Ushuhuda: Niliwahi kutembea kwa mguu kutoka Posta mpaka Goba baada ya kukosa nauli

Unanikumbusha mchizi mmoja nilikutana naye tazara akaniuliza ubungo ni wapi , nikamwelekeza sehemu pa kupandia gari, akanijibu yeye anafanya mazoezi ametokea kigamboni nilimtafakari yule mchizi kwa siku Ile mzima,
Ungempa buku ya maji.
 
Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.

Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.

Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.

Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.
Unaonekana una ego Sana.. Yani ulishindwa kuomba mianne mpaka utembee umbali wote huo?..
 
Pole.....ila huo umbali uliotembea mdogo sana..watu wanatestimony kubwa zaidi...
 
Samahani kwa lugha hii nitakayotumia.

Posta hadi Goba unaona umetembea sana? Hiyo distance hata mtoto wa nyoka si anafika na kurudi.

Kuna watu wametembea zaidi ya kilomita 80 kwa mguu acha kudeka kama kitoto cha nzige.
 
Mnaomshangaa mtoa mada Tatizo sio umbali. Tatizo kutembea Dar tofauti na uko mikoani. Dar kero bodaboda, bajaji, watu kibao, jua na joto, hafu mbaya zaidi unayaona magari kibaooo.

Mi kwa Dar umbali mkubwa ni Ubungo hadi Kongowe ya Mbagala.

Mikoani huko Songea hadi Iringa (2 weeks).

Sometimes uwa nawaangalia sana wale tunatoka Ubungo Mawasiliano tunataka kwenda Mlimani wanasema tupande bajaji. Dah. Wastage of Money.
 
Nyamwage mpaka kivinje kwa mguu we acha tu nimekutana na SIMBA Mara tatu dah
 
Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.

Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.

Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.

Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.

Huo umbali kama si zaidi ya km20 basi hayo ni mazoezi tu.
Hongera kwa kuwa ulifika salama.
Historia huandikwa namna hiyo
 
Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.

Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.

Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.

Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.
Uwoga wako ndio ulio kuponza..Ungepanda daladala mkuu, makondakta huwa hawanaga noma ungewambia wangekuelewa.
 
[Qmiambili E="fundi25, post: 38166079, member: 136622"]
Bado pafupi apo!!
[/QUOTE]
fundi25 Pafupi kama umeamkia Chapati tatu za mia mbili hamsini ama mia tatu na bakuli la maharage! Lakini umeamkia kashata na maji ya kufunga, ni parefu balaa!!!
 
Hakika maisha yana changamoto. Miaka 6 nyuma nikiwa katika harakati za kutafuta kazi Dar es salaam nikitokea mkoa nakumbuka nimewahi kuswaga mguu Posta- Goba baada ya mfuko kukosa mia 4 ya daladala.

Hii ilijitokeza mara nyingi tu. Unatembea mpaka unajiona huna akili au hauko katika hesabu ya walioumbwa na Mungu. Mwendo wa masaa 3-4. Na kinachoumiza zaidi road magari kama yote.

Nimewahi kulala nje siku moja baada ya kukosa kambi siku hiyo. Kuna broo mmoja ndo alikuwa akinichana live kuwa mimi sio mjanja ndio maana naishi kwa mdogo wangu. Sasa naishi kwangu, nina gari, pikipiki na nitafanya kitu kingine within this year.

Kuna vitu ukikumbuka unapata hudhuni sana.
Mbona sio mbali ukifika surenda bridge umefika osterbay kidogo umefika moroco kidogo umefika Victoria kidogo sayansi kidogo mwenge kidogo Makongo then unaitafuta goba [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ila mzee ulitembea kahhhh miguu haikuuma
 
Posta Goba haizidi 20k, unaona kama umetembea mbali sana?

Wamama huko vijijini wanatembea hadi 25kms kufuata maji kila siku kwenda na kurudi. Nenda singida watu wanatembea na punda 40km kwenda kutafta maji na kurudi.

Wasukuma huko Shinyanga wanatembea zaidi ya 50km kwenda minadani kuuza viazi ama mahindi ama pamba tenda wamejitwisha kichwani.

Posta Goba unaona mbali sana ndugu?
Huwezi kutembea km25 kwenda na kuludi kila siku ndugu yangu sikia tu habari yake,hapo ni wastani wa masaa 8 mpaka 6
 
[Qmiambili E="fundi25, post: 38166079, member: 136622"]
Bado pafupi apo!!
fundi25 Pafupi kama umeamkia Chapati tatu za mia mbili hamsini ama mia tatu na bakuli la maharage! Lakini umeamkia kashata na maji ya kufunga, ni parefu balaa!!!
[/QUOTE]
Duh umenikumbusha mbali sana kipindi hicho ninaishi mwana nyamala msisiri nina piga kashata na kahawa tatu chumba nilikuwa nina lipa kodi 3000 aisee acha nijikinge na korona nina toka mwana nyamala hadi Tandika masaa ma chache tu!
Kipindi hicho una nunua barafu unadumbukiza kwenye maji siku inapita barafu ya shilingi tano au kumi! Aisee nisalimie
 
Ha ha hahaa! Nilianzia Kinondoni Moscow kule chini karibu kabisa na mazalia ya mbu wa Muhimbili!! Baadaye nikaamishia "majeshi" Kisenvule, kodi 20,000 miezi mitatu! Sasa hapo uamue nani amsalimie mwenzake! Ha ha haaa!
 
Duh ulikuwa ushuwani mkuu yani 20, 000 ilikuwa kodi hangu ya miezi 6 na hapo nilihama mwana nyamala kwa kidile ulizia habari za hko nilikuwa ni lipa kwa mwezi 2000!
Na kwa kidile ni baada ya kutokea Buguruni Madenge!
Moscow nimekaa kwa mzee moja alikuwa anafuga mbwa karibia na machine ya kusaga miaka 28 iliyopita
 
We ulitembea kwa kukosa nauli wenzio wanatembea kutafuta ugali na ni kila siku ndio maisha yao.
Tumshukuru Mungu kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom