USHUHUDA: Nilivyokutana na ushirikina kazini

Sidhani kwamba katika kazi zao kama hizi wanatumia uchawi, mara nyingi wanatumia elimu na vifaa bora ili kufanikisha malengo yao, naamini uchawi au ushirikina wanao ila sidhani kama wanatumia ktk mambo kama ya sayansi, Mm naishi nao huku
Umeambiwa mashine ilikuwa mpya
 
Hiyo ndy Tanga bwana ...

Mwaka juzi Ndugu yangu form six alipangiwa JKT mkoa wa Tanga .Siku moja wanakimbia mchakamchaka,kundi Lao kwenye uelekeo wanakokwenda wakawaona watu wawili wanakuja.Watu wale walionekana km wanaenda shambani hivi,Ile wanataka wakaribiane wapishane Yule mtu mmoja akadondosha Mia 5 .Kwa sababu hakujua km ameangusha ela akaendelea kutembea Tu km hakuna kilichotokea,kumbe lile kundi la mchakamchaka wale wote waliopo mbele waliiona Ile Mia 5.Walipopishana na wale watu wawili mbio zikaanza kukimbilia Ile ela, Kwa bahati akafanikiwa kuiokota ndugu yangu.

Mchakamchaka ukaendelea kurudi kambini.Njiani Hali ya dogo ikachenji ghafla,kichwa kilimuuma Hadi akaanguka chini.kwa sababu ilichukuliwa ni Hali ya kawaida Kwa watu ku-faint wakati wa mazoezi makali basi wakambeba wakajua ni Hali ya kawaida ambayo huwakuta wengi wakiwa mazoezini.Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi.wakati ananisimulia akanambia wakati amelala chini akawaza kwamba mbn hii Hali imemkuta ghafla sn na wala hakuwa amechoka na mazoezi makali km walivyomtafsiri watu?Ghafla mwili ukazidi kuisha nguvu. Akakumbuka dakika km kumi hivi nyuma alikimbizana na wenzie na kufanikiwa kuiokota Ile Mia 5,alichokifanya ni kuingiza mkono mfukoni na kuitoa Ile hela akaitupa.Dakika km mbili jasho Kali lilimtoka kisha akapata nguvu akainuka Hadi watu wote waliopo pale wakamshangaa maana Walikuwa wanafanya utaratibu wamkimbize hospitali

Alipowasimulia kwamba baada ya kuitupa Ile Mia 5 aliyoiokota ndy akajiskia vizuri,wataalamu wa mambo wakamwambia nyie wa kuja mujiangalie sn hapa Tanga.Ndugu yetu Una bahati sn maana wale jamaa wawili mliopishana Walikuwa ni wachawi na muda si mrefu ulikuwa ufe kisha uwe msukule
 

Tunayo sheria ya uchawi, witchcraft Act ya siku nyingi sana hii sheria tangu mkoloni miaka ya 1930s kama sijakosea. Uchawi Tz ni kosa kisheria Mkuu na kesi zipo.

Ndugu wazungu ni washirikina walioshindikanika hasa hawa wanaokuja kutalii huwa wana mambo mengi sana huwezi ukaamini kabisa.
 
Naamini ni wachawi sana ndio pia wanaomiliki freemanson, but sisi uchawi wetu mara nyingi tunatumia kudhuru
 
miaka kadhaa iliyopita niliwahi kusafiri kikazi ktk kijiji kimoja mkoa wa tanga kinachopatikana katikati ya segera. bahati mbaya sikikumbuki jina.

nilikaa pale kijijini kwa siku tatu nikiwa kama mratibu wa mradi fulani hivi uliofadhiliwa na UNICEF.

kijiji kile kilikuwa hakina umeme na makazi ya wenyeji yalikuwa duni.

kilichonishtua ni gari za watu binafsi zilivyokuwa zinapishana kuja pale kijijini. nilikuwa nashangaa kila baada ya nyumba mbili au tatu, nje zinaonekana gari binafsi zime park.

nilipomuuliza mwenyeji wangu, akaniambia kijiji hiki kina wachawi na waganga wengi.

gari ambazo naziona nje ya vijumba vile vya udongo ni za wateja wa masuala ya ushirikina kutoka sehemu mbalimbali nchini na nchi jirani ya kenya.

kinachowaleta pale kijijini ni kutafuta huduma za kichawi za kuimarisha biashara, kutafuta ukubwa wa vyeo vya kisiasa na mengineyo.

hapo ndio nikakumbuka ule usemi wa "nyumba mganga nyumba mchawi". hiyo ndio tanga mzee baba.
 
