Ushuhuda: Niliwahi kutembea kwa mguu kutoka Posta mpaka Goba baada ya kukosa nauli

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.

Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.

Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.

Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.
 
Posta Goba haizidi 20km, unaona kama umetembea mbali sana?

Wamama huko vijijini wanatembea hadi 25kms kufuata maji kila siku kwenda na kurudi. Nenda singida watu wanatembea na punda 40km kwenda kutafta maji na kurudi.

Wasukuma huko Shinyanga wanatembea zaidi ya 50km kwenda minadani kuuza viazi ama mahindi ama pamba tenda wamejitwisha kichwani.

Posta Goba unaona mbali sana ndugu?
 
Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.

Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.

Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.

Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.
Usikute una PASSO unadai unamiliki Gari
 
Ebwana umenikumbusha mbali sana, maisha haya yana mitihani mingi mno lakini kikubwa ni kutokukata tamaa kabisa
 
Back
Top Bottom