USHUHUDA: Nilivyokutana na ushirikina kazini

USHUHUDA: Nilivyokutana na ushirikina kazini

Mchawi analoga machine au mashine ''inaharibiwa'' na mizimu? Karne hii bado unaamini? Pole sana.
Nimesoma nikaishia kucheka tu!kwenye migodi usipokuwa nunda utaambiwa had upeleke nywele za sehemu nyeti..ila wakishajua boss hatak masuala hayo waka husumbuliwi na kitu !na huko waganga wamejenga majumba ya fahari kupitia wehu kama hawa
 
Tunayo sheria ya uchawi, witchcraft Act ya siku nyingi sana hii sheria tangu mkoloni miaka ya 1930s kama sijakosea. Uchawi Tz ni kosa kisheria Mkuu na kesi zipo.

Ndugu wazungu ni washirikina walioshindikanika hasa hawa wanaokuja kutalii huwa wana mambo mengi sana huwezi ukaamini kabisa.

Natamani kujua hukumu mojawapo ya mchawi ambaye yuko jela kwa kosa la uchawi. Kuhusu wazungu ni hawafai [emoji119] wao wana vyuo kabisa vya witchcraft and wizardry [emoji23] wao hawapai kwa ungo, wanasafiri kwa ufagio [emoji3472]
 
Mikoa ya tanga, Lindi, pwani hii imefungwa kichawi ni ngumu Sana kuwa na maendeleo hadi zindiko liondolewe upo uchawi wa kuuroga mkoa mzima usiwe na maendeleo.Afrika ya weusi yote ni kama imerogwa thus hakuna maendeleo
Mimi kwetu Lindi ..siku moja nilikuwa na mgeni kwenye gari tunatoka Dar tunaenda masasi,tulipofika Lindi mjini akaniuliza hapa wapi nikamjibu hapa ndy Lindi mjini.akakaa kimya me nikafungua dirisha nikaangalia nje huku natabasamu huku gari likiwa linatokomea mdogomdogo 50 km/ h kuelekea masasi
 
Mikoa ya tanga, Lindi, pwani hii imefungwa kichawi ni ngumu Sana kuwa na maendeleo hadi zindiko liondolewe upo uchawi wa kuuroga mkoa mzima usiwe na maendeleo.Afrika ya weusi yote ni kama imerogwa thus hakuna maendeleo
Nakubaliana nawe kwa hili....
 
FYI, Waarabu wapo Oman wanaangalia, wanatazamia karai la maji wanaona MADINI YA KILA AINA huku Tanzania....
Mabeberu wapo Majuu wanatazamia kwa Satelite wanaona muamba na migodi yote....

WaChina wapo barani ASIA wanakuja na vifaa Minerals Detectors vyombo vinatoa results positive reserves....

Sisi tuna leta vikuku,vifaranga elf 20.....
Tutafika kweli... STRUGGLE MAN
Akhui ulisemalo ni kweli...hao jamaa kweli wana teknolojia kubwa kabisa usemayo.....ila hizo "mbanga wanafanzanga"...huko migodini kuna mengi akhy....

Wanaitafuta fedha kwa njia tofauti hao mabwana....

Wachina wao Mungu wao fedha....waulize waliofanya nao kazi katika SHUGHULI za ujenzi n.k

All and All Mungu Mwenyezi ni Alpha na Omega...huwwal awwalu wal akhiru!!
 
sasa kama hawa watu ni wachawi kwanini wasiroge hayo madini yakatoka chini yakaja juu yenyewe wawe matajiri... tunahangaika kuchimba gas na mafuta wakati wao wanaweza kufanya miujiza, waanze sasa kutuletea gas kutokea ardhini baharini ikaja juu...

Inanikumbusha kisa cha jamaa mwenye uwezo wa kufufua watu kwenye makanisa halafu wapendwa wetu wakifa anajikausha hata kuongelea hilo swala...
 
Hapo umeliwa hao waliokwenda kwa mganga huenda kuna mahali wamechezea so baada ya huyo kukuita chemba mwenzake ameenda fasta kurekebisha kisha wakachukua hiyo buku 20 na kutia mfukoni mimi bado siwezi kushawishika kama kweki uchawi upo mpaka niuone na kuugusa kama babu yangu thomaso.
 
