Ushuhuda: Tunaposema Shetani hana rafiki hatudanganyi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakuu mtanisamehe sana kwa kuwarudisha nyuma mwaka 2015 kwenye uzinduzi wa bunge Jipya baada ya Uchaguzi Mkuu ambayo ilikuwa ndio siku ya kwanza kabisa kwa Rais mpya kulihutubia bunge hilo jipya na kulizindua.

Wabunge wote wa Upinzani waliotokana na (UKAWA) walitoka nje kama ishara ya kupinga kuingia ndani ya bunge hilo kwa Dr Shein ambaye aliangushwa kwenye uchaguzi ule na Jabali Maalim Seif na baadaye uchaguzi kufutwa.

Mpinzani pekee aliyebaki ndani ya bunge lile ambalo lilikuwa haramu baada ya kumuingiza Dr Shein kwa cheo cha Rais wa Zanzibar huku akiwa kaangushwa alikuwa Zitto Kabwe. Rais mpya kwenye Hotuba yake akamsifia sana Mh Zitto na kuwaponda wapinzani wote kwa mamia waliomsusia.

Si lengo langu kwa leo kumjadili Zitto Kabwe , maana yaliyopita si ndwele lengo langu ni kuushuhudia msemo wa kweli wa wahenga usemao kwamba " Shetani hana rafiki "

Zitto Kabwe ambaye kwa wakati ule aliunga mkono CCM bungeni , leo CCM ileile aliyoiunga mkono inaitisha kikao ili pamoja na mambo mengine itenge fedha kwa lengo la kuwanunua madiwani wote wa ACT WAZALENDO popote walipo nchini Tanzania , leo wale aliowaunga mkono wamemgeuka ! pamoja na kumpoteza Kanguye lakini bado hawajatosheka , wanamuwinda yeye mwenyewe kama digidigi!

Kwahiyo, kuanzia sasa ni vema maandiko tunayoyaweka humu yasipuuzwe , Shetani ama wakala wake hapaswi kuungwa mkono imeandikwa kwenye vitabu vyote vya dini , haya yanayoendelea nchini Tanzania ni mipango ya Mwenyezi Mungu kuwathibitisha walimwengu kwamba Neno lake liko hai na linaishi.
 
Mpeni salaam, habari zake tunazo. Nyumba yake imebomoka atalala wapi
 
Kwa hii biashara mpya ya chama tawala kupanga mikakatii na kutenga fedha za kuwahadaa na hatimaye kuwanunua viongozi kutoka vyama vikuu vya upinzani ni jambo la kuogofya sana.

Na tena uamuzi huu kufanyika kupitia ajenda zinazopitishwa ndani ya Sekretariate ya Kamati Kuu ya chama. Kweli! Hivi inaingia akilini kabisa watu wenye dhamana ya kuiendesha nchi yetu kujifungia ktk kuta nne, tena chini ulinzi mkali ili kupitisha uamuzi kama huu!

Hivi kweli vituko na vioja hivi vinafanyika hata ktk nchi nyingine makini? Kuna kila haja ya kupima afya ya akili za viongozi wetu ambao wanaweza kuaminika kubeba jukumu kubwa lenye kutuhakikishia hatma ya mamilioni ya Watanzania.

Isije ikawa tuna idadi kubwa ya wadau wa hospitali ya Milembe ambao kwa makosa tumeweza kuwabebesha jukumu ambalo ambalo si lao, na kamwe hawataweza kulibeba, na kuishia kuendelea kutufanyia vituko na vioja kutokana na woga wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu 9th December 2019 Zitto anasusia huku CDM wakienda kujipendekeza CCM Kirumba kutaka urafiki na shetani aliyetoka "kuvuruga" uchaguzi wa serikali za mtaa.

Wote ni walewale tu tofauti ni rangi ya "matambara" mnayopeperusha!

Mnalalamika hakuna Uhuru halafu mnaenda kusherekea siku ya Uhuru upi?
 
Lakini hapa shetani ni zitto na kihere chake alifikiri Magu ni Kikwete akataka kujipendekeza alipoona milango imefungwa akijifanya sasa mkali wacha yamkute

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu 9th December 2019 Zitto anasusia huku CDM wakienda kujipendekeza CCM Kirumba kutaka urafiki na shetani aliyetoka "kuvuruga" uchaguzi wa serikali za mtaa.

Wote ni walewale tu tofauti ni rangi ya "matambara" mnayopeperusha!

