Ushuhuda: Niliwahi kutembea kwa mguu kutoka Posta mpaka Goba baada ya kukosa nauli

Ushuhuda: Niliwahi kutembea kwa mguu kutoka Posta mpaka Goba baada ya kukosa nauli

Niliwahi tafuta kazi nikapata kazi wanapofywatua matofali,nikaambiwa nipange vile vibao vinavyowekewa tofali.

vibao n vingi nadhani unaweza jazaa semi trela hata 5 nilipanga vile vibao kuanzia asubuhi to jioni saa 1 hivi nikaja pewa posho 500 yes ni mia tano yani mia mia tano..

hapo.mgongo wote unauma nina njaa sielewi hii jero naitumia kununua nini,nashukuru kipind kile kulikua namama mmoja anauza mama ntlie nilienda nunua Ukoko wa 500 akanimwagia na mamichuzi nikala ule ukoko Japo uliniumiza tumbo sana ila n moja ya memory chungu sana kuwahi tokea maishani mwangu.
 
Maisha acha tu,Umeshawahi kuskia kiu mpaka ukanywa maji ya mtoni wewe?

Katika kubana bajeti na matumizi,Nilinunua tomato yangu chupa 1200 ile kubwa ndio ilikua mboga yangu kila siku na ugali.Tunaita ugali tomato (haya n maisha tu) tena tomato enyewe unaitumia kwa kujibana knoma noma isiishe,nikikuonyesha tomato ninayolia ugali unaweza hisi sitomaliza ugali ila nlikua namaliza ugali wote tomato nloweka haijaisha.

Ukiona mtu anaweza kula milo mi 3 kwa siku bila kujali aina ya milo anayokula ni moja ya achievement kubwa sana maishani.

maisha si rahisi kama watu wafikirivyo,Maisha yakikuamulia unaweza kula ugali na uji ukafanya mboga..This is life.
Kwa uchungu sana
 
Katika kutafuta kazi kuna siku nilizunguka weee tafuta kazi nagonga maget ya watu naomba kazi nikafika nyumba 1 nikaomba kazi akatoka huyo mmama akaniambia njoo huku nikupe kazi.

Akanionyesha mti niukate kisha niung'oe kbsa pale ulipo kusiwe hata na alama kama palikuaga na mti, kazi nikaanza.

Nikafanikiwa ukata mti,nikaukatakata matawi nikaenda yachoma moto huko.Kazi ikaja kwenye kisiki kilichobaki kukitoa na yule maza alisema nitapomkabidhi kazi ndio atanipa hela.

Nilihangaika na kile kisiki kumbe ule n mti ambao unatakiwa uchimbe shimo kwa pembeni uendee chini sana ili ukakate Mzizi mkuuu ndipo kisiki kinaweza kutoka (mimi sikua najua hayo)

nilihangaika na kile kisiki siku 3 hakitoki,yule mama haelewi somo lolote akija kuniangalia ananiongelesha kwa mazarau ananigombeza namuharibia garden yake nk

Ile kazi ilinishinda nikaondoka nikaitelekeza,ila hapo nimeshashnda ile nyumba zaidi ya 4 days nafanya kazi siku nzima bila mafanikio na mwsho hakuna nlichofanikisha.

basi ndio maisha nikamuachia Mungu.
 
Maisha acheni ndugu zangu ukiona mtu anatoka nyumban jion anajua ntarudi asee mshukuru sana Mungu,kuna wakati maisha yanakutandika hadi ukimuona kuku au mnyama yeyote wakufugwa anahudumiwa anapewa labda chakula au maji Unamuonea wivu unasema Bora namimi ningekua yule Mbwa saivi ningekua napakulala pakula,nk Kagiza ndio hakoooo kanaingia hujui hata unaenda wap...

weeee acheni maisha bwana acheni nyie
 
Kutembea kwa.miguu ilifika mahali nikawa nimechoka kuomba nauli na kuomba msaada nikawa nikiona gari lolote lenye bodi lenye stand nadandia twendeeee sijali n pickup au daladala mimi nadandia lolote linaloenda njia ninayopita.

nakumbuka.kuna siku nilidandia gari.moja mwenye gari nilipopanda akaongeza speeed sana mimi nkawa nashukuru.mungu,ghafla akapga breki ya paap ile breki ikanirusha ndani ya gari,Asee niliinuka nikakurupuka Japo niliumia sana ile siku maana nilivyodondokea ndan ya gari nilienda jigonga mahali vibaya nikaumia mno.
 
kuvaa nguo 1 je? unavaa nguo hyo hyo muda wakufua unaenda mtoni usikuuuuu unavua nguo zotee unafua nguo yako uloivaaa kisha unaikung'uta mpaka maji yanapungua then unairudisha mwilini ikiwa.mbichi hivyo hivyo.

Unatafuta mahali penye wanauza chips unaenda unasimama pemben ya jiko ili upate joto nguo walau ikauke basi unashnda na nguo yako hyoooo mpk kesho yake inakuja kukaaukia mwilini.

kuna kipindi nguo ilichakaaa mpk nkawa nasema leo nikikutana na mtu anaenijua si itaakua aibu sana maana nilikua nusu chizi kwa ule muonekano,Lakini yote n mapito na sasa tunasimuliana kama story ila usiombe yakukute.

