Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wakuu mtanisamehe sana kwa kuwarudisha nyuma mwaka 2015 kwenye uzinduzi wa bunge Jipya baada ya Uchaguzi Mkuu ambayo ilikuwa ndio siku ya kwanza kabisa kwa Rais mpya kulihutubia bunge hilo jipya na kulizindua.
Wabunge wote wa Upinzani waliotokana na (UKAWA) walitoka nje kama ishara ya kupinga kuingia ndani ya bunge hilo kwa Dr Shein ambaye aliangushwa kwenye uchaguzi ule na Jabali Maalim Seif na baadaye uchaguzi kufutwa.
Mpinzani pekee aliyebaki ndani ya bunge lile ambalo lilikuwa haramu baada ya kumuingiza Dr Shein kwa cheo cha Rais wa Zanzibar huku akiwa kaangushwa alikuwa Zitto Kabwe. Rais mpya kwenye Hotuba yake akamsifia sana Mh Zitto na kuwaponda wapinzani wote kwa mamia waliomsusia.
Si lengo langu kwa leo kumjadili Zitto Kabwe , maana yaliyopita si ndwele lengo langu ni kuushuhudia msemo wa kweli wa wahenga usemao kwamba " Shetani hana rafiki "
Zitto Kabwe ambaye kwa wakati ule aliunga mkono CCM bungeni , leo CCM ileile aliyoiunga mkono inaitisha kikao ili pamoja na mambo mengine itenge fedha kwa lengo la kuwanunua madiwani wote wa ACT WAZALENDO popote walipo nchini Tanzania , leo wale aliowaunga mkono wamemgeuka ! pamoja na kumpoteza Kanguye lakini bado hawajatosheka , wanamuwinda yeye mwenyewe kama digidigi!
Kwahiyo, kuanzia sasa ni vema maandiko tunayoyaweka humu yasipuuzwe , Shetani ama wakala wake hapaswi kuungwa mkono imeandikwa kwenye vitabu vyote vya dini , haya yanayoendelea nchini Tanzania ni mipango ya Mwenyezi Mungu kuwathibitisha walimwengu kwamba Neno lake liko hai na linaishi.