Mnalalamika hakuna Uhuru halafu mnaenda kusherekea siku ya Uhuru upi?
nje ya mada
 
Hizi mambo za kwenda ughaibuni kufanya udalali chama unamuachia Abdul Mondo, utalizwa muda si mrefu. Zitto rudi nyumbani kumenoga😀😆
 
Na tena uamuzi huu kufanyika kupitia ajenda zinazopitishwa ndani ya Sekretariate ya Kamati Kuu ya chama. Kweli! Hivi inaingia akilini kabisa watu wenye dhamana ya kuiendesha nchi yetu kujifungia ktk kuta nne, tena chini ulinzi mkali ili kupitisha uamuzi kama huu!
Kama ni kweli, mpango huu upo na unafanyika ndani ya chama cha CCM, chama hiki na viongozi wake wote watakuwa wapapambanaji wa rushwa?

Hili tu ndilo swali mhimu kwangu, na pengine wengi wengine.

Jambo hili pia tunaweza tukalipeleka mbele zaidi ya hapo; kwamba, akitokea mwanachama/kiongozi huko upinzani akawa hanunuliki kwa bei yoyote, na nafasi yake ikaonekana ni tishio kwa chama hiki cha CCM, itakuwa ni ruhusa kumwondosha kwa njia yoyote hata mauti?
Hii ndio tafsiri pekee inayoweza ikafanyika katika hali ya namna hii.
 
Ushajulikana ww ni wa aina gani... Eti nje ya mada...Uzi hadhi imeshuka sasa coz ni unafiki tu.
Sitaki kuchanganya mada , na ndio maana hata kwenye uzi nimesema sitaki kuonekana namshutumu Zitto , bali nimemtaja Zitto humu ili kuweka ushahidi halali wa andiko langu , kwahiyo usiniburuzie unakopenda wewe .
 
Kama ni kweli, mpango huu upo na unafanyika ndani ya chama cha CCM, chama hiki na viongozi wake wote watakuwa wapapambanaji wa rushwa?

Hili tu ndilo swali mhimu kwangu, na pengine wengi wengine.

Jambo hili pia tunaweza tukalipeleka mbele zaidi ya hapo; kwamba, akitokea mwanachama/kiongozi huko upinzani akawa hanunuliki kwa bei yoyote, na nafasi yake ikaonekana ni tishio kwa chama hiki cha CCM, itakuwa ni ruhusa kumwondosha kwa njia yoyote hata mauti?
Hii ndio tafsiri pekee inayoweza ikafanyika katika hali ya namna hii.
CCM haijawahi kupambana na Rushwa mahali popote
 
Sitaki kuchanganya mada , na ndio maana hata kwenye uzi nimesema sitaki kuonekana namshutumu Zitto , bali nimemtaja Zitto humu ili kuweka ushahidi halali wa andiko langu , kwahiyo usiniburuzie unakopenda wewe .
Sawa nimekupata ila keep in mind ulichoambiwa
 
Wakuu mtanisamehe sana kwa kuwarudisha nyuma mwaka 2015 kwenye uzinduzi wa bunge Jipya baada ya Uchaguzi Mkuu ambayo ilikuwa ndio siku ya kwanza kabisa kwa Rais mpya kulihutubia bunge hilo jipya na kulizindua.

Wabunge wote wa Upinzani waliotokana na (UKAWA) walitoka nje kama ishara ya kupinga kuingia ndani ya bunge hilo kwa Dr Shein ambaye aliangushwa kwenye uchaguzi ule na Jabali Maalim Seif na baadaye uchaguzi kufutwa.

Mpinzani pekee aliyebaki ndani ya bunge lile ambalo lilikuwa haramu baada ya kumuingiza Dr Shein kwa cheo cha Rais wa Zanzibar huku akiwa kaangushwa alikuwa Zitto Kabwe. Rais mpya kwenye Hotuba yake akamsifia sana Mh Zitto na kuwaponda wapinzani wote kwa mamia waliomsusia.

Si lengo langu kwa leo kumjadili Zitto Kabwe , maana yaliyopita si ndwele lengo langu ni kuushuhudia msemo wa kweli wa wahenga usemao kwamba " Shetani hana rafiki "

Zitto Kabwe ambaye kwa wakati ule aliunga mkono CCM bungeni leo CCM inaitisha kikao ili pamoja na mambo mengine itenge fedha kwa lengo la kuwanunua madiwani wote wa ACT WAZALENDO popote walipo leo wale aliowaunga mkono wamemgeuka pamoja na kumpoteza Kanguye lakini hawajatosheka , wanamuwinda yeye mwenyewe kama digidigi!

Kwahiyo, kuanzia sasa ni vema maandiko tunayoyaweka humu yasipuuzwe Shetani ama wakala wake hapaswi kuungwa mkono imeandikwa kwenye vitabu vyote vya dini haya yanayoendelea nchini Tanzania ni mipango ya Mwenyezi Mungu kuwathibitisha walimwengu kwamba Neno lake liko hai na linaishi.
Ngoja tuone safari hii kama bado atakosa rafiki
 
Back
Top Bottom