusika ili moyo upone..ila bado imekua ngumu kuna watoto
Hauhitaji msaada wa kweli wewe,hapo ni sawasawa unaenda kuonana na daktari anakuuliza historia ya tatizo unamficha,unadhani hapo unasaidiwaje
 
Mkuu suala la talaka ni la kisheria, huwezi kukwepa mchakato wake na kwa kweli ni jambo linalochukua muda na linaumiza hisia na hata uchumi, mleta mada anahitaji kupata ushauri wa kumuandaa kisaikolojia kama kweli amedhamiria kudai talaka
Mimi nilikuwa muhanga wa talaka nilipotengana na mzazi mwenzangu. Alikuwa na rafiki yake ambae ni hakimu wa kiteto. Akamuuliza namna tunaweza talikiana akasema mimi ninatakiwa kwenda mahakamani kifungua kesi ya madai ya talaka. Nilipoenda nikapewa maelekezo ya kufuata kufungua file na kulipia. Alafu nikapewa barua ya wito ya mwanaume nimpelekee alafu tukapewa tarehe ya kuja.

Siku ya kusikilizwa tulisikilizwa wote na hukumu ikatoka siku hiyo hiyo na mwenzangu alilipia hati ya talaka akapewa nakala yake.

Kinachofanya suala la talaka kuchukua muda mrefu ni mali. Hili la tulichuma wote tugawane ndio linafanya mchakato unakuwa mgumu na mrefu
 
Nashukuru ndugu kwa mchango wako...ila image ambayo nimepaint kwa ndugu zangu watashangaa sana..na wanamuamini na kumuheshimu mnooo.. Sasa nikiwaambia hayyo kesho na keshokutwa sijui watamtazama vp usoni...hajawahi kulalamika kwa ndugu zangu kuhusu mapungufu yangu na mimi ni mwanadamu siko perfect...
Hakuna unachokikwepa, tukikupa ushauri wa kuondoka na kuanza upya,mwosho wa siku ukiondoka si watataka kujua kwa Nini mmetengana?. Si ni bora ukawaeleza Sasa?.
 
Mimi nilikuwa muhanga wa talaka nilipotengana na mzazi mwenzangu. Alikuwa na rafiki yake ambae ni hakimu wa kiteto. Akamuuliza namna tunaweza talikiana akasema mimi ninatakiwa kwenda mahakamani kifungua kesi ya madai ya talaka. Nilipoenda nikapewa maelekezo ya kufuata kufungua file na kulipia. Alafu nikapewa barua ya wito ya mwanaume nimpelekee alafu tukapewa tarehe ya kuja.

Siku ya kusikilizwa tulisikilizwa wote na hukumu ikatoka siku hiyo hiyo na mwenzangu alilipia hati ya talaka akapewa nakala yake.

Kinachofanya suala la talaka kuchukua muda mrefu ni mali. Hili la tulichuma wote tugawane ndio linafanya mchakato unakuwa mgumu na mrefu
Pole na hongera kwa maisha mapya...je mlikua mmejenga au kua na assets pamoja?
 
Ushauri kwenye mambo ndoa ni mgumu sana,hasa katika kipengere cha usalti.
Sanasana nakushauri tu jipe moyo kwanza ikiwezekana ukae mbali na mume wako akili yako itakupa solution either uendelee naye au aendelee na maisha yake.
Bila hata ya kukaa kutafakari..hawezi kubadilika kamwe...i know him more than ten yrs
 
Ya Kwanza ndo Yenyewe hakuna zaidi ya hiyo inayoweza kumuumiza mwanamke maisha yake yote,ndo maana akasema “matokeo” ndio yanayomuumiza
kama ni hilo la kwanza linasameheka.
Anatakiwa afikirie ugumu wa maisha atakayopitia yeye pamoja na watoto wake.
Kisha alinganishe akimsamehe na kuendelea na mume wake anapata hasara gani kama mume anaitunza familia,anajua wajibu wake.
Wenzake huwa wanasusa na kuomba talaka endapo huyo mume hatunzi familia yaani endapo pesa zote na mahitaji yote anapelekewa mchepuko
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
Kubalianeni tu kutunza watoto na kwa kweli moyo wa mwanamke hauna reverse milele. We Anza zako upya na watoto wako kuwa busy na Kaz zako na nakuapia utapata mtu atakupendaaa na wanao wotee, usiogope chochote
 
Nashukuru sana. Mume wangu alikua kila kitu changu...sahivi ninavyomuona...kamwe na katu siwezi kurudisha lile pendo...nimejeruhika na kuathirika kimwili, kiroho na kiakili..
 
Uamuzi unao wewe.
Kuna dada yangu mmoja alikua kwenye ndoa yenye mateso kibao, na yeye alihofia kuondoka kwenye hiyo ndoa kwa kuwaza mustakabali wa watoto wao (walikua wamejaliwa watoto 4, ndoa yao ilikua na miaka 12). Mwisho wa siku alikuja kufariki kwa ugonjwa wa HIV/AIDS. Akawaacha duniani hao watoto ambao alikua anahofia kuondoka kwenye ndoa kwa ajili yao. Mume ambae ndie alimuambukiza bado yupo pia anadunda.
The bottom line is, "Uamuzi ni wa kwako". Kuanza upya inawezekana ila ni pale tu wewe utakapoamua na kuamini inawezekana.
Kuna mtu aliwahi kusema, "whether u believe you can or you cant, you are right."
Tuliza akili ufikiri kwa kina ni nini hasa unakitaka, halafu fanyia kazi maamuzi yako.
kissgarage
Exactly, hata akipona ukimwi bado magonjwa ya moyo na mambo mengine mengii, imagine huyo mume hayupo dunian tu Anza zako freshhh
 
Kubalianeni tu kutunza watoto na kwa kweli moyo wa mwanamke hauna reverse milele. We Anza zako upya na watoto wako kuwa busy na Kaz zako na nakuapia utapata mtu atakupendaaa na wanao wotee, usiogope chochote
Kwakweli naogopa haswa kuanza upya..idadi ya watoto nilionao na sina ajira...nakata tamaa kabisa
 
Find ur own happiness siku ukijifunza kujipa furaha mwenyewe na milango mingine mikubwa itafumguka, ukiona mahali furaha vituko vimezidi pianeni space and move on with life. Mimi principle yangu maishani furaha yangu na peace of mind ni muhimu kuliko chochote coz we live once, so ukiogopa kusepa kisa jamii huku unaumia wewe waweza kufa uache watoto wako yatima, pia nowdays ndoa sio quarantine Bora kujiimarisha kiuchumi, wewe ungekuwa uko vizuri usingewaza Mara mbili kunyanyuka na kuanza life
Hivi wewe umeolewa kweli?mbona huwa unarahisisha tu mambo in a negative way
 
Back
Top Bottom