Ushuhuda wa familia yetu: Nguvu kubwa itumike kuwafundisha watoto kujitegemea ili wasisote kama sisi wahitimu wa vyuo

Nachoamini ni kwamba mtu hujifunza mambo ambayo yanadumu kichwani pindi awapo chini ya miaka 18.

Ni mda huu wengi wanakazania watoo kushika namba moja shuleni, matuisheni hadi weekend, kuwapelekea watoto shule za boarding kwa fasheni, kupiga watoto wasipofanya vizuri darasani, n.k Hali hii inamfanya mtoto awe anajua elimu ya darasani tu, kimbembe kinaanza mtoto kamaliza chuo na lafaulu vizuri tu lakini ndio hivo tena kupata kazi sikuhizi ni ngumu sana.

Binafsi kwa sasa navyolea watoto wangu, moja yupo shule ya msingi ila namlea nikiwa na taswira kwamba akimaliza chuo atakosa ajira japo siombei iwe hivi ila ni kuangalia uhalisia, Najitahidi na ntajitahidi kadri niwezavyo awe na ujuzi katika mambo mbali mbali yatayomsaidia hata akikosa ajira,
 
Coaster alinunua kwa kukopa au shughuli hizo hizo za kinyozi?
Mkuu hata sina uhakika, ila nakumbuka kile kipindi biashara alizokua anafanya nilizozijua mimi ni kuwa kinyozi na kuchezesha hii michezo ya video ambayo ilimwingizia pesa nzuri tu kila siku.
 
Mtaji alipata wapi boss?
Alianza nishingapi kwanza??
 
This is a great testimony ever! I think wakuu, mindsets zetu zibadirike, zama zimeshabadirika. Saizi ajira ni chache ukilinganisha na nambe ya wahitimu wanaomaliza kila mwaka. So, self-employment matters a lot.
 
Bora ufanye Ivo mkuu!!

Pia usisahau na kumpeleka kusoma course hot cake za kompyuta km graphic design n.k

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Huyu Jamaa aliyeleta uzi haelezei vizuri hii issue
Mtaji wa kuanzia saloon bro wako alipata wapi?
 
Mtaji alipata wapi boss?
Alianza nishingapi kwanza??
Huyu Jamaa aliyeleta uzi haelezei vizuri hii issue
Mtaji wa kuanzia saloon bro wako alipata wapi?
Mkuu biashara ya kinyozi sidhani kama mtaji wake ni wa kutisha kusema kwamba unazidi hata milioni.

Frem aliyokodi ya kawaida sana, alikuwa na ujuzi tayari wa kunyoa, viti, kioo, mashine niliona kama vimeshatumika huenda alinunua kwa mtu maana nae alikuwa anayajua haya mambo ya kinyozi kwa mda mrefu tangu sekondari.

Sijajua alipopata mtaji lakini ni mtaji wa kawaida tu maana ilikuwa saloon ya kawaida sana
 
blessed
 
Siamini mtu kwenye mwandiko mzuri Kama wewe ukose ukizi....
 
Hongereni mnaupendo Sana
Ahsante
 
Tukiachana na fashion na kufuata mkumbo ushauri mzuri ni huu:

Kama hutaki kuwa daktari basi Ukishajua kusoma na kuandika, ukajua kujumlisha na kutoa nenda kaitafute elimu itakayokupatia fedha kwa sababu hata wenye elimu za juu kabisa wakishazipata hizo elimu watarudi chini kuitafuta elimu itakayowapatia fedha au wakaajiriwa na wewe.
 
Hivi kuchanganya perfume nao ni ujuzi eeh!!?

Kama ndiyo..tafuta wale wanaochanganya wakufundishe utafute kamtaji uanze kusaka pesa.. perfume za kupima zinalipa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…