Kuwa na pair 1 ya nguo acheni nyie Kuna watu hiii dunia wanapita ktka changamoto za maisha.
 
mtu yyte mwenye gari (liwe lake tu) Muheshimu sana bila kujali n passo au vits namba A ilimradi ni gari,mpe heshima kubwa sana.

Duh lakini Passo inataka moyo bwashee.Mwenyekiti wetu wa Ukoo ana Passo kila tukimaliza vikao vya Ukoo lazima akipige mzinga wa mafuta.

Basi kila nikomwona mtu anaendesha Passo namchukulia kama Mwenyekiti.Halafu wamiliki wengi wa Passo wana kiburi na wepesi sana wa kuchomekea.
 
Watu wametembea katembe katembee huko msumbiji kuitafuta SA baada ya kukosa nauli na kwenye mbuga ya wanyama na wengine walipoteza maisha hapo mbona ni kama unatoka ndani na unaenda nje tuu mkiwaona na namba za GP Kama washkaji zenu jaribuni kuwauliza wengine walikua wanalala park station na wengine garden mpaka wanafukuzwa ila leo mkiwaona magari makubwa kama vile hawajalala nje Mimi niliwahi lala kwenye treni zilizokua zinapaki cape Town station siku moja nikalala ambayo inawahi saa kumi alfajiri kuwachukua wafanyakazi nikaamka nayo huko Belleville mziki ukaanza nishuke hapo Bellvile na nauli sina ya tiket ila vitu vya kawaida kwenye maisha..
 
Niliwahi tafuta kazi nikapata kazi wanapofywatua matofali,nikaambiwa nipange vile vibao vinavyowekewa tofali.

vibao n vingi nadhani unaweza jazaa semi trela hata 5 nilipanga vile vibao kuanzia asubuhi to jioni saa 1 hivi nikaja pewa posho 500 yes ni mia tano yani mia mia tano..

hapo.mgongo wote unauma nina njaa sielewi hii jero naitumia kununua nini,nashukuru kipind kile kulikua namama mmoja anauza mama ntlie nilienda nunua Ukoko wa 500 akanimwagia na mamichuzi nikala ule ukoko Japo uliniumiza tumbo sana ila n moja ya memory chungu sana kuwahi tokea maishani mwangu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Daah watu makatili sana...Jerooo

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Wewe unasema Goba. Mimi hadi Chalinze. Nikataka kuendelea hadi Moro wasamaria wema wakaingilia kati.

COVID sucks!
😂😂😂😂😂😂
Wasamalia wema wakainglia kati...😆😆
 
Nilishatembea kutoka Tanki bovu mpaka Kariakoo pale kwenye office za Gal sport betting kupeleka CV na sikufanikiwa pia. Maisha bana baada ya kugraduate huwa yana changamoto zake aiseee.
 
Tatizo lilianzia kwa mzee wako kutembea kuunga mkono azimio la Arusha, wewe..... then kwa mwanao atanyunda sana! Uwa zinatembea hizi kitu kizazi mpaka kizazi
 
Posta Goba haizidi 20km, unaona kama umetembea mbali sana?

Wamama huko vijijini wanatembea hadi 25kms kufuata maji kila siku kwenda na kurudi. Nenda singida watu wanatembea na punda 40km kwenda kutafta maji na kurudi.

Wasukuma huko Shinyanga wanatembea zaidi ya 50km kwenda minadani kuuza viazi ama mahindi ama pamba tenda wamejitwisha kichwani.

Posta Goba unaona mbali sana ndugu?
Hali ya hewa ya daslam Sio rafiki Sana kutembea umbali mrefu KWA miguu, joto linakuexhaust mapema Sana,binafsi umbali niliokuwa naweza kutembea huko kwetu kusini KWA miguu hapa daslam umbali huo ni changamoto
 
U
Me nilitembea kwa mguu kutoka posta mpaka tabata segerea , kwa kupitia njia ya ubungo, na siku nyingine nilipita njia ya gongo la mboto, ingawa bado sijafanikiwa , nipe Mbinu uliotumia kufanikiwa na kupata gari. Sandali Ali

Sent using Jamii Forums mobile app
Nishawahi kutembea kwa miguu toka Tandika Majaribio hadi Temeke Sudan
Kutokuwa na nauli bhana ni shida halafu unayaona magari ya Kariakoo yanakupita tu
Hiyo nizero distance sana kupanda gari nikuaribu nauli.
 
Watu wametembea katembe katembee huko msumbiji kuitafuta SA baada ya kukosa nauli na kwenye mbuga ya wanyama na wengine walipoteza maisha hapo mbona ni kama unatoka ndani na unaenda nje tuu mkiwaona na namba za GP Kama washkaji zenu jaribuni kuwauliza wengine walikua wanalala park station na wengine garden mpaka wanafukuzwa ila leo mkiwaona magari makubwa kama vile hawajalala nje Mimi niliwahi lala kwenye treni zilizokua zinapaki cape Town station siku moja nikalala ambayo inawahi saa kumi alfajiri kuwachukua wafanyakazi nikaamka nayo huko Belleville mziki ukaanza nishuke hapo Bellvile na nauli sina ya tiket ila vitu vya kawaida kwenye maisha..
Kuna wakati ukisimulia ushuda wa wengine,utashangaa.kuna watu wanashuhuda yu kanti bilivu guys.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Pole na hongera mkuu. Safari ya maisha ina mapito magumu sana
 
Back
Top Bottom