USHUHUDA: Nilivyokutana na ushirikina kazini

Hufunga Akili, mwili, nafsi, moyo na macho. Unajifariji huku unaumia.

Mwaka 2012 nilifunga biashara sehemu fulani baada ya kuona mambo hayaendi, na nikahama. Baada ya kuhama nikapata mfanikio.
Nikapazoea, nikaanza kufeli tena. Nikafnga Biashara, nikahama. Hapa nilipohamia nimepiga sana hela, ila sasa hivi naona mambo yaanza kugoma. Nina mpango wa kupahama.

Mitume wenyewe walihama, mimi nani nisihame pale nionapo mambo hayaendi.

Usipofanya hivyo, hutoboi.,
 
Hakuna kitu kinachosikitisha kama kukatisha uhai wa mnyama hasa asiyeweza kujitetea.Kuku hana kosa lolote anafukiwa akiwa hai.Mnyama kama huyu anastahili kuishi kama nyie mliyemfukia mnavyostahili kuishi
aile Jah
 
Uliza watu wa Kiteto (jirani na huko unakokutaja)

Barabara kuu ile ya Kondoa-Handeni kuna sehemu kibao zina vikonakona vya ajabuajabu ukiuliza unaambiwa humo ilishindikana kunyoosha kwa vikwazo hivyo hivyo

Sehemu moja inaitwa Jangwani hapo kuna mti (wanauita msane) mkubwa sana upo pembeni kidogo tu mwa barabara lakini hauangushwi hata (hifadhi ya) barabara itanuliweje. Unaambiwa hao madereva wa greda (kipindi cha nyuma) kila aliyetaka kuuangusha basi anajikuta kupata dharula kwa kuumwa au kuchoka au kivyovyote tu na wakisema wafanye siku nyingine ndo imetoka hiyo mpaka ikabidi waachane nao huo mti

Kuna Mzee mmoja pale Kibaya alikuwa anajulikana kama "Shehe Kasim" wanasema savei ya kwanza kabisa ya hiyo barabara ilisemekana ipite shambani kwake basi akaenda na vigingi viwili tu akagongelea shambani kwake kimoja pale ilipoambiwa barabara itaingilia na kingine kule mwisho itakapotokea halafu akasema "haya sasa na valime hiyo barabara"... mpaka leo barabara ile imepita kando mbele ya shamba hilo

Sehemu nyingine inaitwa Mafuleta (Handeni) napo kuna mti ila huo sasa ni zaidi ya ule wa Kibaya maana mpaka barabara ikalazimika kuhamishwa kwajili ya maafa yake

Kulifanyika savei (sijui mnaitaje watu wa barabara mimi nimeona nitumie hilo neno) zamani sana ikaonekana baadhi ya watu wavunje nyumba zao barabara inataka kuwa kubwa Wakavunja waliovunja lile swala likapita kukawa kimya mara ikaja tena kwamba hata zile mita za kujenga kutoka road ilipo zimeongezwa yaani kama ulivunja ukajenga kando ya barabara inabidi uvunje tena usogee kando zaidi. Hapo pia walifanya hivyo waliofanya lakini mpaka leo hakuna kinachoendelea na badala yake ikaja kusemekana barabara (hiyo kubwa walokuwa wakiisema) haitapita pale senta tena bali itakunjwa ipite kando ya mji. Sasa cha ajabu wakati hayo yote yanaendelea tangu mwanzoni tu kuna "mabingwa" walikuwa wanasema "hapa haiwezekani na tutaona kama watapitisha hiyo kitu hapa"

Hayo mambo yapo ila namna ya kusolve tu ndo watu wanaenda tofauti, mfano hiyo ya kwenu ya kuzika viumbe wangali hai
 
👍👍👍👍

Haswaaaa....
 
nlimwadithia mfanyakazi mwenzangu mwenye uzoefu wa miaka mingi kazini kuhusu kusitasita kuja kazini.
alinipa ushuhuda wake binafsi...
"wewe unasita tu kuja kazini! ...mimi nliacha kazi kabisa."
Sijaelewa... kwamba aliacha kazi "kabisa" kisha akapata nyingine ambayo ndiyo hiyo amekuwa mzoefu kwayo au?
 
Unachekesha kweli KakaMkubwa... yaani mtu kwa kupalilia kupepelea kupata elfu ishirini ndo apoteze nguvu na (pengine hata) hela nyingi zaidi ya hiyo!!? Kweli? You can't be serious

Bora ungesema mitambo ilichoka tu au ilikorofisha tu kwa muda na kisha ikakaa sawa ila siyo kusema upigaji wakati umeambiwa wote walikuwa wakichakarika bila mafanikio
 
Mnyama Ni mnyama na ndege Ni ndege
Embu tafuta neno animal tujue maana yake.Kwa kukujuza zaidi hata sisi binadamu ni wanyama lakini wa level nyingine compared to other animals.

animal (plural animals)

  1. In scientific usage, a multicellular organism that is usually mobile, whose cells are not encased in a rigid cell wall (distinguishing it from plants and fungi) and which derives energy solely from the consumption of other organisms (distinguishing it from plants).
 
Mama angu ni rafiki angu Sana alinisimulia hiki kisa......


SINEMA ILI ROGWA ISIONYESHE,

Waonyesha SINEMA walipeleka onyesho la SINEMA kijijini....

Maajabu ni kwamba watu walipo jaa ukumbini SINEMA inagoma kuonyesha....wakitawanyika inaonyesha......

Yaan ukawa ivyo mpk onyesho likazuiwa...
 
Ukijua tofauti ya polisi na kibaka utaelewa tofauti ya mganga na mchawi
Sikweli , huwezi kuwa mganga bila ya kujua kuroga, mwanajeshi hawezi kujua kutegua Bomu hasilojua kulilipua na kuua, huwezi kutegua mtego husiojua kuutega!


Kule Bungu , Mkurunga, kuna mganga mmoja ambaye akikosa wateja alikuwa anaenda njia panda usiku wa manane kuroga ili watu wanaopita hapo waumwe alafu waje awatibu !

Waganga wengi (kama sio wote) ni mawakala wa uchawi huo huo (agents) sema kazi yao ni kutegua uchawi, ndio maana kuna baadhi ya watu wanaenda kwa waganga hao hao kutaka kuwalipiza kisasi au kuwakomoa watu wengine wafukuzwe kazi, waumwe, wafe, wafilisike n.k. sasa kama mganga sio mchawi kwanini anatoa dawa au anafanya uganga kumdhuli mwingine?! Kutoa dawa majambazi wasikamatwe n.k.?! Huo pia ni uchawi tu!
 
kumbe haya mambo ni mapana!
 
Sidhani kwamba katika kazi zao kama hizi wanatumia uchawi, mara nyingi wanatumia elimu na vifaa bora ili kufanikisha malengo yao, naamini uchawi au ushirikina wanao ila sidhani kama wanatumia ktk mambo kama ya sayansi, Mm naishi nao huku
Wachaw bhn tena wahind ndo balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…