Mradi wa Barabara ya Bagomoyo Msata aisee kuna Operator wa Excavator kama kapata dharura kipindi hicho basi huwezi kutumia machine yake yaan hata kuwaka haiwaki hata uweke mafundi namna gani,
Mwisho wa siku Boss alimtumua kazi...
 
Cha kushangaza akija mzungu, mchina au muarabu kuchimba kunakua hakuna vikwazo kama hivyo na wanafanikiwa kuchimba na kupata wanachokihitaji.

Pia ninashangaa Serikali haiamini uchawi ila anapokamatwa mchawi kaanguka uchi wanatia pingu na kumpeleka kituo cha polisi je kule anaenda kama mtuhumiwa wa nini au anaenda kuhukumiwa kwa kutokuvaa nguo yaani anatembea uchi.
Mchina au Muhindi ni mchawi acha tuu, hapo anaweza kuja kuwapa vitunguu watu wa hapo site, anakuja babu anamwaga maji kuzunguka eneo
 
Hiyo ndy Tanga bwana ...

Mwaka juzi Ndugu yangu form six alipangiwa JKT mkoa wa Tanga .Siku moja wanakimbia mchakamchaka,kundi Lao kwenye uelekeo wanakokwenda wakawaona watu wawili wanakuja.Watu wale walionekana km wanaenda shambani hivi,Ile wanataka wakaribiane wapishane Yule mtu mmoja akadondosha Mia 5 .Kwa sababu hakujua km ameangusha ela akaendelea kutembea Tu km hakuna kilichotokea,kumbe lile kundi la mchakamchaka wale wote waliopo mbele waliiona Ile Mia 5.Walipopishana na wale watu wawili mbio zikaanza kukimbilia Ile ela, Kwa bahati akafanikiwa kuiokota ndugu yangu.

Mchakamchaka ukaendelea kurudi kambini.Njiani Hali ya dogo ikachenji ghafla,kichwa kilimuuma Hadi akaanguka chini.kwa sababu ilichukuliwa ni Hali ya kawaida Kwa watu ku-faint wakati wa mazoezi makali basi wakambeba wakajua ni Hali ya kawaida ambayo huwakuta wengi wakiwa mazoezini.Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi.wakati ananisimulia akanambia wakati amelala chini akafikiria kwamba mbn hii Hali imemkuta ghafla sn na wala hakuwa amechoka na mazoezi makali km walivyomtafsiri watu?Ghafla mwili ukazidi kuisha nguvu. Akakumbuka dakika km kumi hivi nyuma alikimbizana na wenzie na kufanikiwa kuiokota Ile Mia 5,alichokifanya ni kuingiza mkono mfukoni na kuitoa Ile hela akaitupa.Dakika km mbili jasho Kali lilimtoka kisha akapata nguvu akainuka Hadi watu wote waliopo pale wakamshangaa maana Walikuwa wanafanya utaratibu wamkimbize hospitali

Alipowasimulia kwamba baada ya kuitupa Ile Mia 5 aliyoiokota ndy akajiskia vizuri,wataalamu wa mambo wakamwambia nyie wa kuja mujiangalie sn hapa Tanga.Ndugu yetu Una bahati sn maana wale jamaa wawili mliopishana Walikuwa ni wachawi na muda si mrefu ulikuwa ufe kisha uwe msukule
dunia ina mambo
 
Sidhani kwamba katika kazi zao kama hizi wanatumia uchawi, mara nyingi wanatumia elimu na vifaa bora ili kufanikisha malengo yao, naamini uchawi au ushirikina wanao ila sidhani kama wanatumia ktk mambo kama ya sayansi, Mm naishi nao huku
Mkuu unaishi nao wapi,wale jamaa kwa kutambikia hawajambo kabisa hasa pale siku ya kwanza kabisa ya kuanza kazi,inawezekana wewe hua unakuta kazi ilisha anza miaka kadhaa nyuma huko,hapo huwezi kujua.
 
Back
Top Bottom