Mchawi analoga machine au mashine ''inaharibiwa'' na mizimu? Karne hii bado unaamini? Pole sana.
 
Usijidanganye kuwa wanakuja kifara
 
Kwani waarabu ,Wachina na wazungu hawana hizo mbanga MIGODINI?!!

Ungeishi nao ungekuwa na la kuhadithia hapa....🀣🀣
FYI, Waarabu wapo Oman wanaangalia, wanatazamia karai la maji wanaona MADINI YA KILA AINA huku Tanzania....
Mabeberu wapo Majuu wanatazamia kwa Satelite wanaona muamba na migodi yote....

WaChina wapo barani ASIA wanakuja na vifaa Minerals Detectors vyombo vinatoa results positive reserves....

Sisi tuna leta vikuku,vifaranga elf 20.....
Tutafika kweli... STRUGGLE MAN
 
Sidhani kwamba katika kazi zao kama hizi wanatumia uchawi, mara nyingi wanatumia elimu na vifaa bora ili kufanikisha malengo yao, naamini uchawi au ushirikina wanao ila sidhani kama wanatumia ktk mambo kama ya sayansi, Mm naishi nao huku
Mkuu, hapo kwenye VIFAA bora; hivi Excavator ya mshkaji yenyewe haiingii kwenye vifaa bora?
 
Kwa wale ambao ndio kwaza mnaingia makazini, nyie mjifanye waluga luga tu mbadili viti vilivyotumika na wastaafu, huwa vimebeba mambo mazito
Kuna mshua mmoja alipata teuzi, kwa bahati mbaya alivyofika kwenye ofisi ya alietenguliwa hakujisumbua kutoka furniture alizozikuta.

Kwa ufupi ni kwamba, aliugua ugonjwa wa ajabu hadi mauti yakamfika nakubaliana na wewe maofisini kuna siri kubwa sana.
 

Tatizo waswahili tuna shida sana! Mzungu akiua Mswahili mgodini hicho ni kifo cha kawaida ila ngoja mtu afie kwenye mgodi wa mswahili!! Tambiko.

Nimefanya nao kazi sana, wanaloga kinyama na hakuna wanachofanya bila kuloga. Ajabu alikuwa hatoi pesa au malipo siku ya Jumanne watu wakachukulia kawaida kumbe majini yake yamemkataza!! Fanya wewe mswahili uone utavyoandamwa na kashfa za uchawi.
 
Mimi the same story nimechoma pesa Mingi kufukua madini KILA wakifikia vein dongo linakatika unaanza upya upya means kuchoma milioni.Kuna jamaa yupo pembeni anasema wanajisumbua tu haiwezekani wa kuja waondoke na madini akimaliza kufukua tu tunakata ufa mwingine.Madogo wakaenda kwa mtaalamu Mimi siamini mtaalamu akawaambia mmechelewa ilikuwa kumaliza tu Kazi linashuka dongo jingine chini lakini nitalizuia lisianguke shimoni akafanya yake kweli aisee halijaanguka.
Haya mambo yapo aisee.
 
Kule anaenda kupewa nguo kisha anaachiwa Ili raia wasimdhuru
 
Mikoa ya tanga, Lindi, pwani hii imefungwa kichawi ni ngumu Sana kuwa na maendeleo hadi zindiko liondolewe upo uchawi wa kuuroga mkoa mzima usiwe na maendeleo.Afrika ya weusi yote ni kama imerogwa thus hakuna maendeleo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…