Pole... Afya yako ipo matatani kivipi!? Hauli vizuri sababu ya hizo lumbulumbu hivyo afya inazorota(lumbulumbu inamfanya mtu awe aio mlaji, ama awe mnene kupitiliza kwa kula kula hovyo vitu vya sukari) , ama hizo lumbulumbu zinakuletea maradhi kama meno ama kisukari(allah akuepushe)
Kama ni afya inazorota onana na daktari akueleze vyakula unavyopaswa kula, ndio uwe unatembea navyo.. Mfano kwenye gari utembee na vitu ambavyo ukila vina faida mwilini, kama vile tende, ndizi, matunda kama zabibu n.k, na kama ukiweza ufanye mazoezi hii itakuongezea hamu ya kula.
Mie pia lumbulumbu ni matatizo yangu lakini sasa nimeweza kidogo kujikontroo, kioindi nikiwa sina mazoezi naweza kuka mlo mmoja tu wa maana, ikawa ndio nitolee hiyo, kiasi sasa nahisi dalili ya vidonda vya tumbo (allah atuepushe na haya maradhi) kwa kuligundua hilo, nikaonheza bidii ya mazoezi, atleast sasa napata milo miwili ya nguvu ama mi3 kabisa.. Nakula kula lakini vitu ninavyohisi vina manufaa mwilini, ndani tende hazikauki, halafu nje nakula kula vimachungwa, mara ndizi, n.k
Kingine kama ww si mpishi mzuri basi tafuta mpishi mzuri awe anakupikia msosi ule unaotaka ww, sababu mara nyingi watu wa lumbulumbu tuna kauvivu fulani kakula na tunatafuta vijisababu ilimradi tusile pia wabaguzi wa misosi, unaweza siku ukaamka ukajikita unahamu tu na tambi nyama, sasa hiyo usipopata ndio huli unaishia kutafuna tafuna tuvitu twa hovyo, mie namkubali bimkubwa wangu kwenye upishi hivyo wakati mwingine nafunga safari kwenda kudoea kwake, mie mwenyewe mvivu kupika, pia vyakula vya mgahawani nabagua saana
Nazungumza kwa uzoefu na elimu yangu ndogo ya misosi, vizuri zaidi msake mtaalam wa afya, umueleze tatizo lipi linasababishwa kwako kwa hizo lumbulumbu.
Lumbulumbu ni ina gharimu kishenzi unaweza jikuta kizeembe tu 10 elfu imekatika, na hakuna cha maana ulichokula, mara sijui umekula ubuyu, mara umenunua ice cream, mtaa wa kwanza mtaa wa pili mara umechukua chocolate basi ili mradi tu[emoji23][emoji1787]
Ama kama lumbulumbu inakufanya uwe Chibonge(aina hii ni wachache saaana) watu wa lumbulumbu hawawi vibonge kama
Shunie basi kwenye vitu vya kula kula, pendelea apple [emoji520] na maji kwa wingi, fanya hima ugide maji ya kutosha.