Ushuhuda: Niliwahi kutembea kwa mguu kutoka Posta mpaka Goba baada ya kukosa nauli

Ushuhuda: Niliwahi kutembea kwa mguu kutoka Posta mpaka Goba baada ya kukosa nauli

Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.

Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.

Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.

Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.
Mkuu pole sana,maisha lazima upitie changamoto ili utoboe,dhahabu ili iwe safi basis husafishwa na moto.
 
Dah Nilikuwa Natembea from Usa River hadi Makumira kule... Hakika Palikuwa panachosha mno weekdays zote au kibaya ukimuomba mtu lift ya Baiskeli anakuambia wewe ndio umuendeshe! ukipiga kasia mbili tatu nne za pedal unamuambia mkuu endelea zako tu...
 
Kuna mzee nilikutana naye tabora kaniambia alikuwa ana swaga ngombe toka shinyanga Hadi dodoma kwa mguu
 
Back
Top Bottom