Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Hongera sana kwa kupiga hatua. Naamini hicho kitu kilichobakia na cha kukifanya mwaka huu, kitakua ni kitendo cha kushangaza na kushtua wengi cha kujiunga na CCM 😇 huku ukikisifia hicho chama na Mwenyekiti wake kwa kukutoa Jalalani na kukufanya uwe na maisha bora!!Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.
Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.
Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.
Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.