Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,318
- 8,464
Mimi na wife ni watumishi, wife ni mwalimu na mimi ni afisa manunuzi wa taasisi fulani, tulipoanza maisha hatukuwa na msaidizi wa kazi, ila tulipo barikiwa kupata mtoto wakwanza tuliona kuna haja ya kuwa na binti wa kutusaidia kazi za nyumbani.
Basi katika kutafuta tafuta siku moja nikaenda tabora kikazi, nilipo maliza majukumu niliuliza kwa wenyeji wangu wakaniambia sifa za ninaye mtaka nikawatajia, nilitamani awe na elimu angalau ya kidato cha nne.
Siku chache baadaye, rafiki yangu akanipigia na kuniambia kuwa amefanikiwa kupata mtu, baada ya kushauriana na wife tukaona nivema nimfuate, yaani asitumwe tu kwenye basi, Ijumaa nikawahi kutoka kazini nikarudi home, nikajiandaa kwa safari ya Tabora nikaingia barabarani, nakumbuka nililala Nzega kwenye lodge, asubuhi ya Jumamosi nikaelekea Tabora mjini, nikampitia yule rafiki aliye mtafuta, tukaelekea huko kijijini kwao.
Aisee nilivyomwona tu moyo ukalipuka, ila nikajikaza, mtoto alikuwa mzuri jamani, tukaongea na wazazi wake, baada ya kukubaliana kila kitu tukaanza safari, tukamwacha mshkaji Tabora sisi tukaendelea.
Sikuhiyo ilibidi nikeshe barabarani maana ningelala tu njiani tungezini😂 kwahiyo tulifika Moro kwenye saa 10 alfajiri jumapili, nikamfikisha nyumbani, kwakuwa tulikuwa tumechoka baada ya kuoga tulipumzika.
Jumapili tulishinda nyumbani na wife alishauri maelekezo ataanza kumpatia jumanne, kwahiyo jumatatu baada ya kutoka kazini nikamfuata, home tukaenda mjini kumtafutia simu, pia kufanya shopping ili aendane na familia yetu, badae niligundua alikuwa mchangamfu sana anapenda ku smile na mdadisi, kwakifupi nili enjoy kuzunguka naye sikuile.
Baada ya kurudi jioni wife akaniambia huyu binti kama asipo badilika huenda atarufaa sana maana leo amefanya kazi vizuri sana bila hata kuelekezwa, anahitaji kufahamu mambo machache tu aendelee, pia kwakuwa bado wife alikuwa na likizo ya uzazi alisema ataendelea kusaidiana naye mpaka azoee.
Kwakweli mtoto wa kinyamwezi anajituma, alitufurahisha sana hivyo kuna utaratibu tukamwekea ambao aliupenda na tumeendelea nao mpaka leo.
1. Mshahara wake tunalipa kila tarehe 24 na tunaweka kwenye account yake yeye anapata sms hivyo anakwenda kuchukua kiasi anachotaka muda anaopenda.
2. Tunamwekea fedha nyingine NSSF itakayo msaidia mbeleni.
3. Tulimpeleka driving school, ana leseni na kuna muda mfano tukiwa tunaenda kanisani huwa anadrive bila tatizo na anapenda.
4. Tumemtafutia hati ya kusafiria (passport) likizo moja tulikwenda naye Kenya ilipendeza sana.
5. Kila Weekend tunampokea kazi zote, yeye anapumzika japo mara chache sana anaweza toka na akiwa home huwa anatusaidia japo tumempa hiyo offer.
6. December ni likizo, nje ya mshahara wake tunampa nauli ya kwenda na kurudi kwao na bonus kwaajili ya zawadi za wazazi na wadogo zake.
7. Tumemnunulia kiwanja kiroho safi kabisa kwa jina lake eneo zuri kabisa hapa hapa Morogoro.
Matokeo: anafanya kazi zake vizuri sana, mwaka jana alituita akatuomba kumshauri awekeze wapi kwenye fedha alizo pata, nikamuuliza wewe ulifikiri kuwekeza wapi, akasema anataka kununua pikipiki na kumpa kijana kwa mkataba, tukabariki wazo lake akanunua TVS akampata kijana wa kanisani akamkabidhi.
Kijana anamletea marejesho vizuri kabisa na sehemu ya marejesho huwa anawatumia wazazi wake. Kifupi huyu binti ana akili sana, anawapenda watoto, anafanya kazi vizuri, changamoto alizo nazo ni za kawaida sana kwa mwanadamu, ana nidhamu, anapenda kazi pia.
Nadhani ndugu zangu kuna haja ya kubadili mtazamo kuhusu mabinti wa kazi, hebu tuishi nao kama watoto wetu wa kuzaa. KUNA BARAKA SANA KUFANYA HIVYO, MTABARIKIWA KAZINI, MAMBO YENU YATAENDA, BARAKA ZA WAZAZI WAO ZITAWAHUSU PIA.
Baada ya kupata matunda haya, tunataka tumtafutie chuo cha mambo ya marketing, akajinoe huko ili tumbadilishie kazi na kumpandisha daraja, then tujajua tunafanyaje kupata mwingine.